Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana
Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenela Mukangara kuomboleza kifo
cha aliyekuwa Mtangazaji na Mwandishi Mkongwe na Mahiri hapa nchini wa
iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo kwa sasa ni TBC
Taifa, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko.
Ben Kiko
amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 31 Oktoba, 2014 katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa
akiendelea na matibabu ya figo baada ya kuhamishiwa hapo akitokea
Hospitali ya Jeshi ya Milambo Mkoani Tabora. “Nimeshtushwa,
nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha
Mwanahabari na Mtangazaji huyu Mahiri ambaye ametoa mchango mkubwa wa
kihabari kwa Taifa letu”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba wa Ben
Hamis Kikoromo.
“Namkumbuka Marehemu Ben Kiko, enzi za uhai wake,
kama Mtangazaji aliyekuwa na mvuto mkubwa kwa wasikilizaji wake
kutokana na namna yake ya kipekee ya kuripoti matukio hususan katika
kipindi kilichojizolea umaarufu mkubwa wakati huo cha MAJIRA kilichokuwa
kikirushwa hewani na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD)”.
Wakati
wa vita dhidi ya Nduli Idi Amin wa Uganda mwaka 1978, Ben Hamis
Kikoromo alifanya kazi kubwa kwa Taifa kwani aliweza kuripoti matukio
mbalimbali kutoka katika uwanja wenyewe wa vita, na hivyo kuliwezesha
Taifa na wananchi kwa ujumla kuhabarika vilivyo na matukio yaliyokuwa
yakiendelea.
“Kutokana na msiba huu mkubwa, pokea salamu zangu
za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza mmoja wa
Waandishi na Watangazaji Mahiri katika Tasnia ya Habari hapa nchini.
Vilevile
kupitia kwako, naomba Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi
ziifikie Familia ya Marehemu Ben Hamis Kikoromo kwa kupoteza Kiongozi na
Mhimili Madhubuti wa Familia. Nawaomba Wanafamilia wote, ndugu na Jamaa
wa Marehemu wawe wavumilivu na wenye subira wanapoomboleza kifo cha
mpendwa wao huku wakitambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola”, amesema
Rais Kikwete.
Amewahakikishia Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao
katika muda wote wa maombolezo, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa
Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu Ben Hamis
Kikoromo, Amina.
Aidha Rais Kikwete ametuma Salamu za Rambirambi
kwa Wanahabari kote nchini ambao kwa hakika msiba wa Ben Kiko utakuwa
umewagusa kwa karibu. Hata hivyo amesema kuondoka kwa Ben Kiko kusiwe
chanzo cha wao kukata tamaa, bali kifo chake hakina budi kuwa chachu
katika kujituma zaidi, na wawe tayari kuiga yote mazuri aliyoyafanya
Marehemu enzi za uhai wake hapa duniani hususan katika Taaluma ya
Uandishi wa Ha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
No comments:
Post a Comment