Saturday, January 24, 2015

MASOMO YA TAREHE 25/01/2015 jumapili ya 3 ya mwaka B wa kanisa

25

Januari

 Jumapili: Dominika ya 3 ya Mwaka "B".
SOMO  1. Yon. 3:1-5, 10

 Neno la bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, ondoka uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukaihubiri habari nitakayo kuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikua mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu, Yona akaanza kuingia mjini mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.

    Read More...                                                                      



somo 2. 1Kor. 7:29-31. 

Somo katika Waraka wa kwanza wa mtume Paulo kwa Wakorintho

Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana; na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii  sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.
.

  INJILI.Mk. 1:14-20
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Marko.
Hata baada ya Yohane kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri habari Njema ya Mungu, akisema, wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribi; tubuni na kuiamini Injili. Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikua wavuvi. Yesu akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa zebedayo, na Yohane nduguye, nao pia walikua chomboni, wakizitengeneza nyavu zao. Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR