Tuesday, November 3, 2015

TB JOSHUA NDANI YA TANZANIA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHUK6qHRSPRKRwp43WqBP7yGcDVqgM0iG4P5bHxS27kpf5TiTi3hHC-1QdMvrowXJUv0205P4CCZfVeW_sv6xQYoO_HQJBf_7UBneA-Nud9Q5S-QuHjY9ZWkCCPejM7oEFrrgyNckJtYCt/s1600/unnamed.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizvUtB6kdTMRLsIQdrF4PGjl6vPvQ-2ikKFlNXDXXg9xT7OpDt3L7VKM0vKjy5vnpEZsrvRYfo1dQrKonwD2VigQd0Y4Ec3tA55MhFBSeS_7ySfSi20QjkVnz_Sh42AC6sMSsM8IUOhWdK/s1600/unnamed+%25282%2529.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEij661eCHLHzKuAd5eMIOXcs64ZCphhS_K03eLGffvxYSCrafPMX-eUNw7CQfXlsroDY554v-rTmhYUQqVmLx0wyVtPAwBEtlb3Der4qcQtBDVjk3PkaHxhuXCBDNzcNMIbONa-WEoeXEMU/s1600/blogger-image-1611632315.jpg

TB JOSHUA ATUA DAR LEO KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUMUAPISHA RAISI WA TANZANIA AWAMU YA TANO DR. JOHN POMBE MAGUFULI

LIJUE KABILA LA WACHAGA.

WAJUE WACHAGA
Kabila la Wachaga linafahamika kwa wengi kuwa linapatikana mkoani Kilimanjaro. Kwa asili, Wachaga ni mchanganyiko wa Wamasai, Wasambaa, Wataita, Wakamba na Wakahe.
Wachaga walianza kuhamia kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro kwenye karne ya 17.
Walipofika wakiwa katika vikundi vidogovidogo waliwakuta wakazi, wenyeji kwenye Misitu ya
Mlima Kilimanjaro walioitwa Wakonyingo. Wenyeji hawa ambao huitwa Mbilikimo hawakupenda kuchanganyika na wahamiaji wageni, hivyo wakahama na kuanzisha makao yao ya kudumu kwenye misitu minene iliyopo nchini Kongo. 

Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro.Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga 2,000,000. Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame).
Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika, Wa-Mamba ,Wa-Marangu,Wa-Kilema,na Wakirua.Makabila mengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha.
Watu wengi wanafikiria kwamba Wachaga wanatokana na asili moja. Ukweli ni kwamba wamegawanyika katika himaya 15, wanatofautiana kwa lafudhi, lugha, rangi na mwonekano wa miili yao. Wachaga wapo katika makundi makuu matatu ya Hai, Vunjo na Rombo.
Wale wanaopatikana eneo la Hai ni Wasiha, Wamasama, Wamachame,Wangíuni, Wakibosho, Wauru na Wamoshi. Kwa wale wanaopatikana eneo la Vunjo ni Wakirua, Wakilema, Wamarangu, Wamamba na Wamwika. Kutoka eneo la Rombo ni Wamkuu, Wamashati na Wasseri.Hadi sasa haijulikani vizuri asili ya jina Wachaga, ila wanahistoria wanaeleza kwamba jina hilo linatokana na neno la Kiswahili
linaloitwa 'Kichaka'.Inaelezwa kwamba misafara ya wafanyabiashara iliyokuwa ikiongozwa na Waswahili pamoja na Waarabu, walipokuwa wakipita maeneo ya Vunjo waliwaona wenyeji wa huko wakiwa wamejenga vibanda vya kulinda mazao yao yasiliwe na wanyama waharibifu. Wakawaita wenyeji hawa kwamba wanaishi vichakani na kuanzia hapo wageni wafanyabiashara na Wamisionari walipokuwa wanakuja Kilimanjaro walielekezwa na waongozaji misafara yao kwamba wanakwenda
kwenye nchi ya “Uchakani”, wakimaanisha kwamba kwa watu wanaoishi vichakani. Hatimaye wageni wakashindwa kulitamka vizuri neno hili na kuliita ìUchagani, Jina hili likawekwa kwenye ramani na kuitwa nchi ya “Wachaga”. Hivyo ndivyo wenyeji waliokuwa wakiishi kwenye Miteremko ya Mlima Kilimanjaro walivyopewa jina lao. Wachaga.


Maendeleo ya Wachaga Maendeleo yao hapo awali yalitokana na zao la kahawa. Walifanikiwa kuanzisha vyama vya ushirika na hatimaye mwaka 1932 walianzisha Halmashauri ya Wachaga (Chaga Council) ambayo kwa sasa inatumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Halmashauri hii iliongozwa na Mangi Mkuu Mshumbue Thomas Marealle II. Mwaka 1946, utawala wa Waingereza
uliboresha Baraza la Halmashauri ya Wachaga. Himaya ndogo za Wachaga zipatazo 17 (himaya mbili za Wakahe na Waarusha chini zilijumuishwa kwenye Tarafa ya Vunjo) na kuundwa kwa Tarafa tatu za Hai, Vunjo na Rombo. Halmashauri ya Wachaga ilijenga miundombinu na huduma za jamii ikiwamo kuwasomesha watoto wao kwenye shule na vyuo mbalimbali kama Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Halmashauri ya Uchaga ilikuwa na bendera yake ambayo ipo hadi leo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, yenye nembo tano kuu:
1. Mlima Kilimanjaro uliochorwa katikati ya bendera ukionyesha mandhari nzuri ya kilele cha Kibo. Kilele cha Kibo kinatoa maji safi na ni kielelezo cha umoja wao.
2. Chini ya kilele cha Kibo, upande wa kushoto wa bendera kuna mgomba wenye ndizi. Hiki ni chakula kikuu cha Wachaga.
3. Upande wa kulia wa bendera ni tawi la mbuni ukiwa na matunda yake. Kahawa ni zao lililowaletea maendeleo.
4. Bendera imezungukwa na matawi ya 'sale' lenye matawi mawili (draceana plant). Matawi haya yamefanya mduara kuzunguka kilele cha Kibo, mgomba wa ndizi na tawi la zao la kahawa. Masale ni mmea unaoheshimiwa sana na Wachaga wote. Ni alama ya amani. Masale hutumika katika sherehe na shughuli zote za kimila zinazofanywa na Wachaga. Majani yake ni kijani kibichi yanayoonyesha jinsi Kilimanjaro ilivyo na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya kila aina.
5. Juu kidogo ya kilele cha Kibo yupo chui ambaye amejipumzisha. Chui ni alama kuu ya mamlaka ya Wachaga. Hapo awali kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro walikuwepo chui wengi wa rangi
nyeusi lakini kutokana na ongezeko la watu pamoja na uharibifu wa mazingira chui hawa wametoweka. Sikukuu ya Wachaga Sikukuu ya Wachaga wote ilikuwa ikiadhimishwa Novemba 10 kila mwaka kama kumbukumbu ya siku ambayo Wachaga wote walipokusanyika na kumchagua Mangi Mkuu baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Uchaga. Maadhimisho ya kwanza ya mwaka 1952 yalitanguliwa na uchaguzi wa Halmashauri ya Wachaga wote kuanzia kwenye ngazi ya Uchili (kijiji), Umangi ( uchifu wa eneo) na mwisho ngazi ya baraza kuu.

WAJUE WACHAGGA
Lugha ya Kichagga
Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro.
Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kivunjo, Ki-Old Moshi, Kiuru,Kikibosho, Kimachame, na Kisiha.
Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Ki-Old Moshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho.
Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.

Historia ya elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Ukristo walijenga makanisa na shule.
Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1, 2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote.
Ni vema pia kusema kUwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu.
Kilimo na chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe, viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Pia mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu.
Ndizi za Wachagga
Ingawa Wachagga wa leo wanakula vyakula mbalimbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi.
Kuna ndizi za aina mbalimbali na kwa matumizi tofauti. Mfano ndizi sukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda.
Ndizi mshale hukatwa zikiwa mbichi na kupikiwa vyakula mbalimbali pamoja na nyama ya ng'ombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko, kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.
Aina nyingine ni ndizi ng'ombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam utaona ndizi mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku vumbi au kiti moto.
Wachagga na muhogo
Inasemekana kuwa "Mchagga halisi hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa Wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yake; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani, hasa wa Machame, walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu, ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba hukohuko Kilimanjaro, majirani na watani wa Wachagga, yaani Wapare, walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.
Ulaji kiti-moto
Pamoja na kilimo cha mazao, Wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na Wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukuwa pendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo Wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo Waislamu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".
Majina ya Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: kwa mfano, familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi, Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame.
Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kamnde, Kileo, Kimambo, Tesha, Msaki, Assey, Kyara, Kessy, Ndanu, Macha, Mbishi, Kombe, Njau wanatoka Old Moshi na Vunjo.
Kavishe, Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Silayo, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo.
Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu na Kilema.
Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba Foya, Munishi, Kilawe na kadhalika hutoka Kibosho.
Ukoo wa akina Teri wako Mamba, Chami, Chuwa, Kiria na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha.
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu.
Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.
Utawala wa jadi ya Wachagga
Watawala wa Kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ng'ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya Ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho - anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng'ombe na mazao yao na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo.
Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa Ma-mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa kama mabepari wa kwanza wa kijadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao Ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao.
Usemi maarufu wa "u-Mangi-meza" nadharia inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa Kichagga.
Ardhi
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa Wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi.
Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi huko Uchaga ulipelekea Wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta Wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya n.k. wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula.
Ukienda kwenye mikoa hiyo utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta kwenye makusanyiko ya Wachagga katika mikoa mbalimbali.
Maoni juu ya Wachagga
Ingawa wanaume wa Kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ng'ombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongoni mwao.
Wanawake wa Kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula.
Ingawa kipato cha Wachagga ni kikubwa kulingana na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo ni wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto.
Wengi wa watoto hao ni wale ambao wazazi wao ni watu wa pombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba Uchagga una vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa biashara kubwa. Karibu kila kaya kumi na tano kuna kilabu cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya madebe sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo.
Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchagga kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi, mchana na jioni.
Sababu nyingine ni kazi; mama wa Kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani, hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za biashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi.
Pia baadhi ya kina mama wa Kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri, tofauti na chakula walichoandaliwa watoto, japo ni chakula kilekile.
Pia Wachagga wamekua na desturi ya kuwaenzi wazee wao waliotangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanaporudi nyumbani ifikapo mwezi Desemba. Hili limekuwa suala la kawaida sana na halipingiki. Wengi wao huwa wanarudi na magari, ndiyo sababu utaona ya kwambwa kila ifikapo mwezi Desemba kila mwaka foleni za magari zimekuwa zikiongezeka kutokana na Wachagga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. Wengi wao wamekuwa wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi.

Sunday, November 1, 2015

WABUNGE WAPYA: MAJIMBO WALIPOTEZA UKAWA NA WALIOPOTEZA CCM

Majimbo ya Ukawa yaliopotea
1. Nyamagana
2. Ilemela
3. Bukombe
4. Kasulu Mjini
5. Musoma Mjini
6. Kigoma Kaskazini
7. lindi mjini
8. Kilwa kusini

Majimbo CCM walioyapoteza
1.Monduli
2.Simanjiro
3.Same Mashariki(Mama Kilango)
4.Siha
5.Bunda(kwa Wasira)
6.Arumeru Magharibi
7.Jimbo la Christopher Chiza(huko mkoa wa Kigoma)
8.Tanga Mjini
9.Babati Mjini
10.Babati vijijini
11.Tandahimba
13.Moshi vijijini
14.Tunduma
15.Mtwara mjini
16. Bukoba mjini
17. Ikungi mashariki
18. Serengeti
19. Tanga mjini
20. Mbozi
21 .Ukonga
22 .Temeke
23.Kilombero
24 .Mikumi

Saturday, October 31, 2015

MATOAKEO YA DARASA LA SABA 2015: SHULE KUMI BORA HIZI HAPA

KUANGALIA MAJINA YA WANAFUNZI BONYEZA HAPA. CLICK HERE



Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 67.84, asilimia 10.85 zaidi ya ufaulu wa mwaka 2014 ambapo waliofaulu walikuwa asilimia 56.99.

Dar es Salaam.* Wahitimu 518, 034 kati ya 763, 602 waliofanya mitihani ya kuhitimu darasa la saba iliyofanyika nchini kote kuanzia Septemba 2 hadi Septemba 10, mwaka huu wamefaulu mitihani yao, Baraza la Mitihani
la Taifa (NECTA) limesema leo.

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 67.84, asilimia 10.85 zaidi ya ufaulu wa mwaka 2014 ambapo waliofaulu walikuwa asilimia 56.99.

Dkt Msonde amesema, ufaulu katika masomo yote umeongezeka kwa asilimia kati ya 4.61 hadi 17.22 ikilinganishwa na mwaka 2014 huku watahiniwa
wakifaulu zaidi somo la Kiswahili (asilimia 77.20) na kufaulu kwa kiwango cha chini katika somo la Kiingereza (asilimia 48.56.

Amesema kati ya watahiniwa wote waliofaulu 264, 130 ni wasichana ambao ni sawa na asilimia 64.60 ya wasichana wote 408, 900 waliotahiniwa huku wavulana wakiwa 253, 904 sawa na asilimia 71.58 ya wavulana 354, 706 waliotahiniwa.

Msondo amesema watahiniwa kumi bora wanatoka katika shule za Hazina iliyopo jijini Dar es Salaam, Mugini ya mkoani Mwanza na Twibhoki ya mkoani Mara huku wasichana 10 waliofanya vizuri wametoka shule za
Mugini, Twibhoki na Little flower ya mkoani Mara.

Katika matokeo hayo, Waja Springs ya Geita imeongoza katika orodha ya shule kumi zilizofanya vizuri nchini, ikifuatiwa na Enyamai ya mkoani Mara katika nafasi ya pili, nafasi ya tatu inashikiliwa na shule ya msingi Twibhoki ya mkoani Mara.

Shule nyingine na nafasi ilizoshika kwenye mabano ni; Mugini ya Mwanza(4), Rocken Hill ya Shinyanga (5), Karume ya Kagera (6), Alliance ya Mwanza (7), Little Flower ya Mara (8), Palikas ya Shinyanga (9) na Mtakatifu Caroli ya Mwanza (10).

Kwa mujibu wa matokeo hayo, shule ambazo hazikufanya vizuri katika matokeo hayo ni pamoja na Mwashigini ya Shinyanga, Mabambasi ya mkoani Simiyu, Mwangu iliyopo mkoani Lindi, Mohedagew ya mkoani Arusha na Kwale ya mkoani Pwani.

CHELSEA YAPOTEZA TENA

CHELSEA 1 LIVERPOOL 3

HATUTARUDIA UCHAGUZI WA ZANZIBAR WASEMA CUF


Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Twaha Taslima akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusiana na kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Kulia ni Makamu Mwenyeki wa Kamati hiyo, Severine Mwijage. Picha na Omar Fungo

Wakati CUF ikisema hayo, Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kimetaka kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza jinsi mwenyekiti wa ZEC alivyofikia uamuzi wa kufuta matokeo na akithibitika kuwa alishinikizwa, afukuzwe kazi.

Hatuwezi kurudia uchaguzi,” alisema Taslima. “Tunachofahamu ni kuwa uchaguzi umefutwa kinyume na sheria, hivyo ZEC ibatilishe uamuzi wake na kuendelea kutangaza matokeo ya majimbo yaliyobaki ili mshindi ajulikane.” Alisisitiza msimamo wa chama hicho kuwa Jecha alifuta matokeo hayo bila kuwashirikisha makamishna wake kama sheria ya tume hiyo inavyotaka. “Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 119 kifungu kidogo cha 10, inataka vikao vya ZEC kuhudhuriwa na mwenyekiti au makamu mwenyekiti na wajumbe wanne na uamuzi kuungwa mkono na walio wengi,” alisema. Alisema makamishna wa tume hiyo katika taarifa yao kwa vyombo vya habari wamepinga kuhusika katika uamuzi huo wa kufuta matokeo ya uchaguzi. Taslima alisema uamuzi huo umetolewa na Jecha mwenyewe kwa kushinikizwa na mamlaka za juu za Serikali. Aliziomba jumuiya za kimataifa kuzishinikiza serikali za Jamhuri ya Muungano na Zanzibar ili zimalize mgogoro huo na kuiepusha Zanzibar kuingia katika machafuko. Wakati CUF ikisema hayo, Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kimetaka kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza jinsi mwenyekiti wa ZEC alivyofikia uamuzi wa kufuta matokeo na akithibitika kuwa alishinikizwa, afukuzwe kazi.
Katibu wa ZLS, Omar Said Shaaban, ambaye alikuwa ameambaatana na rais wake, Wakili Awadh Ali Said, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tamko la Jecha la kufuta matokeo ya uchaguzi halina nguvu na linaweza kuhatarisha amani. “Rais aone haja ya kuunda Tume ya kumchunguza mwenyekiti dhidi ya madai ya kushindwa kufanya kazi zake na ikiwa madai hayo yakithibitika, basi
amuondoe mara moja,” alisema Shaaban kwenye mkutano huo uliofanyika
ukumbi wa Ulemavu, Kikwajuni. Wanasheria hao wametaka uchaguzi huo uendelee kuanzia pale ulipoishia, yaani hatua ya kufanya majumuisho ya kura za urais ili mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, 2015 apatikane na kutangazwa kuwa Rais. Chama hicho kimevitaka vyombo vya dola kuchunguza na kuwakamata na hatimaye kuwafikisha mahakamani watu wote waliohusika kumshinikiza mwenyekiti kutoa tamko la kufuta uchaguzi na matokeo yake.
Mbali ya hayo, chama hicho kimetoa wito kwa viongozi wote wa vyama vya siasa kutathmini wajibu wao katika kuheshimu maamuzi ya wananchi yanayofanywa kwa njia ya demokrasia ili kujenga misingi mizuri ya utawala bora.
 “Tunaamini kwamba Rais wetu wa Zanzibar atang’amua mtego huu unaokusudia kumuweka katika historia ya rais wa Zanzibar aliyewahi kuvunja katiba ya nchi na kumuondolea rekodi nzuri aliyonayo ya kuheshimu sheria na utawala bora,” alisema Shaaban. Kwa upande wake Rais wa chama hicho Awadh Ali Said alisema ZLS imepitia kwa makini katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi Nambari 11 ya 1984 ili kujiridhisha kama mwenyekiti ana uwezo wa kufuta matokeo ya Uchaguzi
na kama sababu zilizoelezwa zinakidhi kufanya uamuzi huo. Alisema kwa mujibu wa Ibara ya 119 (1) ya katiba ya Zanzibar ya 1984, tume ni mwenyekiti pamoja na wajumbe sita kama walivyoanishwa na ibara hiyo na kwamba maamuzi yoyote ya Tume, lazima yaungwe mkono na wajumbe walio wengi.
Alisema licha ya utashi huo wa kisheria, wajumbe wawili walieleza hadharani kuwa hawajashirikishwa. “Taarifa iliyotolewa kwa waandishi na wajumbe wa Tume, Nassor Khamis na
Ayoub Bakari, kuwa hakukuwa na kikao chochote kilichofikia uamuzi wa kufuta Uchaguzi wa Zanzibar, haijapingwa mpaka sasa na wajumbe wengine wa Tume. Hii inaleta taswira ya wazi kuwa uamuzi huo haukuwa wa Tume, bali ni wa mtu mmoja ambaye ni mwenyekiti, hivyo kuyafanya kuwa ni batili mbele ya macho ya Sheria,” alisema Said. Pia walisema kanuni ya 41(1) imeweka wazi utaratibu kufutwa kwa siku ya uchaguzi na kutangazwa siku nyingine na namna uamuzi huo utakavyofikiwa na sio kufuta matokeo ya uchaguzi au uchaguzi wenyewe.
“Ni kwa bahati mbaya sana mwenyekiti katika tamko lake hakueleza kama utaratibu umefuatwa. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa Sheria,” aliongeza kiongozi huyo wa ZLS. Alisema tamko hilo linaweza kuiingiza nchi katika mgogoro mkubwa wa kikatiba kama vile kumalizika kwa muda wa mwishowa utawala wa serikali ya sasa kwa mujibu wa ibara ya 28 (2) ya Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Ibara hiyo inaeleza kuwa rais ataacha madaraka yake baada ya kumalizika miaka mitano kuanzia tarehe alipokula kiapo. Katika hatua nyingine, mgombea urais wa ADC, Hamad Rashid amewaambia
waandishi wa habari jana kuwa kwenye ukumbi wa Hoteli ya Grand Malt, Malindi kuwa chama chake kimekosa imani na ZEC kutokana na uendeshaji wake kukosa sifa ya kufuata sheria na kanuni.
Alisema kuwa ili uwazi na uwajibikaji viweze kufikiwa, hakuna budi kwa watendaji wa tume huyo kujiuzulu na badala yake iundwe Tume yenye uwakilishi mpana na usio na mrengo wa kisiasa.
Alisema kuwa hatua hiyo kwa kiasi kikubwa inaweza kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi wa amani na utulivu huku demokrasia ikichukua mkondo wake. Nayo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imemshauri mwenyekiti wa ZEC kutafakari upya uamuzi wake wa kufuta matokeo ya uchaguzi. Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa THBUB,  Bahame Nyanduga inasema wamepitia sababu za  kufuta matokeo zilizotolewa na Jecha na kubaini kuwa zinaweza kutatuliwa iwapo makamishna wa ZEC wataweka tofauti zao pembeni. Nyanduga alisema katika taarifa hiyo kuwa kifungu cha 42(6) cha sheria ya uchaguzi Zanzibar kinaipa ZEC mamlaka ya kushughulikia
matatizo ya uchaguzi na kuyapatia ufumbuzi kwa utaratibu ulioanishwa katika kifungu hicho.
Taarifa hiyo ilisema kifungu hicho kinabainisha kwamba ZEC ina mamlaka ya kutangaza matokeo ndani ya siku tatu na endapo kuna matatizo inatakiwa kuyapatia ufumbuzi na kutangaza matokeo ndani ya muda huo. Wakati huohuo, Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon amesema
ameguswa na tatizo la kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar na kutaka limalizwe kwa kufuata sheria zilizopo kwa amani. Katika taarifa iliyotolewa juzi kutoka New York, Marekani, Moon
amewataka wananchi wa Zanzibar kuwa watulivu na kujiepusha na vitendo vya vurugu na kuwashauri viongozi kutotoa matamko yanayoweza kusababisha vurugu.

Fatuma Karume apinga
Naye Fatma Karume, mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amesema mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha hana mamlaka ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar. Jecha alitangaza kufuta matokeo yote  ya uchaguzi kwa upande wa visiwani Jumatano kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na sheria
katika upigaji kura.

Uamuzi huo umepingwa vikali na watu mbalimbali, huku waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Madola, Umoja wa Ulaya (EU), Umoja wa Afrika(AU) na ubalozi wa Marekani ukitaka ZEC ieleze ni vituo gani vilikuwa na ukiukwaji wa taratibu. Akizungumza na Sauti ya Ujerumani (DW) kuhusu suala hilo, Fatma alidai kuwa Jecha alishinikizwa kuchukua uamuzi huo. “Watu waliwekwa chini ya ulinzi... na wakati huo Jecha hakuwepo,” alisema Fatma.  “Tusema ukweli, Jecha hana jeshi wala polisi. Jecha katumiwa tu kusemamaneno yale. Wazanzibari tumenyimwa haki yetu,” alisema binti huyo wa Rais wa Sita wa Zanzibar. Fatma alisisitiza kuwa uchaguzi haujafutwa kwa kuwa Jecha hana mamlaka ya kufuta uchaguzi na kwamba Serikali imehakikisha matokeo ya uchaguzi
hayatoki.  “Uchaguzi wa Zanzibar ni haki ya Wazanzibari na hakuna mtu anaweza kufuta hiyo haki. Uchaguzi bado upo na wote tumepiga kura, kura zetu zipo na hakuna mtu anaweza kufuta hiyo,” alisisitiza Fatma. Alisema kwa mujibu kwa Katiba ya Zanzibar Baraza la Wawakilishi lilivunjwa Agosti 13, na Katiba hiyo inataka baada ya siku tusini kuwe na Baraza jipya la Wawakilishi. Alisema kama ikifika Novemba 11 au 12 hakuna baraza jipya la wawakilishi, Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein atakuwa anavunja taratibu za kikatiba iwapo ataendelea kuwa Rais.


NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR