Wednesday, March 25, 2015

Masomo ya Jumapili ya Tano ya Kwaresima Mwaka B wa Kanisa tarehe 22/03/2015

22

 Marchi
 Jumapili ya 5 ya Kwaresima Masomo ya Mwaka "B".
Mwanzo

Ee Bwana Mungu wetu, tunakuomba utusaidie tuwe na mapendo kama ya mwanao, aliyeipenda dunia hata kujitoa auawe. tunaomba hayo kwa njia ya Bwana.........
SOMO  1: Yer. 31:31- 34
Somo katika kitabu cha Nabii Yeremia.
  Angalia siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. si kwa mfano wa agano lile nililofanya na Baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
  Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
  Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; ,maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.

WIMBO WA KATIKATI. 
Zab. 19:7-10. 
Kiitikio. Ee Mungu, uniumbie moyo safi..

read more....
SOMO  2: Ebr. 5:7-9
Somo katika Waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Waebrania.

  Yesu, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na ingawa ni mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.
  INJILI.Yn. 12:20-33.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Yohane.
  Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikuku. Basi hao walimwendea filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu, Filipo akaenda akamwambia Andrea; Kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.
  Naye Yesu akawajibu, akasema, saa imefika atukuzwe mwana wa Adamu. Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake, bali ikifa hutoa mazao mengi. Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu. Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo niliyoifikiria saa hii. Baba, ulitukuza jina lako.
   Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa na ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye. Yesu akajibu akasema, sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu, Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
  Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR