Saturday, November 14, 2015

KAMA HAUJAWAHI KUFIKA SERENGETI SASA HAYA NDIYO MAAJABU YA SERENGETI

Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania  kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.
Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya zamadamu yalipatikana liko ndani ya Serengeti.
Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia katika kaskazini-magharibi mwa Tanzania na inaenea kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. Inaenea kiwango cha mraba kilometa 30,000 2.
Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi duniani, ambao hua ni tukio wa nusu mwaka . Uhamiaji huo ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu ya kusafiri.
Kanda hii ina hifadhi za taifa na hifadhi mchezo kadhaa. Jina Serengeti limechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai hasa, "Serengit" kumaanisha "Kiwara kisichoisha".
Inakadiriwa mamalia 70 kubwa na baadhi ya spishi 500 avifauna (yaani ndege) hupatikana huko. Tofauti hii ya juu upande wa spishi ni shughuli makazi mbalimbali kuanzia misitu ya riverine, mabwawa, kopjes mbuga na misitu.  Nyumbu bluu, swara, punda milia na nyati ni baadhi ya mamalia kubwa ambao kwa kawaida hupatikana katika kanda hii.
Karibu Oktoba, karibu wanyama wanaokula majani (si nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za mvua. Katika mwezi Aprili, wao hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena kuvuka Mto wa Mara. Jambo hili la mara kwa mara huitwa kwa Kiingereza "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu zaidi ya 250,000 pekee watakufa safarini kutoka Tanzania kwenda katika mbuga ya wanyama ya Masai Mara huko Kenya pande za juu, ambayo ni jumla ya maili 500. Kifo mara nyingi unasababishwa na maudhi au uchovu.  Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani.



ANGALIA MECHI YA TANZANIA VS ALGERIA LIVE HAPA

Paris shootings and explosions: In pictures

France has declared a national state of emergency and tightened borders after at least 128 people were killed in a night of gun and bomb attacks in Paris.
Eighty people were reported killed after gunmen burst into the Bataclan concert hall and took hostages before security forces stormed the hall.
People were shot dead at restaurants and bars at five other sites in Paris. At least 180 people were injured.
 Fans on pitch at Stade de France

These are the deadliest attacks in Europe since the 2004 Madrid bombings.
French President Francois Hollande, visibly shaken, called Friday night's almost simultaneous attacks "a horror" and vowed to wage a "merciless" fight against terrorism.
Paris saw three days of attacks in early January, when Islamist gunmen murdered 18 people after attacking satirical magazine Charlie Hebdo, a Jewish supermarket and a policewoman on patrol.

The attack on the 1,500-seat Bataclan hall was by far the deadliest of Friday night's attacks. Gunmen opened fire on concert-goers watching US rock group Eagles of Death Metal. The event had been sold out.
"At first we thought it was part of the show but we quickly understood," Pierre Janaszak, a radio presenter, told Agence France Presse.
Police officers arrive at the scene of a shooting in Paris France 13 November 2015

"They didn't stop firing. There was blood everywhere, corpses everywhere. We heard screaming. Everyone was trying to flee."
He said the gunmen took 20 hostages, and he heard one of them tell their captives: "It's the fault of Hollande, it's the fault of your president, he should not have intervened in Syria".
Within an hour, security forces had stormed the concert hall and all four attackers there were dead. Three had blown themselves up and a fourth was shot dead by police.
 Police officers secure the Stade de France stadium during the international friendly football game France against Germany

Attack sites:

La Belle Equipe, 92 rue de Charonne, 11th district - at least 19 dead in gun attacks
Le Carillon bar and Le Petit Cambodge restaurant at rue Alibert, 10th district - at least 12 dead in gun attacks
La Casa Nostra restaurant, 92 rue de la Fontaine au Roi, 11th district - at least 5 dead in gun attacks
Stade de France, St Denis, just north of Paris - explosions heard outside venue, three attackers dead
Bataclan concert venue, 50 boulevard Voltaire, 11th district - stormed by several gunmen, at least 80 dead
map of attack sites







Sunday, November 8, 2015

DR. HELEN KIJO BISIMBA APATA AJALI

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dr. Helen Kijo Bisimba amepata ajali ya gari leo asubuhi katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam. 
Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva wake ambaye naye inasemekana amejeruhiwa. Hivi sasa Mkurugenzi huyo wa LHRC anapatiwa matibabu katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaa.Taarifa zaidi kuwajia

 
 

Thursday, November 5, 2015

WANAFUNZI WAKOSA MIKOPO KUSHINDWA KUENDELEA NA ELIMU YA JUU

ZAIDI ya wanafunzi 50,000 watashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kutokana na kushindwa kupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

Hayo yamebainika ikiwa ni siku tatu tangu HESLB kutoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016, huku idadi kubwa ikiwa haimo katika majina hayo.
Katika mwaka huu wa masomo bodi ya mikopo imeweza kuwapatia mikopo wanafunzi 12,000 pekee sawa na 17.1% ya waombaji zaidi ya 70,000, hivyo kufanya idadi ya wanafunzi waliokosa mikopo kufikia asilimia 82.9 ya waombaji wote.
Wanafunzi waliokosa mikopo ya kuwawezesha kujiunga na elimu ya juu na hivyo wazazi wao kutakiwa kugharamia elimu hiyo wameelezea kusikitishwa na hali hiyo huku wakiitaka serikali kuwaangalia kwa jicho la kipekee kwani hawana uwezo wa kuanza masomo pasipo kufadhiriwa na serikali.
Wanafunzi hao walionekana kukata tamaa ya kutimiza ndoto yao ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu, wamefika makao makuu ya bodi hiyo huku wakiongozana na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutaka kujua hatima yao.
“Nimetokea Tabora, wazazi wangu walinipa Sh. 100,000 ya kutumia wakiamini tunapewa mikopo na serikali, lakini tumenyimwa na hatujui hatima yetu, nimebakiwa na Sh. 6,000, naomba serikali ituhurumie, isikie kilio chetu hatustahili kuteseka hivi,” ameeleza Abdul Omary mwanafunzi mteule UDSM.
Fatuma Bakari, mwanafunzi mwingine kutoka UDSM, amesema: “Siwezi kujiunga na Chuo bila mkopo, tumefika hapa ili kuomba bodi ya mikopo itusaidie hatuna tumaini lolote zaidi ya kuomba Mungu atusaidie tuweze kupata mikopo na kuanza masomo.”
Waziri wa Mikopo serikali ya wanafunzi (Daruso), Shitindi Venance ameeleza kutokukubaliana na majibu waliyopewa na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo kwani yanakatisha tamaa na kuzima ndoto za wanafunzi wa masikini kusoma chuo kikuu.
“Hapa UDSM ni wanafunzi 600 tu waliopata mikopo kati ya wanafunzi 7,000 waliopangiwa kuanza masomo, hili ni janga kubwa kwa watoto wa masikini kwani hawawezi kujisajili chuoni wala kupata makazi katika mabweni mpaka walipe ada na wengi wametoka mikoani.
“Tunachukua hatua moja mbele na kuamua kulifuatilia suala hili kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na katibu mkuu wa wizara ya fedha kwa sababu bodi bado wanasisitiza tuwe na subira ilihali muda umeenda na wanafunzi wanateseka” ameeleza Shitindi.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole amewaambia wanahabari waliofika ofisini kwake kuwa bodi haistahili kulaumiwa kwani serikali kupitia wizara ya fedha na wizara ya elimu ndio yenye uwezo wa kutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji ya wakati husika.
“Lengo la bodi ya mikopo ni kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu kusoma kwa ufadhili wa serikali na wala sio kuwakwamisha, tunaendelea kujadiliana na serikali kuona kama itatuongeza fedha ili tuweze kutoa awamu ya pili ya majina ya wanafunzi waliopata mikopo, tunawaomba wanafunzi wavute subira,” anaeleza Ngole
Hata hivyo Ngole amesema hawezi kusema lini watatangaza majina ya awamu ya pili kwani hilo linategemea ni lini serikali itatoa fedha kwa ajili ya wanafunzi wa awam ya pili.
Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali ilitoa mikopo kwa wanafunzi 30,000 sawa na 51.7% ya waombaji wote 58,000 na hivyo kufanya waliokosa mikopo kuwa wanafunzi 28,000 sawa na 49% pekee tofauti na mwaka huu ambapo waliokosa wamefikia asilimia 82.9

SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA AWAMU YA TANO DK JOHN POMBE MAGUFULI







https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3e4xiDTe-gNu3cEof0uk54uLn1JIxKdQO_YgZDQEozuZDU23GfdDbQBzyt6nLTzGMnacXlAf4sNvqysWjGeCQ-hYgYdjZBvYFLOUV-dp7aALWWETCiI5ObwM5M-IJGa2LIFqy8wRlUCIo/s1600/jpm3.jpg

















https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEicojLPXC4jzE3xHi0IKcFx4jD_6gGUkbLxq6DAzVwJrqpVM926aKZ0ReyOW97eCdT6nKAmf3_Hb0Ypa6LCFDY5Pio3I9PVZLEsD1ksqEoH_Eo4c-1uXFhXqHPS_g4PP4vHOlkHZ6e_IL5z/s1600/jpm5.jpg

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbh6pIOYGJOi_2NNAyyzwGTRiTWDaYOMJ8T51Zu71SbgdiD3mdawAKfUVddsSqrS_BlkJm2Kaw1B5vU6cnz1UjqnP0qooInvxwG2lgIZOXuheBS8peJiunzxBJ46bVX7wCLSnfHvmKe5jK/s1600/jpm6.jpg

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR