Monday, October 21, 2013

Mwaka Mmoja Baada ya kifo cha Padre Massawe: aliyependa Vijana na Mwanahabari



NILIPOKEA taarifa za masikitiko na zenye mshtuko mkubwa kwa njia ya simu  kupitia kwa Paroko wa wanga PD. Dismas Mfungomali wa simu ya mkononi usiku wa manane kuamkia Oktoba 26, 2012 kuwa  aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Kimisionari la Kanisa Katoliki  la Consolata, Padri Salutarius Lelo Massawe (50) amezama baharini wakati akiogelea Bagamoyo na mwili wake haujaonekana.
Ilikuwa kama ni  ndoto, wakati Jumapili iliyopita tulikuwa naye tukijiandaa na mkesha wa kimisionari kwa vijana wote wa jimbi la Dar es salaam,   ambapo nililazimika kumpigia Mwenyekiti wa Mabalozi wa Vijana wa Consolata (CMC) Ndugu Machota , na kumuuliza, na yeye amepata habari jana.
  Padri Massawe alifariki mjini Bagamoyo wakati akiogelea katika  Bahari ya Hindi na wakuu wenzake wa Shirika la Consolata kutoka nchi  mbalimbali waliokuwa na mkutano  katika Kituo cha Kiroho cha Consolata kilichoko Bunju jijini Dar es Salaam. Baada ya mkutano aliwaeleza wenzake kuwa angependa wakapumzike Bagamoyo kwa kutembelea maeneo ya kimisionari sehemu ambapo Injili iliingia miaka ya 1800.
Walipofika Bagamoyo, walimaliza kutembelea makaburi, kanisa, na sehemu nyingine muhimu za kihistoria na kuamua kuanza kuogelea. Kwa mujibu wa padri aliyekuwa naye ni kwamba majira ya saa 10 jioni,  waliamua kuondoka kwenye maji lakini Padri Massawe alitokomea kimya kimya ndani ya maji na hakuonekana hadi  kesho yake asubuhi alipokutwa pembezoni mwa  bahari kwenye mikoko.
Kutokana na kutokuwa mbinafsi,  alionesha dhahiri moyo wa uzalendo kwa taifa lake.  Kila mara alikuwa akiniambia ninatamani sana Watanzania wawe matajiri wote, nisione masikini wakitaabika hasa kulala njaa. Ni vigumu  kutamka au kuandika sifa  zake  zote, Padri Massawe licha  ya kuwa alikuwa Mkuu wa Shirika la Kimisionari la Consolata hapa Tanzania wadhifa aliokabidhiwa mwaka jana, pia alikuwa mwanahabari makini, aliyefanya kazi  kwa kuzingatia misingi na weledi, huku akiamini kuwa habari njema siku zote humjenga binadamu kiafya na kiroho.
Alijitahidi kutumia jarida la  kimisonari  Enendeni linalotolewa mara nne  kwa mwaka  na shirika lake, yeye kama mhariri mkuu kuinjilisha, alitumia vyombo vya habari vya Tumaini Media, radio, TV na gazeti la Tumaini Letu kufundisha na kuwatia Wakristo moyo.
Padri Salus Lelo (kama tulivyozoea kumwita) ameishi Iringa ambako ndiko yaliko Makao Makuu ya wamisionari wa Consolata kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja, hadi anafariki dunia lakini wananchi wa Iringa walionekana wenye majonzi mazito kuliko ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa naye siku zote sehemu nyingine. Hii inaonesha upendo wa dhati ambao aliwaonesha kwa muda mfupi.
Tunajiuliza ni nani kati yetu anayeweza kurithi tunu na  vipaji alivyokuwa navyo Padri Salus Massawe? Je, mioyo yetu inatamani kupata neema kama ya kwake? Tulipofika Iringa eneo la Kanisa Kuu la Jimbo (cathedral)  parokia ya Bikira Maria Consolata alfajiri  31, Oktoba 2012,  ilikuwa ni simanzi, vilio vilivyorindima na kuwafanya umati wa ndugu tuliosindikiza msiba kutoka Dar es Salaam na Moshi kuanza kulia tena.
Waumini walikuwa wamekesha kanisani hapo kwa siku mbili, walipouona mwili wa kipenzi chao waliangua kilio kikubwa. Vilio hivi, vilifuatiwa na mazishi yaliyofanyika katika Parokia ya Tosamaganga,  umati mkubwa ulishiriki, wananchi wa Iringa walitamka wenyewe kuwa tumempoteza kiongozi wa kabila letu, ‘Mtwa’ kwa Kihehe wakimaanisha chifu.
waamini , waliamua kumuwekea historia ya pekee kwa kumzika  kwa heshima za kichifu wa kabila la Wahehe kwa kupigiwa  mizinga  20 angani. Tulijiuliza hivi na mapadri wanapigiwa mizinga kama wanajeshi? Lakini hayo hata yeye hakujua kama yatatokea akifariki. Kifo cha Padri Massawe  kinaweza kujengwa taswira nyingi miongoni mwa jamii.  Ni kwanini yeye? Na ni kwanini pale Bagamoyo? Lakini  yote tumuachie Mwenyezi Mungu.
Waliosoma naye SAUT  wanasikitika hasa wanapokumbuka, uhamasishaji usio na kikomo wa Padri Massawe kwenye michezo, shughuli za kijamii, burudani, vikao, kuanzishwa kwa asasi ya kutetea uhai wa binadamu (Pro-Life) ambayo alikuwa mwasisi na mwenyekiti wa kwanza. Mashindano ya mpira wa miguu maarufu SAUT kama FAWASCO, alihakikisha darasa lake la ‘Mass Comm (2005-08)’ linachukua kombe na likafanya hivyo.
Jumapili jioni alikutana na kikundi cha  wazaliwa wa Kibosho ‘Konkya’ waliokuwa wakiishi Mwanza na mikutano ilikuwa ikifanyika pale Kilimanjaro Hotel Mabatini, tukiwa naye. Wakati wa Misa Baba Askofu  wa Jimbo la Iringa, Taracius Ngalalekumtwa,  alieleza jinsi ambavyo Padri Massawe amefanikiwa kujenga mahusiano mazuri na jamii nje na ndani kila mara akionesha uso wa matumaini na mapendo.
Pamoja na upadri wake,  kupangiwa kazi za ofisini,  hata wakati wa masomo alikuwa padri anayejitahidi kukutana na makundi ya watu wote, wenye mali, wasio na mali, wenye elimu na wasio na elimu, alikuwa padri anayetambua utu wa kila mtu, kuhakikisha kila mwanadamu anayekutana naye anakuwa na amani na furaha moyoni.  Mara kadhaa nilimpelekea watu walio kata tamaa na  wenye changamoto mbalimbali za kimaisha, lakini walirudi na hali mpya, wamebadilika.
Huyo hakuwa padri anayegawa fedha, mali ila alikuwa akigawa upendo wa dhati, furaha, amani na matumaini. Ndiyo maana askofu anasema: ‘ Padri Massawe alikuwa zaidi ya padre kwani alitumikia nafasi yake kama mkuu wa shirika, mwalimu, padri, daktari na kiongozi wa kijamii  huku akijitahidi kujenga mahusiano na kila anayepishana naye.
‘Usihesabu umri wako kwa miaka uliyonayo, hesabu umri wako kwa kuangalia watu ambao umehusiana nao vizuri. Padri Massawe alijitahidi kuhusiana  vizuri na kila aliyepishana naye bila kujali dini, imani au kabila lake,’ anasema  Baba Askofu.
Katika mkutano uliofanyika Bunju, ambao marehemu alikuwa mwenyeji,  ulihudhuriwa pia na padri Mtanzania ambaye ni Makamu Mkuu wa Shirika la wamisionari Wakonsolata duniani,  kutoka Roma,  Padri Detrick Mpandawazima,  ambaye walikuwa wote baharini na alishuhudia akifariki, alimtaja marehemu Padri Massawe kama kiongozi mwenye kipaji kikubwa ambaye bado alihitajika kulitumikia shirika hilo na taifa la Tanzania.
Tutamkumbuka kwa kujitahidi kuomba neema ya Mungu ili tuishi maisha mazuri ya kumtumikia Mungu. Kuishi maisha ya kujitoa kwa ajili ya wengine na kusambaza upendo wa Mungu. 
sasa ni mwaka mmoja toka ututoke tunazidi kukumbuka kwa mengi ulifanya kwetu, Tunamuombea Mwenyezi Mungu aipokee Roho yake na ampumzishe kwa amani. Amina!

Thursday, October 17, 2013

Katekesi ya Papa- Tunasadiki katika Kanisa moja la Kitume kwa sababu.....



Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mahujaji na wageni, inaendelea kuitafakari sala ya Kanisa, ya Nasadiki, Jumatano hii akitazama kifungu Nasadiki katika Kanisa moja Takatifu na la Kitume. Na alianza kwa kuwahoji mahuajii na wageni wanaofika Roma kwa ajili ya hija , iwapo wamewahi kujiuliza ina maana gani kusema , Kanisa la Mitume na umuhimu wa Mitume Petro an Paulo, ambao waliyatoa maisha yao hapa Roma , kwa ajili ya kuifikisha Injili na kuishuhudia Injili . Lakini pia akasema, kuna zaidi katika hilo....

Papa alieleza na kusisitiza kwamba Kanisa la kitume, kwa sababu, lina uhusiano kina, katika urithi wake na Mitume kwa kwanza, lile kundi dogo la wanaume kumi na wawili walioitwa na Yesu kwa majina na kuishi nae na hatimae kuwatuma nje kuhubiri mafundisho yake ( Mk 3:13-19 ).

Papa alieleza na kufafanua maana ya neno “Apostolo” Mtume , kwamba ni neno la Kigiriki lenye maana ya "aliyetumwa ", ni mtu anayepeleka ujumbe wa kufanya jambo fulani. Ni neno lenye nguvu , na Mitume waliitwa na kuchaguliwa na Yesu kuendeleza kazi yake , ya kusali na kupeleka habari njema ya upendo wa kuokoa kwa watu wote. Hivyo sala na kutangaza Injili , inakuwa ni kazi ya kwanza muhimu ya mtume.. Papa ametaja hili ni muhimu kwa sababu, mara nyingi , wengi tunafikiri, kuwa mtume ni kwenda kuihbiri injili peke yake. Sivyo, ni kufanya kazi nyingi ...
Papa alifafanua, na kurejea siku za mwanzo wa Kanisa, akisema, pia kulikuwa na matatizo na vikwazo kwa mitume kulingana na wakati wao. Na hivyo walitayarisha watu wengine kama mashemasi, katika kukabilaina na kupungukiwa na wakati wa kuomba na kutangaza Neno la Mungu. Na kama tunavyo fikiri juu waandamizi wa Mitume - Maaskofu, na pia Papa,ambao nao pia wana tatizohili la kupungukiwa na muda wa kusali na kuitangaza Injili kama warithi wa mitume. kwa muono huo, Papa Francisko amesisitiza, kila muumini wa kanisa ni mtume, kwa sababu yumo ndani ya Kanisa la kitume. Na hivyo waamini wote wanatakiwa kuwa mitume katika kazi yake ya kuihubiri Injili ya wokovu wa ulimwengu.
Papa alieleza na kutaja mambo matatu katiak mafundisho yake kwamba, Kanisa ni la kitume kwa sababu, limejengwa juu ya maombi na mahubiri ya Mitume, kwa mamlaka yalitolewa kwa mitume na Kristo mwenyewe,kama alivyoandika Mtakatifu Paulo kwa Wakristo wa Efeso (2, 19-20) .
Pili Kanisa ni la kitume kwa sababu hudumisha ukamilifu wa mafundisho ya Kristu na njia za wokovu, kwa msaada wa Roho Mtakatifu , kama inavyo eleza Kateksimu ya Kanisa. Kanisa karne hadi karne limetunza hazina hii ya thamani, ambayo ni maandiko matakatifu , mafundisho , sakramenti, huduma ya wachungaji, ili twaamini waweze kuwa waaminifu kwa Kristo na kuyashiriki maisha yake.
Na tatu Kanisa ni la kitume kwa sababu, ujumbe wake uliodmanishwa kwa mitume ni ujumbe wa injili kwa dunia nzima, unaoendelea katika njia ya historia ya ujumbe huo, ambao Yesu aliukabidhi Mitume. Yesu mwenyewe alisema, nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi . Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote , mpaka mwisho wa ulimwengu "( Mt 28:19-20). Na hivyo Kanisa mizizi yake imo katika mafundisho ya Mitume, mashahidi wa kweli wa Kristo. Hivyo , leo tunapaswa kufurahia na kulipenda kanisa kama ni mahali pa kukutana na Bwana Mfufuka , aliyewatuma mitume wake , kuwaalika wote waliokutana nao kuufahamu ukweli wa Injili , furaha ya imani na ahadi ya maisha ya Milele, iliyotangazwa na Mitume. 

JUMAPILI DOMINIKA YA 29 ya Mwaka C. Tarehe 20/10/2013

JUMAPILI DOMINIKA YA 29 ya Mwaka C.
      RATIBA ZA IBADA 
KIGANGO CHA MH. ISIDORI BAKANJA- BOKO.
MISA YA KWANZA 12:15-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI     SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. FRANCIS WA ASIZ-MBWENI 
MISA YA KWANZA SAA 1:10-3:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 3:00-4:30 ASUBUHI

KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
SAA 1:00-3:00 ASUBUHI.
MISA YA PILI SAA 3:00-5:00

KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA-MBWENI TETA
MISA NI SAA 3:00-5:00.


MASOMO 

 Somo 1:Kut.17:8-13
Wakati huo Waameleki walitokea, wakapigana na Israel huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na waameleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikiwa Musa alipoinua mkono wake, Israel walishinda; na aliposhusha mkono wake, Amaleki walishinda. lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; bali wakatwa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akamwaangamizaAmaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.

SOMO 2: 2Tim.3:14 - 4:2
Wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa Imani iliyo katika Kristo Yesu. kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayehukumu waliohai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

INJILI. :Lk.18:1-8
Yesu aliwaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala msikate tamaa. Akasema, palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea endea , akisema, nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikata tamaa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima. Bwana akasema, sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
             
  1.  Maandalizi ya Dekania Cup yanaendelea kwa upande wa tImu ya Mpira wa  Pete jumamosi tarehe 19 wanacheza kutauta mshindi wa tatu dhidi ya bunju.


  1. tunawakumbusha vijana wote kuendelea kulipa ada kwa maendeleo ya chama chetu..... mapendo sana malipo kwa njia ya benk kwa jina na number hii :viwawa parokia ya boko account no 01524526820100 crdb bank tegeta branch
JIANDAE NA ZIARA YA UINJILISHAJI MWAKA 2014.....................

Thursday, October 10, 2013

Ziara ya Uinjilishaji JImbo la Mbulusehemu ya Promo www viwawaboko blogs...

MASOMO NA MATANGAZO YA J2 YA DOMINIKA YA 23 MWAKA C TAREHE 13/10/13

JUMAPILI DOMINIKA YA 28 ya Mwaka C.
      RATIBA ZA IBADA 
KIGANGO CHA MH. ISIDORI BAKANJA- BOKO.
MISA YA KWANZA 12:15-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI     SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. FRANCIS WA ASIZ-MBWENI 
MISA YA KWANZA SAA 1:10-3:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 3:00-4:30 ASUBUHI

KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
SAA 1:00-3:00 ASUBUHI.
MISA YA PILI SAA 3:00-5:00

KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA-MBWENI TETA
MISA NI SAA 3:00-5:00.


MASOMO 

 Somo 1:2Fal.5:14-17
Naamani alishuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. akaja akasimama mbele yake; akasema sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duaniani mwote, ila katika Israel, basi nakuomba upokee mbaraka kwa utumwa wako. lakina akasema, kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutia apokee; lakini akakataa. naamani akasema, kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana.

SOMO 2: 2Tim.2:8-13
Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo Injili yangu. Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi. Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika kristo Yesu, Pamoja na utukufu wa Milele.
 Ni neo la kuaminiwa. kwa maana, kama tukifika pamoja naye, 
Tutaishi pamoja naye pia: kama tukistahimili tutamiliki pamoja naye;
Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi, 
Yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

INJILI. :Lk.17:11-19
Yesu alipokwenda njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya. Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajioshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika a mmoja wao alipoona kwamba wamepona, alirudi, huku akimtukuzaMungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa msamaria. Yesu akamjibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wako wapi? je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu Utukufu ila mgeni huyu? akamwambia, Inuka, nenda zako, Imani yako Imekuokoa.
             
  1.  Maandalizi ya Dekania Cup yanaendelea kwa upande wa tImu ya Mpira wa  Pete.


  1. tunawakumbusha vijana wote kuendelea kulipa ada kwa maendeleo ya chama chetu..... mapendo sana malipo kwa njia ya benk kwa jina na number hii :viwawa parokia ya boko account no 01524526820100 crdb bank tegeta branch
JIANDAE NA ZIARA YA UINJILISHAJI MWAKA 2014.....................

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR