Tuesday, February 26, 2013

HISTORIA YA UJENZI WA KANISA LA MBULU

Shujaa wetu: Franz Wesinger-Mhandisi aliyejenga kanisa Katoliki Mbulu

  Kanisa la Mbulu ndilo kanisa kubwa kuliko yote Tanzania na la pili kwa ukubwa Afrika Mashariki kanisa hili lilijengwa na   Mhandisi Franz Wesinger aliyezaliwa mwaka 1928 huko Bavaria Ujerumani.
Mwaka 2003, akiwa na miaka 75 mhandisi Franz Wesinger ambaye pia ni msanifu wa majengo alirudi Tanzania kwa ajili ya kupanga ujenzi wa kanisa jipya la Katoliki Arusha na ni katika kipindi hicho ambacho mapadre wawili wa kanisa Katoliki jimbo la Mbulu walikumbwa na kashfa ya ufisadi kama baada ya kufuja jumla ya Shilingi za Kitanzania Milioni 340 kwa bei ya 1000 kubadili dola moja wakati huo  (dola 340,000). Mapadre hao, msaidizi wa askofu (Vicar General) John Nada na father Melkiadus Qameyu wa parokia ya Dareda walituhumiwa kupoteza kiasi hicho cha fedha baada ya kutapeliwa na mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Mohamed mrisho kuwa angeziongeza mara mbili....mafaza wakaingia mkenge...
Turudi kwa Franz Wesinger, huyu bwana alifanya mahojiano na gazeti la Arusha Times mwaka 2003 na haya ni sehemu ya maelezo yake kuhusu ujenzi wa Kanisa hilo
"Katika miaka 15 iliyopita, Jimbo la Mbulu limepiga hatua kubwa sana. Jitihada za awali za marehemu Askofu Hhando zimezaa matunda kwani walianza kidogo au kusema ukweli halisia walianza bila fedha lakini waliweka imani yao kwa Mungu huku wakitumia msaada kidogo kutoka kwa wamihionari kutoka Ulaya na ujenzi ulianza. Amini usiamini, walianza ujenzi wakitumia sepetu lililovunjika na toroli la mbao. Kanuni kuu ilikuwa kubana matumizi na kuhudumu (huduma) pamoja kukawa kichocheo kikubwa katika jimbo zima kumtumikia Mungu" alisema Franz
"Hata baada ya ujenzi na kanisa kuwekwa wakfu zilibaki kontena 12 zikiwa zimejaa vifaa vya ujenzi, mashine, magenerata, jukwaa kubwa, magari mawili na lifti (cranes) bila kutumika"
"Kuna tofauti kati kuhudumu kwa imani na kutumaini kupata faida pasipo kufanya kazi" aliongeza Franz akizungumzia ufisadi uliotokea Mwaka moja baada ya ujenzi wa kanisa hilo kukamilika.
"Hata wana wa Israeli walimsahau Mungu na kuabudu ndama wa dhahabu baada ya Mungu kuwatoa utumwani mwa Wamisri na kuwapitisha katika bahari ya Shamu"
"Waisraeli walikombolewa lakini walitaka kupata faida pasipo kufanya kazi, hauwezi kumtumikia Mungu kwa ulanguzi"
Franz Wesinger alieleza kuwa anajisikia fahari kubwa sana moja ya sehemu maskini zaidi Tanzania ina Kanisa kubwa zaidi na zuri zaidi nchini na kuona fahari kuwa imejenga hilo kanisa lenyewe kwa msaada pekee wa Mungu"
Chini ya usimamizi wa Franz Wesinger ujenzi wa kanisa hili ambalo leo ni fahari kubwa kwetu ulikamilika kwa ufanisi wa hali ya juu na kutimiza ndoto ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo Kuu la Mbulu Marehemu Hhando. Franz Wesinger anatoa funzo la uaminifu na kuacha "legacy" kwa vizazi vijavyo. Sina uhakika kama bado yupo hai lakini Franz Wesinger alifanya kazi kubwa sana tofauti na "wahandisi" wetu ambao ninauhakika kisingebaki kitu baada ya ujenzi na katu kazi ya ujenzi wa kanisa hilo usingekamilika.
 

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR