22
|
JUNI
JUMAPILI YAMWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTU
MWAKA "A" 2014
MWAKA "A" 2014
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI
Zaburi: tazama sala ya siku
Zab:147:12-15. 19-20
K. Msifu Bwana, Ee Yerusalemu
SOMO 1:Kum.8:2-3, 14-16a
Musa aliwaambia makutano:
Utaikumbuka
njia ile yote Bwana, Mungu wako, aliyokuongoza miaka hii arobaini katika
jangwa, ili akutweze, kukujaribu, kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika
amri zake, au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana.
Usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu
haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana.
Basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, uliyekutoa katika
nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa
lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji;
aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, aliyekulisha jangwani kwa mana,
wasiyoijua baba zao.
SOMO 2:1Kor. 10:16-17
Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa
damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa maana
sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
INJILI: Yn.6:51-58
Yesu aliwaambia Wayahudi:
Mimi ndimi
chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki,
ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima
wa ulimwengu. Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu
kutupa sis mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia, Amin, Amin, nawaambieni,
msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani
yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu
yangu anao uzima wa milele; name nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili
wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili
wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, name hukaa ndani yake. Kama vile
Baba aliye hai alivyonituma mimi, name ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye
kunila atakuwa hai kwa mimi. Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si
kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
No comments:
Post a Comment