Wednesday, December 31, 2014

Masomo ya jumatano tarehe 31/12/2014

Jumatano, 31 Desema 2014
Jumatano katika Octava ya Kuzaliwa Bwana

1Yoh 2:18-21;
Zab 95: 1-2, 11-13;
Yn 1: 1-18

Jibu katika Neno la Mungu

Dibaji ya Injili ya Yohane ni nyimbo nzuri inayoimba juu ya simulizi ya Krismasi, fumbo la Umwilisho. Kutoka katika ufahamu huu wa binafsi wa kuishi na Kristo, Yohane alikuwa ameshawishika kwa kina sana kuwa Yesu ndiye Neno, Aliyekuwako tokea mwanzo pamoja na Mungu, Aliyekuwa mwili na kukaa kwetu. Andiko hili tukufu linatoa muunganiko wa imani ya Kikristo. Ukristo sio dini ya kitabu bali ni dini au neno la Mungu, sio neno lililoandikwa na lisilo nena, bali ni ya umwilisho na Neno liishilo. Kwahiyo, hususani katika Adhimisho la Ekaristi, wakati habari njema inapohubiriwa, ni Kristo Mwenyewe ndiye anayehubiri kupitia watumishi wake, wakitafuta jibu sawa la imani ipendwayo ambayo Yeye aliomba kwa wale wote ambao Aliwahubiria katika Palestina. Na kanisa ni katika kiini chake cha ndani, jumuiya ya wale wote wanaosikia neno la Mungu na kulizingatia. Swali ni, je, kama wanajumuiya wa hii jumuiya ya imani inayosikiliza, je, ni namna gani tunajibu?  Je, daima tupo tayali kujifungua wenyewe katika neno la Mungu namapenzi yake kwetu sisi? Au tunajikuta sisi wenyewe hatupendi, tusio badilika kutokana na nguvu ya neno la kubadilisha, isiyoenda kutokana na tofauti ya neema iletwayo?

Sala: Bwana, tuongoze katika upendo mkuu wa neno lako na tutie nguvu ya unyenyekevu katika kujibu na kutii imani. Amina.

"Amri ya maisha ya kikristo itaonekana si katika kitabu kilichoandikwa, ball ni katika tendo la binafsi la Roho Mtakatifu mwenye kumsukuma na kumwongoza Mkristo. Ni "sheria ya Roho ya uhai wa Kristo Yesu". "Maana Mungu amekwisha miminia mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia". Jambo hili ni kweli pia kwa raume na mke wakristo na famllia ya klkrlsto. Mwongozo na sheria ya maisha yao ni Roho wa Yesu aliyemiminwa ndani ya mioyo yao katika adhimisho la sakramenti ya Ndoa. Katika mfululizo pamoja na Ubatizo katika maji na Roho, ndoa huweka upya sheria ya kiinjili ya upendo, na pamoja na zawadi ya Roho, hukaza zaidi katika mioyo ya waume na wake Wakristo. Upendo wao ukisafishwa na kuokolewa, ni tunda la Roho mwenye kufanya kazi katika mioyo ya waumini na kufanyiza, wakati huo huo, amri ya msingi ya maisha katika uhuru wa kimadaraka." – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 63.

VIWAWA BOKO
www.viwawaboko.blogspot.com

Tuesday, December 30, 2014

masomo ya tarehe 30/12/2014

Jumanne, 30 Desemba 2014
Jumanne katika Octava ya Kuzaliwa Bwana

1 Yoh 2:12-17;
Zab 95: 7-10;
Lk 2: 36-40

Kuitwa kuwa Watakatifu

Katika Injili Yesu anatamka kuwa yeye pekee anamfahamu Baba. Ni Neno la Mungu ndilo linaufanya ujio wake mioyoni mwetu, ndilo linalomfanya Yeye afahamike mioyoni mwetu. Jibu letu sio tu kushinda ovu, bali katika hali chanya kutembea katika njia ya utakatifu. “watakatifu sio watu wakubwa sana, wala hawakuzaliwa wakamilifu. Wapo kama sisi, kama kila mmoja wetu … je, nini kiliyabadilisha maisha yao? Walipo utambua upendo wa Mungu, waliufuata kwa moyo wao wote bila ya kubakiza wala bila ya unafiki” – Papa Fransis. Utakatifu sio upendeleo wa watu wachache, wa wale wote wanaovaa kanzu au kiremba, bali pia wale wote wenje majinsi na viatu vya tennis; ni wa wale wote wanaokwenda katika filamu, wanaosikiliza muziki, wanaotumia muda wao na marafiki zao. Lakini wote wanahitaji kumpatia Mungu nafasi ya kwanza, awe mbele ya kazi zao, familia zao, na marafiki zao. Tunawahitaji watakatifu wanaotafuta muda kwa ajili ya kusali kila siku na wanaojua namna ya kuwa katika upendo na usafi, useja, na mambo yote mema. Tunawahitaji watakatifu walio na moyo wa kujitolea katika kuwasaidia masikini na kuyafanya mabadiliko yanayohitajika katika jamii.

Sala: Bwana, tupe busara ya kuishi katika ulimwengu lakini si kujikita sisi wenyewe katika hali yake. Amina.

"Kusudi kubwa la sala ya kanisa la nyumbani ni kuhudumia kama utangulizi wa kiasili kwa ajili ya watoto kuwa sala ya kiliturjia ya Kanisa zima, katika maana ya kuifanyia maandalizi na kuieneza katika maisha ya binafsi, familia na kijamii. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kushiriki kwa wanajumuiya wote wa familia ya Kikristo katika adhimisho la Ekaristi, hasa siku za Jumapili na sikukuu, na masakramenti mengine, hasa sakramenti za kuingizwa watoto katika Ukristo. Miongozo ya Mtaguso Mkuu ilifungua wajibu Mpya kwa familia ya kikristo ilipoorodhesha familia kati ya vikundi vile ambavyo ilipendekeza kusali sala ya Kanisa kwa pamoja. Kwa namna hiyo hiyo, familia ya Kikristu itakazana kuadhimisha nyumbani, na kwa namna inayofaa kwa wanajumuiya wake, nyakati na sikukuu za mwaka wa kiliturjia." – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 61.

VIWAWA BOKO
www.viwawaboko.blogspot.com

Thursday, December 25, 2014

alhamisi 25/12/2014 mosomo ya sherehe ya kuzaliwa bwana noel

Alhamisi, 25 Desemba 2014
Sherehe ya Kuzaliwa Bwana (Noeli)

Isa 52: 7-10;
Zab 97: 1-6;
Ebr 1:1-6;
Yn 1: 1-18

NENO lilinenwa; Mungu asiyefahamika alilifanya lifahamike, furahini!

Leo Kanisa pamoja na viumbe vyote vyajawa na furaha kwani vimefanywa upya na kuwa kiumbe kipya kwa njia ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. “Neno” basi na uwe mwanga (Mwa. 1:3), lililoleta uumbaji sasa limeongelewa tena, kupitia kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mkombozi wetu. Mwanga (Yn. 1:8), sasa anang’ara katika giza. Mwanga, atoaye mwanga kwa kila mtu amekuja ulimwenguni. Mungu asiyefahamika, sasa amefanywa afahamike, Baba sasa anajidhihirisha mwenyewe, kupitia mwanae wa kiume, Yesu. Neno alifanyika mwili na akakaa kwetu.

Umwilisho au Noeli ni sherehekeo la furaha hii – Mungu wetu anakuwa mwili na anakuja kukaa ndani yetu wanadamu. Tukio hili lilikuwa kubwa sana kiasi cha dunia ya Magharibi kiutamaduni imefanya karne yake katika vipindi viwili vya nyakati kwa mwaka wa kuzaliwa kwake: BC (Kabla ya Kristo) and AD (Anno Domini,kutoka kilatini ni katika Mwaka wa Bwana). Tukio hili liliufanya ulimwengu ufurahi , malaika walifurahi kwa Utukufu kwa Mungu, waliomba kwaajili ya amani duniani kwa watu. Ingawa ukaribisho wa Bwana Yesu haukuwa wa furaha sana ulimwenguni. Mkombozi hakuwa na nafasi ya kuzaliwa, bali katika uhakika, katika moja ya vijiji vidogo Bethlehemu. Hakuwa na tafrija ya ukaribisho, isipokuwa tu kwa baadhi ya wanyama katika hali ya ukimya na baadae wachungaji wachache waliomuabudu Yeye. Mfalme Herode alimchukulia mtoto kuwa kama ni tishio, alitaka mtoto Yesu auwawe. Katika miaka ya mbeleni, mkombozi wetu alikanwa, alivamiwa na kusurubiwa. Na kwa hayo yote aliyoyapokea, mkombozi pekee alirudisha huruma, huruma na upendo. Leo, Yesu amezaliwa kati yetu tena, katika hali yetu ya kumkana na hali ya dhambi; Yeye amezaliwa Bethrehemu ya hali ya ubinafsi, umimi, mateso, vita, unyonyaji, nakadharika. Je, sisi tupo kama wachungaji, waliokwenda kwa Yesu na kuzitoa heshima zao au tupo kama Herode, aliyemchukua Yesu kuwa kama ni tishio la uhuru wetu, katika hangaiko la kutafuta starehe? Je, tunakwenda kufurahi pamoja na wachungaji au kupanga mabaya kama Herode?

Katika milongo miwili iliyopita, dunia yetu imekuwa nzuri sana kwa wanadamu pamoja na uwepo wa kimungu wa Mungu mwenyewe. Ndani yake pia, wengi wametamani kuwa katika giza. Leo Yesu anahitaji azaliwe ndani yetu, awe Neno linenwalo, mwanga unaoondoa giza lote. Je, tupo tayali kujitoa wenyewe kwake Yeye? Je, tupo tayali kuufahamu mwanga huo? Je, tupo tayali kuupokea upendo wake?

Sala: Bwana Yesu, nakuhitaji Wewe uzaliwe ndani yangu leo, Nakuhitaji Wewe unijaze kwa mwanga Wako na kuondoa giza lote ndani yangu, Ninahitaji kunena juu yako katika maneno na maisha yangu. Amina.

"Kwa sababu ya heshima na utume wao, wazazi wakristo wanao wajibu wa pekee wa kuwalea watoto wao katlka sala, wakiwaingiza katlka ugunduzi wa polepole wa siri ya Mungu na mazungumzo ya binafsi naye. "Ni hasa katika familia ya kikristo, ikitajirishwa kwa neema na msaada wa sakramentl ya ndoa, kwamba toka miaka ya awali kabisa watoto budi wafundishwe, kufuatana na imanl ile waliyopewa katika Ubatizo wawe na elimu ya Mungu, kumwabudu na kuwapenda jirani zao"" – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 60.

VIWAWABOKO
www.viwawaboko.blogspot.com

Monday, December 22, 2014

masomo ya jumatatu 22december2014

Jumatatu, 22 Desemba 2014
Juma la 4 la Majilio

1 Sam 1: 24-28;
1 Sam 2: 1, 4-8;
Lk 1: 46-56

Msifu Mungu Muda Wote!

Wimbo wa Bikira Maria lazima ulinganishwa na wimbo wa sifa wa Hana (1 Sam 2:1-10) na Zakaria (Lk 1:68-79). Wakati sifa za kinabii za Maria zinasimama kwa njia mbalimbali, tofauti kubwa zaidi zipo katika hali zao. Hana alimsifu Bwana wakati akimtoa Samweli. Alikuwa katika haibu ya utasa (1Sam 1:7). Kuzaliwa kwa Samweli kulibadilisha hayo yote, na hivyo Hana alikuwa na sababu ya kumsifu Bwana. Vilevile, Zakaria alivumilia miaka mingi sana bila kuwa na mtoto na kuwa kiziwi na bubu kwa muda wa miezi tisa (Lk 1:20, 62). Sasa wakati mwanae wa kiume alipozaliwa, ulimi wake ulifunguka (Lk 1:64), na alikuwa na sababu ya kumsifu Bwana. Kinyume chake, Mwinjili Luka anaweka sifa za Maria mwanzo wa ujauzito wake. Maria alikuwa akimsifu Bwana sio tu baada ya mateso yake bali kabla na wakati wa mateso yake. Yeye hakusifu tu baadae bali alisifu popote pale. Alikuwa akisifu kwa imani na sio kwasababu aliona hali fulani iliyo nzuri. (2 Kor 5:7).

