Somo La Kwanza: Ufunuo.7:2-4, 9-14
Wimbo Wa Katikati: Zaburi: 24:1-6 (K) 6
Somo La Pili: 1 Yoh. 3:1-3
Injili: Mathayo 5:1-12
Sikukuu ya Watakatifu wote
Kalenda ya Kanisa Katoliki inajumuisha sikukuu za watakatifu wengi na
hata wafia dini. Lakini Novemba mosi, ni sikukuu ya watakatifu wote.
Kweli tunasherehekea sikukuu za watakatifu fulani fulani katika siku
tofauti lakini Novemba Mosi, tunasherehekea sikukuu ya watakatifu wote,
wale tunaowajua na wale tusiowajua. Watakatifu ni wengi na wamefanya
kazi nyingi tofauti tofauti lakini zote zikiwa na umuhimu wake katika
kuiendeleza na kuikuza imani yetu. Watakatifu ni wengi na hatuwezi
kuwajua wote. Hivyo sikukuu hii inawajumuisha pamoja kama kundi moja la
watu walioyaishi maisha yao vyema hapa duniani. Sikukuu hii ni kichocheo
katika maisha yetu ya imani kwani inatubidi tufuate nyayo zao, tuishe
tukimtegemea Mungu zaidi ya chochote. Watakatifu walio pamoja na Mungu
mbinguni wanatuombea na kutupa moyo sisi watakatifu tulio safarini
kwenda mbinguni. Watakatifu tunao sherekea siku yao leo ni mashujaa wa
imani na kielelezo kwetu, wanatupa moyo kuwa, “Ndiyo kumfuata Kristo
kunawezekana.” Kesho Novemba mbili tutawakumbuka marehemu wote. Hawa ni
ndugu zetu, wasafiri wenzetu ambao tayari wameiacha dunia hii lakini
bado hawajafika mbinguni, wanavikwa mavazi meupe (Ufu.7:9) wanatakaswa
kabla ya kuingia mbinguni
Sherehe ya watakatifu wote inatukumbusha
kuufuata wito wetu wa kuwa wana wa Mungu. Baada ya mwanadamu kuupoteza
utu wake kwa kutenda dhambi, Mungu alimtuma mwanae ulimwenguni ili wale
wote wamuaminio wapate ufalme wa milele (Yn. 3:16). Watakatifu
wameshaupata ufalme huu wa milele ni wajibu wetu sisi wakristo kufuata
mfano wao. Wao walishinda adui wa roho kwa kutumaini neema za Mungu.
Injili
ya leo inatuonesha furaha ya watakatifu ilivyo, na njia inayotuwezesha
kufika kufika mbinguni. Tunasikia kwamba, “Heri walio maskini wa roho;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Kumbe basi, tukitaka vita vya miaka
michache hapa duniani vitatuletea furaha na heri ya milele. Inatubidi
basi tuvumilie kabisa katika imani yetu, tujaribu kila tuwezavyo
tuvishinda vishawishi kwani Mungu hatajaribu zaidi ya neema aliyotupa
kuvishinda vishawishi hivyo. Watakatifu tunaowakumbuka leo, wanatupenda
wanatuombea kwa Mungu ili tuwe pale walipo, karibu na Mungu na kwenye
heri ya milele. Sikukuu hii haina budi kuamsha matumaini makubwa
mioyoni mwetu.
Sala:
Ee Mungu niongezee kiu na njaa ya kuyafanya mapenzi yako na
siku moja niwe pamoja na watakatifu mbinguni tukikusifu na kuiombea
dunia.
Amin
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
No comments:
Post a Comment