KUTOKA VIWANJANI
Jana
zilichezwa mechi za ligi ya Parokia ya Boko maarufu kama Majeta cup,
mechi ambayo ilikuwa na msisimko mkubwa ilikuwa kati ya Bunju na Mbweni
iliyochezwa katika uwanja wa Mbweni, majigambo yalikuwa mengi kabla ya
mechi ,mvuto mkubwa ukiwa kwa makocha wa timu hizo ndg James Nkii kocha
wa timu ya Bunju, na ndg Fabian Masanja kocha wa timu ya Mbweni. mpira
ulikiwa upo sawa kwa timu zote mpaka wakati wa mapumziko timu hizi
zilikuwa hazijafungana, kipindi cha pili kilianza kwa nguvu sana, huku
kila timu ikifanya mabadiliko ambayo kwa upande wa mbweni, yalizaa
matunda kwani walipata magoli wawili ya haraka, dakika chache kabla
mpira kuisha bunju nao waliamkaa na kupata goli moja la kufutia machozi
mwisho wa mpira matokeo yalikuwa Mbweni 2 na Bunju 1
No comments:
Post a Comment