HISTORIA YA UKRISTO
Musa, mwanamapinduzi aliyewakomboa watu wa
Israeli kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 kabla ya kuzaliwa
kwa Yesu, ndiye nabii wa kwanza kutabiri wazi ujio wa Masiya au Kristo
(Kumbukumbu la Torati 18:15-22, hususan mstari 18: "Nitawainulia nabii
kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zenu; na nitatia neno langu kinywani mwake
na atasema nao yote niliyomwamuru."
Kuja kwake
kulitimia katika Agano Jipya, ambalo ni ukamilifu wa yote yaliyotabiriwa katika
Agano la Kale. Kwani Musa
alitumwa kuanzisha Agano la Kale kama maandalizi ya Agano Jipya, akikabidhi
mifumo mingi ya nje na ndani kwa watawala na waamuzi waliomfuatia
watakaoshikilia Agano la kusubiri Masiya wakishirikiana na manabii na makuhani.
Yesu alizaliwa
miaka kama 1800 baada ya Abrahamu. Vitabu vya Injili vinaeleza matukio na mafundisho ya Yesu ambayo ndiyo
mwongozo wa imani hiyo. Maisha na kazi ya Yesu yameibua mambo mengi katika historia. Ndiyo sababu kalenda iliyoenea duniani huhesabu miaka kutoka ujio wake; huu
ni mchango mmojawapo wa Ukristo.
Mafundisho ya msingi ya Yesu
Hotuba ya
Mlimani na Carl
Heinrich Bloch. Hotuba
ya Mlimani inachukulika
na Wakristo kuwa utimilifu wa Torati iliyotolewa na Musa katika Mlima Sinai.
Yesu alifanya ishara za kustaajabisha, au
miujiza. Matokeo ni kwamba, watu wengi wakamwamini. Nikodemu, mshiriki mmojawapo wa baraza la Sanhedrini, ambayo ilikuwa pia
mahakama kuu ya Kiyahudi, alivutiwa na kutaka kujua zaidi kuhusu siri ya
miujiza hiyo na ujumbe kutoka kwa Mungu; kwani yeye alihamasika kuona ishara
zile kutoka kwa Mungu. Yesu akamjibu kwamba hakika mtu hawezi kuingia ufalme wa
Mungu asipozaliwa mara ya pili kwa maji na Roho. Pia akajieleza kuwa mpatanishi
wa ulimwengu wa dhambi na Mungu na kwamba
kila
anayemgeukia kwa imani hatapotea, bali atarithi uzima wa milele: Kristo ni
mfano wa nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa. (Yohana 2:23-3:21; Hesabu
21:9).
Akiwa akitembea
kando ya Ziwa la Galilaya, Yesu alikuta umati wa watu umekusanyika. Basi
akapanda mashua na kuenda mbali kidogo na ufuoni, akaanza kuwafundisha kuhusu
Ufalme wa Mbingu kupitia mfululizo wa mifano. Mmojawapo ni hili lifuatalo: Ufalme
wa Mbingu ni kama punje ya haradali ambayo mtu anaipanda. Ingawa ni mbegu
ndogo sana inakua na kuwa mti wa mboga kubwa kuliko yote. Inakua mti ambao
ndege wanauendea, wakipata makao katika matawi yake. (Mathayo 13:1-52; Marko
4:1-34; Luka 8:4-18; Zaburi 78:2; Isaya 6:9,10).
No comments:
Post a Comment