28
SEPTEMBER
JUMAPILI YA 26 YA MWAKA "A" 2014.RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHISOMO 1. Eze. 18:25-28
Bwana ameniambia hivi: Ninyi mwasema; Njia ya Bwana ni sawa. Sikilizeni sasa, Enyi nyumba ya Israeli; je! njia yangu siyo iliyo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa? Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, atakufa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa. Tenamtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai. kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.
SOMO 2. Flp. 2:1-11
Ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, mwenye mapenzi mamoja, mwenye Roho moja, mkinia mamoja. Usitende neon lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa na bora kuliko nafsi yake. kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo yake mwenyewe. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa binadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
INJILI.Mt. 21:28-32
Yesu aliwaambia wakuu wa makuhanina wazee, Mwaonaje? mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, mwanangu, leo nenda kafanya kazi katika shamba la mizabibu. Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akijibu akasema, sitaki; baadaye akatubu, akaenda. je! katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin, nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Matangazo
jiandaye na Kongamano la ujirani kati ya Parokia ya Boko na bunju' mwema, nunue Ticketi yako sasa kwa Tshs 18,000. Kongamano litafanyika kuanzia tarehe 28-29/11/2014, Parokiani Boko w
No comments:
Post a Comment