Wednesday, January 7, 2015

Nendeni Jangwani kwa ajili ya Mwaka 2015

Katika Maandiko Matakatifu tunasoma yafuatayo: "Mara akaongozwa na Roho kwenda jangwani, akakaa huko siku arobaini akijaribiwa na shetani" (Marko 1:12-13).Yesu anaenda Jangwani na kukaa huko kwa muda wa siku arobaini. Lengo la kwenda jangwani si kujaribiwa ila kujiandaa kwa kazi iliyokuwapo mbele yake, kazi ya kumkomboa mwanadamu. Yesu alikwenda kutafakari kazi yake yote na yale yatakayompata katika kazi hiyo. Yesu alikwenda kutengeneza dira ya utekelezaji wa kazi ya ukombozi.

Read More
Nasi tunapoanza Mwaka Mpya 2015 tunahitaji kuingia katika 'jangwani' la kiroho na kimaisha ili kujitengenezea dira ya utekelezaji kwa mwaka mzima. Tujiwekee malengo binafsi, malengo ya familia, Jumuiya, kanda, kigango, parokia, jimbo na mahali pa kazi. Ni kipindi cha kujiwekea malengo ya kiroho, kiuchumi na kijamii. Mathalani. Mfano :
KIROHO: Jipangie mwaka huu unataka kufika wapi? Panga mambo yako ya kukua kiroho;tafakari ya Neno la Mungu; sala binafsi, sala za familia, ushiriki wako katika Jumuiya, kanda, kigango, parokia na kijimbo. Panga kushiriki mafungo ya kiroho, semina za kiroho, hija na matendo ya huruma. Ushiriki wako katika vipindi vya Kwaresma, Pasaka, Majilio na Krismas n.k.
KIUCHUMI: Tengeneza dira ya kiuchumi mwanzoni mwa mwaka kwa kupanga unataka kufika wapi kiuchumi mwaka huu. Usiache suala la uchumi likuendeshe bali wewe ulitawale kwa kufuata utakachojipangia mwanzoni mwa mwaka. Utajikuta unafanya mambo mengi kwa mpangilio hadi unafurahia maisha. Panga bajeti ya mwaka mzima; mapato na matumizi yako yaandike ili yakuongoze.
Bajeti yako iwe shirikishi ili itekelezeke, isiwe siri yako. Shiriki au ongoza kupanga bajeti ya mwaka ya familia, jumuiya, parokia, jimbo na mahali pa kazi. Iheshimu bajeti hiyo. Bajeti yako ianze na matumizi ili ikuongoze kupanga mapato. Kama mapato ni madogo kulingana na matumizi; fanya ubunifu, fikiria fursa mpya na zifanyie kazi, pia punguza matumizi yasiyo ya lazima, kadi za michango isiyo ya lazima, vikao visivyo na tija vitakavyokugharimu n.k. Wakati mwingine ni heri ya lawama kuliko fedheha!
Panga zaka yako, sadaka, majitoleo, michango ya Jumuiya, mavuno ya parokia, mavuno ya jimbo n.k usikurupuke kila siku na kwenda kutoa 'makombo' hayana nafasi mbele ya Mungu ni sawa na kujiletea 'laana' maishani mwako.
Mambo mengine muhimu ya kupanga katika dira ya mwaka huu ni pamoja na kushiriki matukio muhimu ya kijamii. Ni mwaka wa kura za maoni ya kupata katiba ya nchi yetu, usithubutu kupanga kutokushiriki, huo ni wajibu wa kila raia wa Tanzania.
Kushiriki uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais. Ili tupate viongozi wazuri, wachamungu, waadilifu na wakweli, jitokeze ili uchaguliwe na/au uchague kiongozi atakayetufaa kuiongoza jamii na nchi yetu.
Mwaka wa Familia utafungwa rasmi mwaka huu, Je, umeambulia nini kiimani? Umejiwekea mikakati gani ya kutengeneza mapungufu yaliyo ndani ya familia yako? Shiriki vyema semina za mwaka wa familia. Huu pia ni Mwaka wa Watawa Duniani, Je, unashiriki namna gani katika kuhamasisha, kukuza na kulea miito mitakatifu ndani ya Kanisa?
Huu ni mwaka wa uchaguzi wa viongozi wa Kanisa - walei kuanzia ngazi ya Jumuiya ndogondogo hadi Taifa. Jitokeze uchaguliwe na uchague viongozi hao. Shiriki kikamilifu kwani kanisa linakuhitaji.
Yote hayo yanatuhitaji kwenda 'jangwani' ili kujipanga. Tumshirikishe Mungu kupitia sala na mafungo. Tumkabidhi Mungu malengo yetu ya mwaka 2015. Tujitathmini mara kwa mara juu ya utekelezaji wa malengo hayo. Tuache kuishi kwa mazoea, mwaka 2015 tuwe wahalisia, tusibahatishe! Tuepuke mikwaruzano, tuongeze furaha na ufanisi. Tuwe 'Kristu' katika maisha yetu ya kila siku ili kuisaidia jamii. Tuache kulalamika lalamika, tuchukue hatua.

Tuesday, January 6, 2015

UMOJA WA VIJANA DEKANIA YA MT. GASPER DEL BUFFALO - kufanya uchanguzi wa Viongozi tarehe 10/01/2015

Dekania ya Mt. Gasper ni Dekania ilipo katika Jimbo kuu la Dar es salaam, inaundwa na Parokia kumi na moja ambazo ni  Parokia ya Bunju, Boko Tegeta, Madale, Bahari Beach, Mtongani, St. Gasper, Maria Del Mathias, Sala sala, Mt. Dominiko, Bikira Maria Mama wa huruma, Mbezi Beach  Pamoja na Parokia teule za Thomas More Mbezi Beach, Yohane Mtume, Nyaishozi Tegeta na Parokia ya Ununio tegeta.

Baada ya Baba mlezi wa vijana wa Dekania kuona mwenendo mbaya wa viongozi na kuamua kuwashirikisha Mapadre wote wa parokia za Dekani hii, kwa pamoja wameridhia kuvunja uongozi wa VIWAWA dekania, na kuitisha uchaguzi mpya ili wapatikane viongozi wapya watakao leta maendeleo kwenye dekania yetu.

Uchaguzi huo utafanyika tarehe 10/01/2015 Parokiani Bunju kuanzia saa 3:00 asubuhi, wajumbe wa uchaguzi huo ni Kamati tendaji ya VIWAWA, Parokia zote za dekania yetu.

Pia tarehe 17/01/2015 kutakuwa na Semina ya vijana wote wa Dekania itakayofanyikia Pale Parokiani St. Gasper na atakuwepo Msanii wa Nyimbo za Bongo Fleva Roma Mkatoliki.

IBADA YA MISA TAKATIFU YA UTOAJI DARAJA LA USHEMASI NA UPADRE LEO KANISA LA ST. JOSEPH, JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM

Mafratel waliopata Ushemasi,
  1. Shemasi DanielMatugwa Vicent -  Parokia ya Changombe
  2. Shemasi Meinrad Bigirwamungu - Parokia ya Mtongani
  3. Shemasi Raymond AlbanoMbaula  -  Parokia ya Kigamboni
Na Shemasi aliyepata daraja la Upadre  ni Padre Tito Deogratius Rwegoshora - Parokia ya Kibaha

Baba Askofu Kardinal Pengo atangaza Kigango cha Orongoni kuwa Parokia na kitahudumiwa na Mapadre wa Shirika la Wamisionari wa Mt. Francis wa Asizi.
Pia ametangaza Parokia Teuli ambazo zitakuwa chini ya uangalizi mpaka zitakapokuwa Parokia ambazo ni;
  1. Kigango cha Ununio kilichokuwa chini ya parokia ya Tegeta na kitakuwa kinahudumiwa na Mapadre wa Shirika la Mt. Vicent wa Mbinga.
  2. Kigango cha Mt. Yohane Mtume Nyaishozi kilichokuwa chini ya Parokia ya Tegeta na kitakuwa kinahudumiwa na Mapadre wamisionari wa Maria Emaculate 
  3. Kigango cha Thomas More kilichokuwa chini ya Parokia ya Mt. Gasper kitakuwa kinahudumiwa na Mapadre wa Jimbo na Paroko atakuwa PD. Gilbert Makuru aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mikocheni


Sunday, January 4, 2015

Masomo ya Tarehe 4/01/2015 mwaka B, wa Kanisa Dominika ya kwanza ya Mwaka Mpya 2015

04
 Januari
 Jumapili: ya tokeo la Mama Epifania.
SOMO  1. Isa. 60:1-6

 Ondoka, ee Yerusalemu, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa Bwana umekuzukia. maana tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu latazifunika......
somo 2. Efe. 3:2-5, 5-6 

Ndugu zangu; Ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo......


  INJILI.Mt. 2:1-12
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.

Yesu alipozaliwa Bethelehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifiki Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. Basi mfalme Herode  aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao; Kristo azaliwa wapi? Nao wakamwambia katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Nawe Bethlehemu, katika Nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda, kwa kuwa kwako atatoka mtawala atakaye wachunga watu wangu Israel. Kisha Herode akawaita wale Mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota, Akawapeleka Bethlehemu, akasema, shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende kumsujudia, Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.  Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine
Ratiba ya Ibada ya Jumapili ya tarehe 02/11/2014
Kigango cha Boko
Misa ya Kwanza- saa 12:15 Mpaka saa 1:45 Asubuhi.
Misa ya Pili        -  saa 2:00 Mpaka saa 3:50 Asubuhi.
Misa ya Tatu     -   saa 4:00 Mpaka saa 5:30 Asubuhi.

Kigango cha  Mt. Rafael Mbweni Malindi

Misa ya Kwanza   - saa 1:00 Mpaka saa 2:50 Asubuhi
Misa ya Pili            - saa 3:00 Mpaka saa 4:50 Asubuhi.

Kigango cha Mt. Fransisco wa Asizi - Mbweni
Misa ya Kwanza - saa 1:15 mpaka saa 2:50 Asubuhi.
Misa ya pili          - saa 3:00 mpaka saa 4:50 asubuhi

Kigango cha Mt. Anthony wa Padua - Mbweni Mpiji
Misa ni saa 3:00 mpaka saa 5:00 asubuhi

Wednesday, December 31, 2014

Masomo ya jumatano tarehe 31/12/2014

Jumatano, 31 Desema 2014
Jumatano katika Octava ya Kuzaliwa Bwana

1Yoh 2:18-21;
Zab 95: 1-2, 11-13;
Yn 1: 1-18

Jibu katika Neno la Mungu

Dibaji ya Injili ya Yohane ni nyimbo nzuri inayoimba juu ya simulizi ya Krismasi, fumbo la Umwilisho. Kutoka katika ufahamu huu wa binafsi wa kuishi na Kristo, Yohane alikuwa ameshawishika kwa kina sana kuwa Yesu ndiye Neno, Aliyekuwako tokea mwanzo pamoja na Mungu, Aliyekuwa mwili na kukaa kwetu. Andiko hili tukufu linatoa muunganiko wa imani ya Kikristo. Ukristo sio dini ya kitabu bali ni dini au neno la Mungu, sio neno lililoandikwa na lisilo nena, bali ni ya umwilisho na Neno liishilo. Kwahiyo, hususani katika Adhimisho la Ekaristi, wakati habari njema inapohubiriwa, ni Kristo Mwenyewe ndiye anayehubiri kupitia watumishi wake, wakitafuta jibu sawa la imani ipendwayo ambayo Yeye aliomba kwa wale wote ambao Aliwahubiria katika Palestina. Na kanisa ni katika kiini chake cha ndani, jumuiya ya wale wote wanaosikia neno la Mungu na kulizingatia. Swali ni, je, kama wanajumuiya wa hii jumuiya ya imani inayosikiliza, je, ni namna gani tunajibu?  Je, daima tupo tayali kujifungua wenyewe katika neno la Mungu namapenzi yake kwetu sisi? Au tunajikuta sisi wenyewe hatupendi, tusio badilika kutokana na nguvu ya neno la kubadilisha, isiyoenda kutokana na tofauti ya neema iletwayo?

Sala: Bwana, tuongoze katika upendo mkuu wa neno lako na tutie nguvu ya unyenyekevu katika kujibu na kutii imani. Amina.

"Amri ya maisha ya kikristo itaonekana si katika kitabu kilichoandikwa, ball ni katika tendo la binafsi la Roho Mtakatifu mwenye kumsukuma na kumwongoza Mkristo. Ni "sheria ya Roho ya uhai wa Kristo Yesu". "Maana Mungu amekwisha miminia mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia". Jambo hili ni kweli pia kwa raume na mke wakristo na famllia ya klkrlsto. Mwongozo na sheria ya maisha yao ni Roho wa Yesu aliyemiminwa ndani ya mioyo yao katika adhimisho la sakramenti ya Ndoa. Katika mfululizo pamoja na Ubatizo katika maji na Roho, ndoa huweka upya sheria ya kiinjili ya upendo, na pamoja na zawadi ya Roho, hukaza zaidi katika mioyo ya waume na wake Wakristo. Upendo wao ukisafishwa na kuokolewa, ni tunda la Roho mwenye kufanya kazi katika mioyo ya waumini na kufanyiza, wakati huo huo, amri ya msingi ya maisha katika uhuru wa kimadaraka." – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 63.

VIWAWA BOKO
www.viwawaboko.blogspot.com

Tuesday, December 30, 2014

masomo ya tarehe 30/12/2014

Jumanne, 30 Desemba 2014
Jumanne katika Octava ya Kuzaliwa Bwana

1 Yoh 2:12-17;
Zab 95: 7-10;
Lk 2: 36-40

Kuitwa kuwa Watakatifu

Katika Injili Yesu anatamka kuwa yeye pekee anamfahamu Baba. Ni Neno la Mungu ndilo linaufanya ujio wake mioyoni mwetu, ndilo linalomfanya Yeye afahamike mioyoni mwetu. Jibu letu sio tu kushinda ovu, bali katika hali chanya kutembea katika njia ya utakatifu. “watakatifu sio watu wakubwa sana, wala hawakuzaliwa wakamilifu. Wapo kama sisi, kama kila mmoja wetu … je, nini kiliyabadilisha maisha yao? Walipo utambua upendo wa Mungu, waliufuata kwa moyo wao wote bila ya kubakiza wala bila ya unafiki” – Papa Fransis. Utakatifu sio upendeleo wa watu wachache, wa wale wote wanaovaa kanzu au kiremba, bali pia wale wote wenje majinsi na viatu vya tennis; ni wa wale wote wanaokwenda katika filamu, wanaosikiliza muziki, wanaotumia muda wao na marafiki zao. Lakini wote wanahitaji kumpatia Mungu nafasi ya kwanza, awe mbele ya kazi zao, familia zao, na marafiki zao. Tunawahitaji watakatifu wanaotafuta muda kwa ajili ya kusali kila siku na wanaojua namna ya kuwa katika upendo na usafi, useja, na mambo yote mema. Tunawahitaji watakatifu walio na moyo wa kujitolea katika kuwasaidia masikini na kuyafanya mabadiliko yanayohitajika katika jamii.

Sala: Bwana, tupe busara ya kuishi katika ulimwengu lakini si kujikita sisi wenyewe katika hali yake. Amina.

"Kusudi kubwa la sala ya kanisa la nyumbani ni kuhudumia kama utangulizi wa kiasili kwa ajili ya watoto kuwa sala ya kiliturjia ya Kanisa zima, katika maana ya kuifanyia maandalizi na kuieneza katika maisha ya binafsi, familia na kijamii. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kushiriki kwa wanajumuiya wote wa familia ya Kikristo katika adhimisho la Ekaristi, hasa siku za Jumapili na sikukuu, na masakramenti mengine, hasa sakramenti za kuingizwa watoto katika Ukristo. Miongozo ya Mtaguso Mkuu ilifungua wajibu Mpya kwa familia ya kikristo ilipoorodhesha familia kati ya vikundi vile ambavyo ilipendekeza kusali sala ya Kanisa kwa pamoja. Kwa namna hiyo hiyo, familia ya Kikristu itakazana kuadhimisha nyumbani, na kwa namna inayofaa kwa wanajumuiya wake, nyakati na sikukuu za mwaka wa kiliturjia." – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 61.

VIWAWA BOKO
www.viwawaboko.blogspot.com

Thursday, December 25, 2014

alhamisi 25/12/2014 mosomo ya sherehe ya kuzaliwa bwana noel

Alhamisi, 25 Desemba 2014
Sherehe ya Kuzaliwa Bwana (Noeli)

Isa 52: 7-10;
Zab 97: 1-6;
Ebr 1:1-6;
Yn 1: 1-18

NENO lilinenwa; Mungu asiyefahamika alilifanya lifahamike, furahini!

Leo Kanisa pamoja na viumbe vyote vyajawa na furaha kwani vimefanywa upya na kuwa kiumbe kipya kwa njia ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. “Neno” basi na uwe mwanga (Mwa. 1:3), lililoleta uumbaji sasa limeongelewa tena, kupitia kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mkombozi wetu. Mwanga (Yn. 1:8), sasa anang’ara katika giza. Mwanga, atoaye mwanga kwa kila mtu amekuja ulimwenguni. Mungu asiyefahamika, sasa amefanywa afahamike, Baba sasa anajidhihirisha mwenyewe, kupitia mwanae wa kiume, Yesu. Neno alifanyika mwili na akakaa kwetu.

Umwilisho au Noeli ni sherehekeo la furaha hii – Mungu wetu anakuwa mwili na anakuja kukaa ndani yetu wanadamu. Tukio hili lilikuwa kubwa sana kiasi cha dunia ya Magharibi kiutamaduni imefanya karne yake katika vipindi viwili vya nyakati kwa mwaka wa kuzaliwa kwake: BC (Kabla ya Kristo) and AD (Anno Domini,kutoka kilatini ni katika Mwaka wa Bwana). Tukio hili liliufanya ulimwengu ufurahi , malaika walifurahi kwa Utukufu kwa Mungu, waliomba kwaajili ya amani duniani kwa watu. Ingawa ukaribisho wa Bwana Yesu haukuwa wa furaha sana ulimwenguni. Mkombozi hakuwa na nafasi ya kuzaliwa, bali katika uhakika, katika moja ya vijiji vidogo Bethlehemu. Hakuwa na tafrija ya ukaribisho, isipokuwa tu kwa baadhi ya wanyama katika hali ya ukimya na baadae wachungaji wachache waliomuabudu Yeye. Mfalme Herode alimchukulia mtoto kuwa kama ni tishio, alitaka mtoto Yesu auwawe. Katika miaka ya mbeleni, mkombozi wetu alikanwa, alivamiwa na kusurubiwa. Na kwa hayo yote aliyoyapokea, mkombozi pekee alirudisha huruma, huruma na upendo. Leo, Yesu amezaliwa kati yetu tena, katika hali yetu ya kumkana na hali ya dhambi; Yeye amezaliwa Bethrehemu ya hali ya ubinafsi, umimi, mateso, vita, unyonyaji, nakadharika. Je, sisi tupo kama wachungaji, waliokwenda kwa Yesu na kuzitoa heshima zao au tupo kama Herode, aliyemchukua Yesu kuwa kama ni tishio la uhuru wetu, katika hangaiko la kutafuta starehe? Je, tunakwenda kufurahi pamoja na wachungaji au kupanga mabaya kama Herode?

Katika milongo miwili iliyopita, dunia yetu imekuwa nzuri sana kwa wanadamu pamoja na uwepo wa kimungu wa Mungu mwenyewe. Ndani yake pia, wengi wametamani kuwa katika giza. Leo Yesu anahitaji azaliwe ndani yetu, awe Neno linenwalo, mwanga unaoondoa giza lote. Je, tupo tayali kujitoa wenyewe kwake Yeye? Je, tupo tayali kuufahamu mwanga huo? Je, tupo tayali kuupokea upendo wake?

Sala: Bwana Yesu, nakuhitaji Wewe uzaliwe ndani yangu leo, Nakuhitaji Wewe unijaze kwa mwanga Wako na kuondoa giza lote ndani yangu, Ninahitaji kunena juu yako katika maneno na maisha yangu. Amina.

"Kwa sababu ya heshima na utume wao, wazazi wakristo wanao wajibu wa pekee wa kuwalea watoto wao katlka sala, wakiwaingiza katlka ugunduzi wa polepole wa siri ya Mungu na mazungumzo ya binafsi naye. "Ni hasa katika familia ya kikristo, ikitajirishwa kwa neema na msaada wa sakramentl ya ndoa, kwamba toka miaka ya awali kabisa watoto budi wafundishwe, kufuatana na imanl ile waliyopewa katika Ubatizo wawe na elimu ya Mungu, kumwabudu na kuwapenda jirani zao"" – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 60.

VIWAWABOKO
www.viwawaboko.blogspot.com

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR