Friday, August 16, 2013

Ungana nasi Kuanzia kesho hadi Jumapili Parokiani Boko

kesho kuanzia saa mbili asubuhi Viwawa wa Parokia ya Boko wataanza sherehe za jubile ya miaka kumi ya Parokia yetu, Sherehe hizi zitaanza kwa semina ambazo zitatolewa na Fratel na Padre Ngowi mada zitakuwa ni Jitambue Kijana mkatoliki na Makuzi ya Vijana pia kutakuwa na mechi kali ya fainal ya Ligi ya Paroko cup ambayo itatanguliwa na upigiji wa Penalt ambao utafanywa na Baba Paroko, Paroko Msaidi na Padre Mlezi wa Viwawa, Pia wenyeviti wote wa jumuiya za Parokia yetu watapiga Penalt.

usiku vijana watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa show mbali mbali na tutapata muda wa kupreview ziara ya mbulu na kuangalia yale matukio muhimu ya kukumbukwa kwenye tamasha la mwaka jana \.

yote ni kwa upendo na Mungu amutuchagua sisi tuwe mfano basi tuwatumikie mwengine na kuwaonyesha njia.................karibuni sana

Thursday, August 8, 2013

USIKOSE KUWA SEHEMU ZA SHAMRA HIZI

LEO TAREHE 8/8/13 SIKUKUU YA NANE NANE, FIKA KATIKA UWANJA WA MBWENI MALINDI JESHINI KUSHUHUDIA MECHI KALI YA NUSU FAINAL LIGI YA PAROKO CUP KATI YA TIMU YA ST. GASPER YA BOKO VS ST. RAPHAEL YA MBWENI MALINDI, MECHI HII ITAANZA SAA KUMI KAMILI JIONI.

SIKU YA JUMAPILI TUTAKUWA NA MECHI NYINGINE KALI YA NUSU FAINAL KATI YA DAMU TAKATIFU VS MARIA DEL MATHIS ZOTE ZA BOKO MECHI ITACHEZWA KATIKA UWANJA WA MBWENI MALINDI KUANZIA SAA KUMI JIONI FIKA BILA KUKOSA NA UWE SEHEMU YA BURUDANI HII

Saturday, August 3, 2013

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Waislam wakati wa Maadhimisho ya Siku kuu ya Id El Fitri




Kwa Waislam wote duniani.
Ninayo furaha kubwa kuchukua fursa hii kuwasalimia wakati huu mnapoadhimisha Siku kuu ya Id El Fitri, inayofunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, uliotengwa kwa ajili ya kufunga, swala na sadaka.
Ni mapokeo ya siku nyingi kwamba, katika Siku kuu hii, Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini linawatumia ujumbe wa matashi mema, ukiambatana na mada kwa ajili ya tafakari ya pamoja. Mwaka huu, ambao ni mwaka wangu wa kwanza kama Papa, nimeamua kutia sahihi mimi mwenyewe na kuwatumieni, ndugu zangu wapendwa, kama alama ya heshima na urafiki kwa Waislam wote, lakini kwa namna ya pekee viongozi wa kidini.
Kama wengi wenu mnavyofahamu, Makardinali waliponichagua mimi kama Askofu wa Roma na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, nilichagua jina la “Francisko” Mtakatifu maarufu aliyempenda Mungu na watu wote, kiasi hata cha kuwaita ndugu zake. Alipenda, akasaidia na kuwahudumia wahitaji, wagonjwa na maskini; ni mtu aliyetunza sana mazingira.
Ninafahamu kwamba, familia na mwelekeo wa kijamii unapata nafasi ya pekee kwa Waislam katika kipindi hiki, ni vyema kutambua kwamba, kuna uwiano wa mambo haya hata katika imani ya Kikristo na utekelezaji wake.
Mwaka huu, mada ambayo ninapenda kutafakari pamoja nanyi bila kuwasahau wote watakaobahatika kuusoma ujumbe huu ni ile inayowahusu Waislam na Wakristo: Kuhamasisha hali ya kuheshimiana kwa njia ya elimu.
Mada ya mwaka huu inapania kufafanua umuhimu wa elimu kadiri tunavyofahamiana, ili kujenga msingi wa kuheshimiana. “Kuheshimiana” maana yake ni mwelekeo wa upendo kwa watu tunaowathamini na kuwajali. Huu ni mchakato wa “pande mbili za shilingi” unaozihusisha pande zote.
Tunachoalikwa kuheshimu kwa kila mtu kwanza kabisa ni maisha yake, mwili wake mzima, utu na haki ambatanishi zinazotokana na utu huo, heshima, mali yake, kabila, utambulisho wake wa kitamaduni, mawazo na msimamo wake wa kisiasa. Tunaalikwa kufikiri, kuzungumza na kuandika kwakuwaheshimu wengine, si tu wakati wanapokuwepo, bali ni kwa daima na kwa wakati wote, kwa kuachana na shutuma au kuwachafulia wengine sifa yao njema. Familia, shule na mafundisho ya dini pamoja na njia za mawasiliano ya kijamii zina dhamana ya kuhakikisha kwamba, lengo hili linafikiwa.
Nikiangalia dhana ya kuheshimiana katika uhusiano wa majadiliano ya kidini, hasa zaidi kati ya Waislam na Wakristo, tunaalikwa kuheshimu dini ya wengine, mafundisho yao, vielelezo vya imani na tunu msingi za maisha ya kiroho. Viongozi wa kidini waheshimiwe pamoja na nyumba za ibada. Inatia uchungu kuona viongozi au nyumba za ibada zinashambuliwa.
Ni wazi kwamba, tunapoheshimu dini ya jirani zetu au pale tunapowatakia wengine matashi mema katika Maadhimisho ya Siku kuu zao za kidini, tunapania kushiriki furaha yao, bila hata ya kufanya rejea kwenye maudhui ya imani yao.
Kuhusiana na elimu kwa vijana wa Kiislam na Kikristo, ni wajibu wetu kuwalea vijana ili waweze kufikiri na kuzungumza kwa heshima kuhusu dini na wafuasi wa dini nyingine, pamoja na kujizuia kuzibeza au kukashifu imani na ibada zao.
Tunafahamu kwamba, kuheshimiana ni msingi wa kila mahusiano, lakini zaidi miongoni mwa waamini wanaoungama imani zao. Kwa njia hii, ukweli na urafiki wa kudumu unaweza kukua.
Nilipokutana na Wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao mjini Vatican hapo tarehe 22 Machi 2013, nilisema, “Haiwezekani kuanzisha uhusiano mwema na Mwenyezi Mungu, wakati unawabeza watu wengine. Kwa hiyo ni jambo la muhimu kuzidisha majadiliano miongoni mwa dini mbali mbali, lakini zaidi na Waamini wa dini ya Kiislam. Katika Ibada ya Misa Takatifu, mwanzo wa utume wangu, nilifurahi kuona viongozi wa Serikali na wa Kidini kutoka katika Ulimwengu wa Waislam.”
Kwa maneno haya, ninapenda kusisitizia kwa mara nyingine tena umuhimu wa majadiliano na ushirikiano miongoni mwa waamini, lakini zaidi kati ya Wakristo na Waislam; jambo linalopaswa kuendelezwa.
Ni matumaini yangu kwamba Wakristo na Waislam watajitahidi kuwa ni vyombo vya kukuza hali ya kuheshimiana na urafiki, hasa kwa njia ya elimu.
Hatimaye, ninapenda kuwatumia sala na matashi mema, ili maisha yenu yaweze kumtukuza Mwenyezi Mungu pamoja na kuwakirimia furaha wale wanaowazunguka. Ninawatakieni Siku kuu Njema ninyi nyote!
Francisko.
Imetolewa Vatican,

Monday, July 29, 2013

Brazil, Kwa herini! Tutaonana tena Mungu akipenda!




Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya 28 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013 kwa Ibada ya Misa Takatifu kwenye ufuko wa Copacabana, Rio de Janeiro, Brazil, tukio ambalo limehudhuriwa na watu millioni tatu, amewashukuru na kuwaaga wananchi wa Brazil na kwa namna ya pekee, Rais Dilma Vana Rousseff kwa niaba ya wananchi wa Brazil kwa matendo makubwa waliyomfanyia Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, anarejea mjini Vatican akiwa amesheheni matukio ya furaha ambayo kwa sasa yanageuka kuwa ni sala. Anasikia ile hamu ya kuendelea kukaa na wananchi wa Brazil, waliomwonesha moyo wa ukarimu na urafiki. Anawashukuru kwa tabasamu la nguvu na la kweli walilommegea wakati wote alipokuwa anakutana nao bila kusahau sadaka na majitoleo ya vijana wengi walioacha shughuli zao ili kuweza kuwakirimia upendo na huduma, ndugu zao katika Kristo.

Anawakumbuka vijana aliokutana nao kwenye Hospitali ya Mtakatifu Francisko inayowahudumia waathirika wa dawa za kulevya, bila kusahau upendo wa wananchi wa kitongoji cha Varginha. Baba Mtakatifu anasema, kwa hakika anaona mkono wa Yesu ukitenda kazi miongoni mwa vijana na kwa umati mkubwa wa watu aliokutana nao katika kipindi cha juma zima, muda ambao kamwe hataweza kusahau katika maisha na utume wake!

Baba Mtakatifu anaendelea kuwashukuru kwa namna ya pekee vijana waliokuwa ni kiini cha Maadhimisho ya Siku ya 28 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013. Wengi wao walikuja kama wafuasi wa Kristo, sasa wanarudi makwao wakiwa wamefundwa na kuiva kama Wamissionari. Ni vijana ambao wako tayari kutolea ushuhuda wa maisha yao kwa njia ya furaha, huduma, daima wakijitahidi kujenga utamaduni wa upendo. Ni vyema vijana wakasimama kidete kulinda na kutetea utu na heshima ya binadamu sanjari na kujitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya Injili ya Kristo.

Baba Mtakatifu anawakumbusha vijana kwamba, Yesu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanza mchakato wa kuwatafuta, anapenda kuwasha moto wa Injili ili waweze kwenda kutangaza Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia. Baba Mtakatifu anasema, yeye binafasi amekwisha onja baadhi ya matunda ya kazi hii, wengine wataendelea kufurahia katika utimilifu wake.

Baba Mtakatifu Francisko amemshukuru Bikira Maria wa Aparecida. Anasema, kwenye madhabahu ya Bikira Maria wa Aparecida, amepiga magoti kwa ibada kwa ajili ya kuombea dunia, lakini kwa namna ya pekee wananchi wa Brazil. Anasema, amemwomba Bikira Maria ili aweze kuimarisha imani ya Kikristo nchini Brazil kama ilivyo hata kwa nchi nyingine duniani; imani ambayo ni amana kubwa kwa utamaduni wa wananchi wa Brazil.

Ni mwaliko anasema Baba Mtakatifu wa kuendelea kujenga na kudumisha amani na mshikamano kati ya watu. Mwishoni kabisa, Baba Mtakatifu anaendelea kuwaomba wananchi wa Brazil na wote wenye mapenzi mema kumsindikiza katika maisha na utume wake kwa njia ya Sala, kwani anauhitaji mkubwa wa sala!

Tamasha la vijana 2013

Kila mwaka vijana wa Parokia ya Boko huwa wanakutana kwa siku tatu katika Tamasha la Vijana Parokia, Kilele cha Tamasha hili huwa ni siku ya kumbukumbu ya Mwenye Heri Isidore Bakanja ambaye ni Somo wa Parokia yetu. 

Kwa mwaka huu sherehe hizi zitaambatana na maadhimisho ya miaka kumi tangu tuwe parokia, kutokana na ukubwa wa sherehe hiyo.. Halmashauri ya Walei Parokia wakaombe sherehe hizi pamoja na tamasha zisogwe mbele mpaka tarehe 18/08/2013, ili maandalizi yaweze kufanyika kwa ufasaha zaidi.

kwa upande wa Vijana mashindano ya Mpira wa miguu yanaendelea na fainal inatarajiwa kufanyika tarehe 17/08/2013 katika uwanja wa Boko... pia tutakuwa na fainal ya mpira wa Pete kwa wasichana, michezo ya ndani kama kuvuta kamba, kukimbia na Yai, maigizo, mashairi, vichekesho, sarakasi , kuimba n.k.

Kwa upande wa semina ni furaha kubwa sana kwetu, kwani tunao mababa wa kiroho ambao wapo Parokiani kwetu na wanasubiri tu hiyo siku tutakuwa naye Baba Paroko Pd: Dismass, Pd:Mlezi wetu Dominick na Sauti ya Radi Paroko Msaidizi PD: Nicolus Ngowi.

Fika uwe sehemu ya Mabadiliko chanja....yenye tija ya kukomaza mapendo Mioyoni mwetu, kuleta maendeleo ya Kiroho na Kijamii ndani ya Familia zetu na Jamii nzima kwa ujumla.

Kwa mchango wa Tshs 7000 kwa ajili ya Chakula Vinjwaji na Malazi Mepesi..........

Sunday, July 28, 2013

MSIMAMO WA PAROKO CUP BAADA YA MECHI ZA MWISHO ZA MZUNGUKO WA PILI




MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013


PAROKO CUP 13 :KUNDI A
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magoliwaliofungwapoint
Mt. Gasper42116 7 7
Damu Takatifu41129 6 5
Mbweni412146 4


MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013


PAROKO CUP 13 :KUNDI B
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magoliwaliofungwapoint
MARIA DEL MATHIAS4202105 8
MT. RAPHAEL421154 7
ANTHONY WA PADUA4031410 1

Tuesday, July 9, 2013

KILA MWENYE PUMZI AMSIFU BWANA

  Nani wa msifu Bwana na vipi? Imeandikwa, Zaburi 150:1-6 . Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika anga la uweza wake msifuni katika matendo yake makuu msifuni kwa kadiri ya ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu msifuni kwa kinanda na kinubi; msifuni kwa matari na kucheza msifuni kwa sese na filimbi. Msifuni kwa matoazi yaliyayo msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. 

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR