Thursday, January 7, 2016

IKULU LEO AFIKA RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA NA JAJI MSTAAFU WARIOBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam January 7,2016.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.


Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.


Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.

"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Januari, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam January 7,2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzo January 7,2016


HEKALU LA DK. LWAKATARE LASHINDIKANA TENA KUBOMOLEWA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjx7hKNyj6kogEU4YKMrs3_WNqiA7tSU_dYjwI5xi9vxCSYcBTmSddO_eYfY5pxYtWbPcQIrQ25fKg6cAisuWEvYzihJddO4MEcA7tXEDYLzLqobHPaeqV0YbEBp6BrBfE7mkZGO32EiOLm/s1600/3.jpgMAHAKAMA Kuu Kitengo cha Ardhi imezuia nyumba anayoishi Mchungaji wa Kanisa  la  Assemblies of God Mikocheni, Dk. Getrude Lwakatare kubomolewa.
 
Uamuzi huo wa mahakama ulitolewa juzi na Jaji John Mgeta, baada ya Wakili wa Lwakatare, Emmanuel Muga kuwasilisha maombi ya kupinga ubomoaji huo chini ya hati ya dharura.
 
Jaji Mgeta alizuia ubomoaji wa jengo hilo ama kuchukua hatua yoyote kuhusu jengo hilo lililopo Kawe Beach.
 
Muga aliwasilisha maombi akimwakilisha mdai ambaye ni mtoto wa Mchungaji Lwakatare, Robert Brighton dhidi ya wadaiwa NEMC, Manispaa ya Kinondoni na wadau wengine wote.
 
“Mheshimiwa jaji, nawasilisha maombi ya zuio la kubomoa nyumba ya mteja wangu chini ya kifungu namba 95 cha Sheria ya Mwenendo wa Madai na kifungu namba 2(3) cha JALA vinavyotoa mamlaka kwa mahakama kutoa nafuu stahili pale kunapokuwa na ukiukwaji wa kuvunja haki ya wazi,” alidai.
 
Akitoa uamuzi huo alisema tayari pande husika zilikuwa na kesi namba 70 ya mwaka 2012 na ikamalizika kwa kutoa hukumu na kukazia hukumu iliyompa haki ya ushindi mdai.
 
“Mahakama ilimpa haki mdai, lakini chakushangaza mdaiwa anakiuka matakwa ya hukumu na kutaka kubomoa nyumba, kwa hali isiyokuwa ya kawaida mdai anahitaji ulinzi wa mahakama hii ya haki,”alisema Jaji Mgeta.
 
Alisema nyumba hiyo ipo katika kiwanja namba 2019 na 2020 ambapo hati yake ilitolewa mwaka 1979.
 
Inadaiwa mwaka 2011 NEMC ilitoa notisi ya kuvunja nyumba hiyo baada ya kushinikizwa na wakazi wa eneo hilo wakidai ujenzi wake unaziba Mto Ndumbwi na uko jirani na mikoko.
 
Wakili Muga aliwasilisha maombi ya kuzuia nyumba  ya mteja wake kubomolewa  baada ya Wizara  ya  Maliasili  na  Utalii kupitia  wakala  wa  misitu  Tanzania (TFS ), kuweka alama  ya X wakidai imo katika hifadhi  ya  bahari.

ANZA KURUDISHA MKOPO WAKO WA ELIMU YA JUU (CAG ATETA

Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeanza kukagua taasisi za umma kuhusu utekelezaji wa sheria inayozitaka kuwatambua waajiriwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu.
 
Hadi Mei mwaka jana, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilikuwa imekusanya Sh65.2 bilioni kati ya Sh123.8 bilioni zilizopaswa kuwa zimerejeshwa.
 
Bodi hiyo iliwakopesha wanafunzi Sh1.8 trilioni tangu mwaka wa masomo 1994/95 hadi Juni 2014 kati ya fedha hizo, Sh51 bilioni zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, George Nyatega alisema ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mikopo iliyoiva, CAG ameanza kutekeleza matakwa ya kisheria ya ukaguzi kwenye taasisi za umma ili kuwabaini wanafunzi waliopaswa kuanza kurejesha mikopo yao.
 
“Ni imani ya HESLB kuwa waajiri katika utumishi wa umma watatoa ushirikiano kwa ofisi ya CAG ili kuondokana na matatizo ya kisheria,” alisema.
 
Nyatenga alisema sheria iliyoanzisha HESLB inazitaka taasisi zote za umma kuijulisha kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya ndani ya siku 28 na bodi kuthibitisha kama waajiriwa hao ni wanufaika wa mikopo au la.
 
Mkurugenzi huyo alisema baada ya bodi kupokea taarifa na kuthibitisha kuwa waajiriwa ni wanufaika wa mikopo, mwajiri atapaswa kuijulisha HELSB na kuanza kukata sehemu ya mshahara wa mwajiriwa ndani ya siku 30. 

SUMATRA WAKARIBISHA MAONI YA WANANCHI JUU YA NAULI ZA MABASI YAENDAYO KASI



MAMLAKA ya Udhibiti,Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), inatarajia kukusanya maoni ya wananchi juu ya viwango vya nauli za mabasi yatakayotoa huduma ya usafiri wa haraka Jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa SUMATRA kwa vyombo vya habari kwenda kwa wananchi  ambapo ofisi hiyo itawaalika wadau wote wa usafiri hususani wananchi kuchangia maoni kwenye mkutano utakao fanyika januari 5 kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 na nusu asubuhi.

Mamlaka  pia inapokea maoni ya wananchi kupitia anuani ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo ambayo ni S.L.P 3093 au kwa barua pepe ambayo info@sumatra.go.tz ambapo kabla ya kufikia uamuzi wadau wanatakiwa kutoa maoni ya kuridhia viwango vya nauli  kwa mujibu wa sheria ya Sumatra.

Maoni ya maandisi yatapokelewa kwenye ofisi ya Mkuregenzi Mkuu iliyopo Jengo la Mawasiliano House Makutano ya barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Nkumo kuanzia Saa 4 asubuhi hadi saa 9 alasiri mwisho wa kupokelewa maoni hayo ni Januari 13 mwaka huu.

Mamlaka hiyo imepokea maombi ya nauli kutoka kampuni ya UDA-RT inayolenga kutoa huduma ya mpito ya usafirishaji jijini Dar es Salaam katika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa Dart.

Maombi yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ni Safari kwenye njia za pembeni (feeder route) shilingi 700 ,safari kwenye njia kuu (trunk route) shilingi 1200 na njia zote mbili ni 1400 ambapo wanafunzi watalipa nusu nauli anayotoa mtu mzima.

HARMONIZE AMEAMUA KUCHORA TATOO YA BOSS WAKE

Msanii wa label ya WCB anayekuja juu kwa sasa, Harmonize ameamua
kuuthibitishia ulimwengu kuwa anajivunia kuwa mtoto wa kimuziki wa staa
wa Tanzania, Diamond Platnumz kwa kuchora tattoo yenye picha yake na
kuandika a.k.a ya Boss wake iliyozua utata hivi karibuni ‘Simba’.
h n d
Hiki ndicho alichokiandika Harmonize kwenye picha aliyoipost Instagram
kuelezea sababu za kuchora tattoo hiyo:
Harmonize tattoo
Harmonize tattoo

/“Katika Maisha Yangu Sikuwahi Kuwaza Kuwa Itatokea Siku Nikajichora
Tatoo But Diamond Nimtu Mwenye Mchango Mkubwa Sanaaaa Katika Maisha
Yangu Leo Hii Mimi Ninathaminika Kutoka Kwenye Kunyanyasika
Ninaheshimika Kutoka Kwenye Kudhalaulika Nimekuwa Maarufu Na Kupata
Uthamani Mkubwa Kupitia Yeye Siotu Kwa Kipaji Nilicho Nacho Kwani
Wangapi Wanavipaji…??? Naisaidia Familia Yangu Kwa Kile Nikipatacho
Sihaba Akiwa Na Mchango Wake Mkubwa Sana…… Lakini Mwisho Wasiku Haya Ni
Maisha Nahii Ni Dunia Inamambo Mengi Sanaa Hasa Sisi Vijana Ambao
Niwepesi Wa Kujisahau Kinaweza Tokea Kitu Kidogo Sanaa Ukasahau Wema Na
Fadhira Ulizotendewa, Lakini Pia Mungu Ndio Katukutanisha Na Karibia
Watu Wengi Wanajua Tumekutanaje Kwamana Nimekuwa Nikiulizwa Katika
Vyombo Vya Habari Tofauti Tofauti So Watu Wengi Wanajua Tulivyo Kutana
But Hakuna Anaejua Tutaachana Vipi kwamana Sisi Ni Binadamu Kuna Kifo
Leo Na kesho Huwezi Jua Yawanadamu Ni Mengi Siamini Kuwa Binadamu Wote
Duniani Wanafurahia Mahusiano Na Ukaribu Wetu Na Huwezi Shindana Na
Binadamu Ukijua Yambele Wenzio Wanajua Yanyuma Ndio Mana Yakujichora
Hiii Picha Yake Amabayo Haitofutika Hadi Naingia Kaburini Hata ikitokea
Hatupo Pamoja Nikiitazama Hii Picha Itabaki Kama Kumbu Kumbu Na Heshima
Yangu Kwake Hadi Siku Yangu Ya Mwisho Haya Ni Maamuzi Yangu Binafsi…..”/

Uganda yaongoza orodha ya nchi zinazoridhika zaidi kimapenzi

081512-health-std-Gonorrhea-kissing-couple-diseasesUganda imeongoza orodha ya nchi duniani ambazo wananchi wake wanaridhika zaidi kimapenzi.

Utafiti huo ulifanywa na kampuni inayotengeneza condom, Durex na kuhusisha watu 26,000 kuanzia miaka 16 katika nchi 26.
Katika utafiti huo walibaini kuwa ni watu 44 pekee ndio wanaoridhika na maisha yao ya mapenzi. Uganda, Switzerland na Hispania ndio zimeongoza orodha ya watu wanaoridhika zaidi kimapenzi. Utafiti huo ulibaini kuwa waganda 5 kati ya 10 hushiriki tendo hilo walau kwa saa moja kila wiki. Hii ilionekana kuwa ni juu zaidi kwa watu kushiriki tendo hilo duniani.
Tanzania haipo kwenye orodha hiyo.
Hii ni orodha nzima:

1. Uganda
2. Switzerland
3. Hispania
4. Italia
5. Brazil
6. Ugiriki
7. Uholanzi
8. Mexico
9. India
10. Australia
11. Ujerumani
12. China

Isome Orodha ya Albamu 10 zilizouza zaidi Marekani (USA) mwaka 2015

Adele-2015-press-Alasdair-McLellan-XL-billboard-650-2Kampuni ya Nielsen Music imetoa orodha ya album 10 zilizouza zaidi mwaka 2015 nchini Marekani.

Imeanza kuangalia mauzo ya album hizo kuanzia Dec. 29, 2014 hadi Dec. 31, 2015. Hii ni orodha nzima:
1 Adele, 25 – 8,008,000
2 Taylor Swift, 1989 – 3,105,000
3 Justin Bieber, Purpose – 2,225,000
4 Ed Sheeran, X- 2,206,000
5 The Weeknd, Beauty Behind the Madness – 2,045,000
6 Drake, If You’re Reading This It’s Too Late – 1,919,000
7 Meghan Trainor, Title – 1,795,000
8 Sam Smith, In the Lonely Hour- 1,741,000
9 Sam Hunt, Montevallo – 1,378,000
10 Fetty Wap, Fetty Wap- 1,295,000

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR