Friday, February 27, 2015

Masomo ya Jumapili ya Pili ya Kwaresima Mwaka B (Tarehe 01/03/2015)

01

 Marchi
 Jumapili ya 2 ya Kwaresima Masomo ya Mwaka "B".
SOMO  1: Mwa. 22:21- 2, 9a, 10-13, 15-18

Somo katika kitabu cha Mwanzo.
Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Uchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya Kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia. Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu. Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee. Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, Kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketeza badala ya mwanae. Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni, akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga uliopo pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote duniani watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

WIMBO WA KATIKATI. Zab. 116:10, 15-19. 
K. Nitaenenda mbele za Bwana
         Katika nchi za walio hai..

read more....
SOMO  2: Rum. 8:31b - 34
Somo katika Waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Warumi.

Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake  mwenyewe, Bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Ni  nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea..
  INJILI.Mk. 9:2-9.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Marko.
Yesu akamtwaa Petro, na Yakobo na Yohane, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao; mavazi yake yakimeta- meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe. Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu, Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa na kimoja cha Eliya. Maana hakujuala kunena,kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi. Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, huyu ni mwanangu, mpendwa wangu,msikieni yeye. Mara hiyo walipotazama hku na huku, hawakuona mtu pamoja nao ila Yesu peke yake. Na walipokuwa wakishuka mlimani aliwakataza wasimweleze mtu aliyoyaona, hata Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR