Nembo ya Mwaka wa Imani
Imeundwa kwa alama mbalimbali zinazobeba maana maalum.
A) Mashua: Hii ni ishara ya Kanisa linalosafiri.
B) Mlingoti:
Huu ni Msalaba ambao juu yake kuna monogramu (chapa ya herufi zaidi ya
moja zinazochanganyika pamoja, moja juu ya nyingine) IHS. Hizi ni herufi
tatu za kwanza za Kigriki za jina la Yesu: I = Iota, H = eta, S =
Sigma. Alama hizi zinatumika pia kuonyesha kifupisho cha jina la Yesu
ambapo kwa kilatini zinatumika kusimama badala ya maneno: Iesus Hominum
Salvator; yaani, Yesu Mwokozi wa Wanadamu.
C) Mduara:
Nyuma ya monogramu ipo alama ya mduara ambao unaizunguka pia monogramu
hiyo. Hii ni alama ya Jua ambayo inawakilisha Ekaristi Takatifu.
(Tafsiri ya maelezo, TEC, 2012)
Nembo ya Ofisi ya Vijana
Vijana
wane walioshikana mikono wanasimamia vyama vya Kitume vinavyounda umoja
wa Vijana. Katikati kuna alama ya kamba, chini ya neno Fidei. Kamba ni
chombo cha kufunga vitu viwili au zaidi. Kamba inayoshikanisha vijana
wote ni Imani. Neno Fidei ni neno la Kilatini lenye maana, “ya Imani”.
Yaani, umoja huu unahusu imani.
Programu
zote za Mwaka wa Imani zitakuwa na nembo hii. Pia, kauli mbiu ya mwaka
huu, kwetu vijana, itakuwa pia sala, maneno ya mwinjili Luka,
“Bwana, utuongezee imani”
Luka 17:5.
2012—2013