Sala: Tusaidie Maria, kumsifu Bwana daima kama ulivyomsifu wewe. Amina.

"Kwa upande wake, familia ya kikrlsto imepandildzwa katlka fumbo la Kanisa kwa kadiri hiyo hata kuwa mshiriki, kwa namna yake ya pekee katlka utume wa wokovu wa kanisa: Kwa nguvu ya Sakramenti, wakrlsto mume na mke na wazazl "katika hall na jinsi yao ya maisha wanayo karama ya pekee katika Taifa la Mungu". Kwa sababu hii hawapokei tu pendo la Kristo na kuwa jumuiya iliyookolewa, ball wanaitwa pia kuwashirikisha pendo la Kristo ndugu zao, na hivyo kuwa jumuiya yenye kuokoa. Kwa namna hii, pindi familia ya Kikristo ni tunda na ishara ya kuzaa kwa Kanisa kimungu, husimama pia kama mfano, ushuhuda na mshiriki wa umama wa Mungu(116)." – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 49.

VIWAWABOKO
www.viwawaboko.blogspot.com

Sunday, December 14, 2014

Masomo yajumapili 14 desemba 2014, juma la tatu la majilio

Jumapili, 14 Desemba 2014
Juma la 3 la Majilio

Isa 61: 1-2, 10-11;
Lk 1: 46-48, 49-50, 53-54;
1Thes 5: 16-24;
Yn 1: 6-8, 19-28

Je, uelewa wako ni upi juu ya Kristo?

Msemo “mtazamo wa kwanza ni mtazamo bora” umekuwa ni mmoja wa msema wa hatari na wenye uharibifu, katika historia ya saikolojia. “Yohane alikuja kushuhudia nuru …huyu hakuwa ile nuru” (Yn 6 – 8). Wayahudi walifurahishwa kutokana na kile Yohane alichokuwa akitenda. Kabla ya kuwa na mtu yeyote yule awe makini na mwenye kushawishi. Wanashangaa kama yeye ni masiha! … au walau nabii kama Eliya. Ingawa Yohane haitaji kujiweka mbele. Kwa umakini anawarekebisha mtazamo wao wa kwanza. Ilimpasa Yesu kujitoa sadaka mwenyewe juu ya msalaba kuwafanya wao vile alivyo.

Leo Dominika ya tatu ya Majilio inatuitwa ‘Dominika ya Furaha’, itokanayo na maneno ya antifona ya kuingilia. “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema Furahini! Bwana yu karibu” (Flp 4:4) Katika somo letu la Kwanza kuna viashiria vya furaha vilivyoongelewa na nabii kwa ajili ya liturujia hii. Vifungu vyaonyesha kuwa vyafahamika, kwasababu Yesu katika sura ya nne ya Injili ya Luka abadilisha kifungu hiki, anasoma mistari hii na kurudi kwa ndugu zake wa nazareti na anatangaza kuwa somo hili linamuhusu Yeye. Anakuja kutuponya na kutuweka huru!

Sala: Bwana Yesu, ninangojea kwa furaha ya tumaini kuupokea uponyaji na uhuru wako. Amina.

"Hata katika shlda za kazi ya malezi, shida ambazo nl kubwa zaidi aghalabu siku hizi, wazazi sharti wawafunze watoto wao kwa uaminlfu na ujaslrl katika tunu za maisha ya binadamu. Watoto sharti wakue pamoja na msimamo sahihi wa uhuru kuhusu mali ya dunia, kwa kuchagua mtindo wa maisha ulio rahisi na wa kujinyima, na kusadikishwa kabisa kwamba "binadamu ni mwenye thamani zaidi kwa hali aliyo nayo kuliko kwa kile alichonacho"" – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 37.


NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR