Saturday, January 19, 2013
Friday, January 18, 2013
Historia ya Ukristo
Historia ya Ukristo
Sanamu ya Yesu
Kristo mkombozi ilijengwa Rio de Janeiro
(Brazil) ni kubwa
kuliko zote zilizopata kutengenezwa.
UKRISTO....
Ukristo ni Dini inayomwamini Mungu pekee kama alivyofunuliwa na Yesu Kristo
ambaye ndiye mwanzilishi wake.
Dini hiyo,
iliyotokana na ile ya Wayahudi, inayolenga kuenea kwa Binadamu wote, na kwa sasa ni kuu kuliko zote duniani,
ikiwa na wafuasi zaidi ya bilioni mbili.
Kitabu chake
kitakatifu kinajulikana kama Bibilia. Ndani yake inategemea hasa Injili na
vitabu vingine vya Agano jipya.
Asili
Chimbuko la
Ukristo ni kuwepo kwa mtu aliyezaliwa takriban miaka 2000 iliyopita huko
mashariki ya kati, katika kijiji cha Bethlehemu kilichopo hadi
hivi leo kwenye mipaka ya Palestina, naye alikuwa
akiitwa Yesu wa Nazareti au mwana wa Yosefu mchonga samani; mama yake akifahamika
kwa jina la Bikira
Maria.
Masiya Yesu
Ukristo ni
matokeo ya utume wa Yesu, uliopokewa na waliomwamini kuwa ndiye Masiya, yaani Mpakwamafuta (Kristo kwa Kigiriki), mkombozi
aliyetimiliza ahadi za Mungu kwa uzao wa Abrahamu.Utabiri wa
kuja kwake ulianzia katika bustani ya Edeni pale Mungu alipomwambia mwanamke ."uzao
wako utamponda kichwa" nyoka, yaani shetani.
HISTORIA YA UKRISTO 2
HISTORIA YA UKRISTO
Musa, mwanamapinduzi aliyewakomboa watu wa
Israeli kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 kabla ya kuzaliwa
kwa Yesu, ndiye nabii wa kwanza kutabiri wazi ujio wa Masiya au Kristo
(Kumbukumbu la Torati 18:15-22, hususan mstari 18: "Nitawainulia nabii
kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zenu; na nitatia neno langu kinywani mwake
na atasema nao yote niliyomwamuru."
Kuja kwake
kulitimia katika Agano Jipya, ambalo ni ukamilifu wa yote yaliyotabiriwa katika
Agano la Kale. Kwani Musa
alitumwa kuanzisha Agano la Kale kama maandalizi ya Agano Jipya, akikabidhi
mifumo mingi ya nje na ndani kwa watawala na waamuzi waliomfuatia
watakaoshikilia Agano la kusubiri Masiya wakishirikiana na manabii na makuhani.
Yesu alizaliwa
miaka kama 1800 baada ya Abrahamu. Vitabu vya Injili vinaeleza matukio na mafundisho ya Yesu ambayo ndiyo
mwongozo wa imani hiyo. Maisha na kazi ya Yesu yameibua mambo mengi katika historia. Ndiyo sababu kalenda iliyoenea duniani huhesabu miaka kutoka ujio wake; huu
ni mchango mmojawapo wa Ukristo.
Mafundisho ya msingi ya Yesu
Hotuba ya
Mlimani na Carl
Heinrich Bloch. Hotuba
ya Mlimani inachukulika
na Wakristo kuwa utimilifu wa Torati iliyotolewa na Musa katika Mlima Sinai.
Yesu alifanya ishara za kustaajabisha, au
miujiza. Matokeo ni kwamba, watu wengi wakamwamini. Nikodemu, mshiriki mmojawapo wa baraza la Sanhedrini, ambayo ilikuwa pia
mahakama kuu ya Kiyahudi, alivutiwa na kutaka kujua zaidi kuhusu siri ya
miujiza hiyo na ujumbe kutoka kwa Mungu; kwani yeye alihamasika kuona ishara
zile kutoka kwa Mungu. Yesu akamjibu kwamba hakika mtu hawezi kuingia ufalme wa
Mungu asipozaliwa mara ya pili kwa maji na Roho. Pia akajieleza kuwa mpatanishi
wa ulimwengu wa dhambi na Mungu na kwamba
kila
anayemgeukia kwa imani hatapotea, bali atarithi uzima wa milele: Kristo ni
mfano wa nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa. (Yohana 2:23-3:21; Hesabu
21:9).
Akiwa akitembea
kando ya Ziwa la Galilaya, Yesu alikuta umati wa watu umekusanyika. Basi
akapanda mashua na kuenda mbali kidogo na ufuoni, akaanza kuwafundisha kuhusu
Ufalme wa Mbingu kupitia mfululizo wa mifano. Mmojawapo ni hili lifuatalo: Ufalme
wa Mbingu ni kama punje ya haradali ambayo mtu anaipanda. Ingawa ni mbegu
ndogo sana inakua na kuwa mti wa mboga kubwa kuliko yote. Inakua mti ambao
ndege wanauendea, wakipata makao katika matawi yake. (Mathayo 13:1-52; Marko
4:1-34; Luka 8:4-18; Zaburi 78:2; Isaya 6:9,10).
HISTORIA YA UKRISTO 3
Maana ya Kristo
Mtume
Paulo anazungumza
hivi kuhusu Kristo:
Walakini iko
hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao
wanaotawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri;
ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
ambayo wenye kutawala dunia hii hawaijui hata moja; maana kama wangalijua,
wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu; Lakini, kama ilivyo andikwa:
Mambo ambayo
jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa
mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Lakini Mungu
ametufunulia sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana
ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo
ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuaye ila Roho wa
Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu,
makusudi tupate kuyajua yaliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno
yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamnu, bali yanayofundishwa na Roho,
tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya
asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake ni upuzi, wala hawezi
kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni
huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu, Maana,
Ni nani
aliyefahamu nia ya Bwana, amwelimishe?
Lakini sisi
tunayo nia ya Kristo. (1 Wakorintho 2:6-16).
Kanisa siku za mwanzo
Jumuia ya
Wakristo inaitwa Kanisa, lililotajwa
na Yesu katika Mathayo 16:18:-
Wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu,
nitalijenga kanisa langu. Wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Ujio wa Roho Mtakatifu
Wednesday, January 16, 2013
Wednesday, January 9, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...