Wednesday, March 23, 2016

MADHARA YA KUANGALIA VIDEO ZA NGONO(PORNOGRAPH)

Madhara Yanayosababishwa na Ponografia
HABARI ya kila aina kuhusu ngono inapatikana kwa urahisi kupitia televisheni, sinema, video za muziki, na Internet. Je, ni kweli kwamba habari hizo chungu nzima za ponografia hazina madhara, kama watu wengi wanavyotaka tuamini?*
Jinsi Ponografia Inavyowaathiri Watu Wazima
Hata watetezi waseme nini, ponografia inaathiri sana maoni ya watu kuhusu ngono na maadili. Watafiti kwenye Hazina ya Taifa ya Utafiti na Uelimishaji wa Jamii walikata kauli kwamba “kutazama ponografia kunaweza kuwafanya watazamaji wafanye ngono potovu.” Ripoti hiyo inasema “imani ya kwamba wanawake husababisha na hufurahia ubakaji, na kwamba wabakaji ni watu wa kawaida imeenea sana miongoni mwa wanaume wenye zoea la kutazama ponografia.”
Watafiti fulani wanasema kwamba kuzoea kutazama ponografia kunaweza kuathiri uwezo wa kufurahia na kufanya ngono katika ndoa. Dakt. Victor Cline, mtaalamu wa kutibu watu wanaotawaliwa na mambo ya ngono, ametambua kwamba watu wanaotazama ponografia huendelea tu bila kuacha. Mtu anayeanza kutazama ponografia kidogo-kidogo, asipoacha mwishowe anaweza kuwa na zoea la kusoma habari na kutazama picha chafu zaidi za ponografia. Cline anadai kwamba zoea hilo linaweza kuongoza kwenye matendo mapotovu ya ngono. Wanasayansi wanaochunguza tabia za wanadamu wanakubaliana na jambo hilo. Dakt. Cline anaripoti kwamba “upotovu wowote wa ngono unaweza kuanza hivyo . . . na kwamba mtu hawezi kuacha hata akisumbuliwa sana na dhamiri.” Hatimaye, huenda mtu anayetazama ponografia akajaribu kufanya mambo yasiyo ya adili aliyoona, na mara nyingi matokeo huwa mabaya.
Tatizo hilo linaweza kuanza hatua kwa hatua bila kutambuliwa, asema Cline. Aongeza: “Huongezeka na kuenea kama kansa. Kwa kawaida zoea hilo halikomi, wala haliwezi kutatuliwa kwa urahisi. Haishangazi kwamba mara nyingi wanaume waliozoea kutazama ponografia hawakubali kwamba wana tatizo, na ni kawaida kwa wenzi wa ndoa kukosana, nyakati nyingine kutalikiana, na hata mahusiano mengine ya karibu huharibika kwa sababu hiyo.”
Jinsi Vijana Wanavyoathiriwa
Takwimu zinaonyesha kwamba watazamaji wengi wa ponografia ni wavulana wenye umri wa kati ya miaka 12 na 17. Kwa kweli, wengi wao hujifunza masuala ya ngono hasa kupitia ponografia. Hilo lina matokeo mabaya sana. Ripoti moja yasema kwamba “ponografia hazionyeshi kamwe mimba za matineja na magonjwa yanayoambukizwa kingono kama UKIMWI, na hilo hutokeza wazo la uwongo la kwamba mambo yanayoonyeshwa katika ponografia hayana madhara.”
Watafiti fulani husema kwamba kutazama ponografia kunaweza pia kuathiri ukuzi wa kawaida wa ubongo wa mtoto. Dakt. Judith Reisman, mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Vyombo vya Habari, akata kauli: “Uchunguzi wa athari za sauti na picha za ponografia katika utendaji wa kawaida wa ubongo unaonyesha kwamba kutazama ponografia huathiri kabisa uwezo wa kawaida wa kufikiri. Pia hudhuru ubongo wa watoto unaoathiriwa kwa urahisi kwa sababu hufanya wasione mambo kihalisi na hudhuru afya yao ya kiakili na ya kimwili, na huwazuia kupata furaha.”
Jinsi Mahusiano Yanavyoathiriwa
Ponografia huathiri mitazamo na tabia. Ujumbe wake unavutia hasa kwa sababu si halisi na hivyo unaifanya ionekane kuwa yenye kusisimua zaidi kuliko mambo halisi. (Ona sanduku “Utakubali Ujumbe Gani?”) “Watu wanaotazama ponografia hutarajia mambo yasiyo halisi ambayo huharibu mahusiano,” yasema ripoti moja.
Ponografia inaweza kuwafanya wenzi wa ndoa wakose kuwa wanyofu na wakose kuaminiana, sifa ambazo ni muhimu katika ndoa. Kwa sababu ponografia hutazamwa hasa faraghani, mara nyingi humfanya mtu atumie hila na uwongo. Wenzi wa ndoa huhisi kwamba wamesalitiwa. Hawaelewi kwa nini mwenzi wao havutiwi nao tena.
Madhara ya Kiroho
Ponografia husababisha madhara mabaya ya kiroho. Inaweza kuwa kizuizi kikubwa kwa mtu anayetaka kuwa na uhusiano na Mungu.* Biblia huhusianisha hamu ya ngono na tamaa na ibada ya sanamu. (Wakolosai 3:5) Mtu anayetamani kitu huwa na hamu kubwa sana ya kukipata hivi kwamba kinakuwa jambo kuu maishani mwake kuliko vitu vingine vyote. Kwa kweli, wale ambao wamezoea ponografia hutanguliza tamaa zao za ngono badala ya Mungu. Kwa hiyo wanazifanya kuwa sanamu yao. Amri ya Yehova Mungu inasema: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.”—Kutoka 20:3.
Ponografia huharibu mahusiano yenye upendo. Mtume Petro, ambaye alikuwa amefunga ndoa, aliwahimiza waume Wakristo wawaheshimu wake zao. Mungu hatasikiliza sala za mume anayekosa kufanya hivyo. (1 Petro 3:7) Je, mtu anayetazama picha chafu za wanawake faraghani anamheshimu mke wake? Mke angehisije akigundua? Na Mungu ambaye “ataleta hukumuni kila kazi” na ambaye “huzipima roho” angeonaje? (Mhubiri 12:14; Mithali 16:2) Je, mtu anayetazama ponografia anaweza kumtarajia Mungu asikilize sala zake?
Ponografia hukazia kutosheleza tamaa za mtu binafsi kwa vyovyote vile. Kwa hiyo, kutazama ponografia ni kukosa upendo. Hudhoofisha uwezo wa Mkristo wa kudumu akiwa safi kiadili na kuwa mwadilifu mbele za Mungu. “Haya ndiyo mapenzi ya Mungu,” akaandika mtume Paulo, “kwamba mjiepushe na uasherati; kwamba kila mmoja wenu apaswe kujua jinsi ya kupata umiliki wa chombo chake mwenyewe katika utakaso na heshima, si katika hamu yenye tamaa ya ngono . . . , kwamba yeyote asifikie hatua ya kudhuru na kuziingilia haki za ndugu yake.”—1 Wathesalonike 4:3-7.
Ponografia huwatumia vibaya hasa wanawake na watoto. Huwavunjia heshima na pia huwashushia hadhi na kuwanyima haki zao. Yule anayetazama ponografia hushiriki na kuunga mkono matumizi hayo mabaya ya wanawake na watoto. ‘Hata mtu akijiona kuwa mwema kadiri gani,’ wasema watafiti Steven Hill na Nina Silver, ‘anapotazama au kukubali ponografia, anakuwa asiyejali au hata mwenye chuki kuelekea mtu anayedai eti anamjali.’
Kuacha Zoea la Kutazama Ponografia
Vipi ikiwa unapambana na zoea la kutazama ponografia? Je, kuna lolote unaloweza kufanya ili kuacha zoea hilo? Biblia hutoa tumaini! Kabla ya kumjua Kristo, baadhi ya Wakristo wa awali walikuwa waasherati, wazinzi, na wenye pupa. Hata hivyo, Paulo alisema, “lakini mmeoshwa mkawa safi.” Hilo liliwezekanaje? Paulo ajibu: “Mmetakaswa . . . kwa roho ya Mungu wetu.”—1 Wakorintho 6:9-11.
Usipuuze kamwe nguvu za roho takatifu ya Mungu. “Mungu ni mwaminifu,” yasema Biblia, “naye hatawaacha nyinyi mshawishwe kupita vile mwezavyo kuhimili.” Kwa kweli, ataandaa njia ya kutokea. (1 Wakorintho 10:13) Kusali kwa bidii—kumwambia Mungu shida zako daima—kutakuwa na matokeo mazuri. Neno lake hutia moyo hivi: “Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza.”—Zaburi 55:22.
Bila shaka, lazima utende kupatana na sala zako. Unahitaji kuazimia kutoka moyoni kukataa ponografia. Rafiki unayemtumaini au mshiriki wa familia anaweza kukusaidia sana, akikupa utegemezo na kitia-moyo unachohitaji ili kushikamana na azimio lako. (Ona sanduku “Kupata Msaada.”) Kukumbuka kwamba hatua hiyo itampendeza Mungu kwaweza kukusaidia uendelee kushikamana na azimio lako. (Mithali 27:11) Kwa kuongezea, kujua kwamba kutazama ponografia kunamchukiza Mungu kwaweza pia kukuchochea uache zoea hilo. (Mwanzo 6:5, 6) Haitakuwa rahisi, lakini unaweza kufaulu. Unaweza kuacha zoea la ponografia!
Kwa kweli, ni hatari kutazama ponografia. Inadhuru na kuharibu. Inawapotosha wale wanaoitayarisha na pia wale wanaoitazama. Huwashushia heshima wanaume na wanawake, ni hatari kwa watoto, na ni zoea ambalo linapasa kupingwa.

SPIKA WA BUNGE AFANYA MAAMUZI MAPYA YA KUWANGOA


Dar es Salaam. Spika John Ndugai amefanya mabadiliko ya wajumbe 27 wa
Kamati za Kudumu za Bunge yaliyowangoa wenyeviti watano, huku mmoja
akipoteza nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bunge.

Hatua hiyo imekuja wakati kukiwa na tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge wa
baadhi ya kamati na kusababisha baadhi kujiuzulu ujumbe wakishinikiza
uchunguzi ufanyike ili waliohusika wawekwe hadharani na kuchukuliwa hatua.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliacho cha
Bunge inasema Spika Ndugai amefanya mabadiliko hayo kwa kuzingatia
mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda kamati hizo
siku 59 zilizopita.

Waliongolewa uenyekiti ni Richard Ndassa, ambaye alikuwa Kamati ya
Uwekezaji na Mitaji (PIC), Dk Mary Mwanjelwa (Kamati ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira), Martha Mlata (Kamati ya Nishati na Madini).

Waliovuliwa umakamu mwenyekiti ni Dk Raphael Chegeni (Kamati ya Huduma
za Maendeleo ya Jamii) na Kangi Lugola (Kamati za Hesabu za Serikali).

Mabadiliko haya yamefanywa chini ya Kanuni ya 116(3) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge ambayo inatoa mamlaka ya kuteua wabunge kuunda kamati
mbalimbali za Bunge,รข€ inasema taarifa hiyo.

Kwa kuhamishwa kutoka kamati wanazoziongoza, wabunge hao wamepoteza
nafasi zao za uenyekiti, wakati Mwanjelwa, ambaye alipata nafasi ya
Mwenyekiti wa Bunge kutokana na kuwa mmoja wa wenyeviti wa kamati hizo,
amepoteza wadhifa huo wa kuwa mmoja wa wenyeviti watatu ambao humsaidia
Spika kuongoza shughuli za Bunge.

Sifahamu chochote, alisema Dk Mwanjelwa, mmoja wa wenyeviti watatu wa
Bunge, alipoulizwa na Mwananchi kuhusu mabadiliko hayo.

Ninachoweza kusema uamuzi wa Spika ndiyo wa mwisho, ila sina
ninachofahamu kuhusiana na mabadiliko haya. Yaani ndiyo nimesoma kwenye
mtandao muda si mrefu kabla hamjanitafuta.

Taasisi za Serikali zinazotuhumiwa kutoa fedha kwa wajumbe wa Kamati za
Bunge, ambazo zina jukumu la kuzisimamia, ni Shirika la Nyumba (NHC),
Bima ya Afya (NHIF), Shirika la Umeme (Tanesco) na Mamlaka ya Udhibiti
wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo alisema suala la
taasisi yake kutoa rushwa kwa wabunge limewashangaza, na wanasubiri
vyombo vya uchunguzi kutoa matokeo kuhusu tuhuma hizo.

Matokeo ya uchunguzi kuhusu tuhuma hii ndiyo ambayo yanaweza kuanika
bayana kama kweli tunahusika au lah. Ni jambo ambalo hata sisi
limetushangaza, alisema.

Kutokana na mabadiliko hayo, kamati ambazo viongozi wake wameondolewa
zitalazimika kufanya uchaguzi wa viongozi.

Kamati zinazotakiwa kupata wenyeviti wapya ni ya Nishati na Madini,
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma na Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii
ambayo itatakiwa kufanya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake, wakati
zitakazochagua makamu ni ya Hesabu za Serikali ya Mitaa (LAAC) na ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Waliohamishwa wazungumza

Akizungumzia suala hilo, Dk Chegeni alisema wajumbe wawili wa kamati
yake, Zitto Kabwe (Kigoma Mjini) na Hussein Bashe (Nzega Mjini),
wamemuandikia Spika barua za kujiondoa kwenye nafasi zao ili kupisha
uchunguzi wa rushwa.

Wajumbe wa kamati wamesikitishwa na taarifa hizi na kwa pamoja tumeamua
kuchukua hatua. Tumemuandikia Spika barua ya kupisha uchunguzi ili
kujiridhisha na madai yaliyobainishwa. Wajumbe wote waliohudhuria kikao
cha leo wamesaini,รข€ alisema Dk Chegeni.

Zitto aliiambia Mwananchi kuwa amemuandikia Spika barua ya kujiondoa,
akitaka uchunguzi ufanyike na atakayehusika achukuliwe hatua kali.

Bashe alithibitisha kujiondoa akitaka uchunguzi ufanyike na watuhumiwa
wote watajwe kwa majina ili hatua zichukuliwe.

Utumishi wangu kwa kamati uko palepale nisingependa kuhamishwa lakini
watuhumiwa wajulikane,รข€ alisema Bashe.

Akizungumzia taarifa zilizochapishwa na gazeti moja jana, Dk Chegeni
alisema: Si kweli. Hata huyo katibu anayeelezwa kutumwa hakuwa nasi
mpaka mwisho wa ziara pale Bima ya Afya. Alitoa udhuru kuwa mwanaye
anaugua na akaruhusiwa kuondoka mapema tu. Leo (Jana) kamati imewauliza
wajumbe na makatibu wote na wamekana kuhusika.

Baada ya kujiridhisha na kutohusika kwa wajumbe wake, Dk Chegeni alisema
kamati imepitisha maazimio matatu, ambayo ni kutaka uchunguzi ufanyike
ili ofisi ya Spika ijiridhishe, watakaobainika wachukuliwe hatua za
kikanuni na kisheria, na gazeti lililoandika habari hiyo lithibitishe
tuhuma hizo na likishindwa liiombe msamaha kamati.

Jana (juzi) nilitumwa na mwenyekiti wangu nihudhurie kikao Spika
kilichokuwa kifanyike saa 5:00 asubuhi, lakini kiliahirishwa. Leo (jana)
hajahudhuria kikao chetu na kanijulisha kuwa anahudhuria kikao hicho
kikichoahirishwa jana (juzi). Sina taarifa za mahojiano na Takukuru,
alisema Lolencia Bukwimba akimzungumzia Ndassa.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema hajajiuzului ujumbe wa
kamati kama habari zilivyoenea, lakini yeye pamoja na wajumbe wenzake wa
Kamati ya Huduma za Jamii wamemtaka Spika awaeleze kilichotokea kwa kuwa
ndiye kiongozi wao.

Kwa mfano mimi nijiuzulu nini wakati si mtuhumiwa? alihoji.

Nikijiuzulu, maana yake naacha kazi za kibunge.

Alisema anashangaa habari kama hizo zinatokea wapi wakati hajasikia kama
kuna mbunge yeyote aliyehojiwa dhidi ya tuhuma hizo.

Kuhusu tuhuma za rushwa, Mbilinyi alisema si rahisi kwa kitu hicho
kutokea kwa kuwa wabunge hawawezi kuwatuma makatibu wa kamati kufuata
fedha za rushwa.
Kwa sababu huwa tunawaona kama wapelelezi, hivyo si rahisi mtu
akamuamini kiasi cha kumtuma akamchukulie mzigo, alisema.

Pia alisema kwa wakati huu ambao Bunge ni changa, haiwezi kuwa rahisi
wakakubaliana kuchukua rushwa kwa kuwa bado wabunge hawajafahamiana vizuri.

Mbunge wa Jimbo la Bukene, Selemani Zedi alisema hajapata taarifa rasmi
za kuhamishwa kutoka kamati ya PIC kwenda ya Katiba.

Nitawajibika kwenye kamati nitakayopangwa kwa sababu spika anayo
mamlaka ya kunipanga popote,alisema.

Kuhusu vitendo vya rushwa, alivitaka vyombo husika kufanya uchunguzi ili
atakayebainika kuhusika achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Mwaka 2012, wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini walituhumiwa kupokea
hongo kutoka kwenye makampuni ya mafuta ili waunge mkono azimio la
kushinikiza aliyekuwa katibu mkuu wa wizara husika, Eliackim Maswi
angolewe.

Wakati huo, Spika Anne Makinda aliahidi kuwapeleka watuhumiwa kwenye
Kamati ya Maadili na Haki za Bunge ili wachunguzwe na kuahidi kuwa
matokeo ya ripoti hiyo angeiwasilisha bungeni.

Siku hiyo, Spika Makinda pia alitangaza kuivunja kamati ya nishati.

Tuesday, March 22, 2016

MJUE TEMBO (NDOVU) MNYAMA MKUBWA

Ndovu au TemboNdovu au tembo ni aina za wanyama wenye umbo kubwa kupita wanyamapori wote. Watoto wake wakizaliwa hufikia kg 100 na ndovu mzima huwa na uzito wa tani 2 hadi 5; kimo ni hadi m 4.
Kibiolojia ni mamalia. Sehemu ya pekee mwilini ni mwiro ambao hali halisi ni pua la tembo lililorefuka na kufanya kazi pia kama mkono wake yaani kwa kutumia mwiro ndovu hushika vitu na kufanya utafiti kwa kugusagusa.

Pembe-jino zake zinatafutwa sana kama mapambo na biashara ya pembe za ndovu imeshakuwa hatari kabisa kwa ndovu wote kwa sababu wanawindwa mno. Hivyo kwa mapatano ya kimataifa biahsara ya pembe hizi imepigwa marufuku.







Kwa jumla kuna spishi tatu za Tembo ambao wanafanana lakini hawazai pamoja. Tembo-nyika ambao ni wakubwa kuliko wengine.
Tembo wa Asia ni wadogo kwa Tembo Nyika lakini anazoea wanadamu kwa hiyo katika nchi kama Uhindi au Uthai hutumiwa kama mnyama wa kazi akibeba mizigo au watu. Zamani spishi hii ilitumiwa hata vitani. Kwa mfano jemadari Hanibal wa Karthago alishambulia Dola la Roma kwa msaada wa Tembo wa kijeshi waliovuka milima ya Alpi.
Tembo-misitu, Tembo huyu asili yake ni  Afrika lakini wataalamu wamethibitisha ni spishi tofauti. Hufikia kimo cha mita 2 tu anaishi hasa katika misitu ya Kongo.

Spishi za Afrika

  • Loxodonta africana, Ndovu-nyika (African Bush Elephant)
  • Loxodonta cyclotis, Ndovu-misitu (African Forest Elephant)

Spishi ya Asia

  • Elephas maximus, Ndovu wa Asia (Asian Elephant)
  •   Tembo hula  majani. Kwa chakula hiki ambacho ni kigumu hutegemea meno yao.
    itaendelea

WAJUE MAMEYA WA MANISPAA ZA ILALA, KINONDONI NA TEMEKE JIJI LA DAR ES SALAAM





Meya
                      HON. CHARLES KUYEKO
                    ILALA MUNICIPAL
                               MAYOR


Image result for meya wa temeke 2016
 HON. CHAUREMBO ABDALAH JAFAR
                TEMEKE MUNICIPAL
                          MAYOR

MEYA MPYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM NI MH. ISAYA CHACHA

  Kaimu Mkurugenzi Jiji la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Mhe. Isaya Chacha Diwani wa Kata ya Vijibweni (CHADEMA) kutoka Manispaa ya Temeke kuwa Meya Mpya wa Jiji hilo.
 
Kaimu Mkurugenzi huyo alimtangaza Isaya kuwa mshindi mara baada ya uchaguzi huo kufanyika leo  jijini Dar es Salaam ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67 wakati kura 7 ziliharibika katika uchaguzi huo.

Sunday, January 10, 2016

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHA WAKAZI WA MABONDENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM


Utangulizi
Nchi yetu ina kingo za mito na mabonde na maeneo mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao.  Kutokana na uhaba wa makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la Mto Msimbazi.
 
Serikali za awamu zote, zimekuwa zikifanya jitihada za kuwaondoa wakazi wa maeneo ya mabondeni wanaoishi katika maeneo hayo kinyume cha sheria lakini mafanikio yamekuwa si ya kuridhisha.

Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo moja ya misingi yake mikuu ni utii wa sheria za nchi, imeanza jitihada za kuwaondoa wakazi hawa. 
Tuliamua kuanza na Bonde la Mto Msimbazi kwasababu ndiko kwenye watu wengi na athari kubwa.Sababu zetu kuu za kufanya zoezi hili ni kusafisha mabonde na mito katika jiji la Dar es Salaam na mazingira yanayozunguka ni:-

Kunusuru maisha ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi. Eneo la Bonde la Mto Msimbazi lilitangazwa kuwa ni eneo hatarishi kuishi binadamu tangu mwaka 1949 na baadaye 1979.

Kupanua uwezo wa mito ya Dar es Salaam ili kupitisha maji ya mvua kwa kasi kubwa, hivyo kupunguza uwezekano wa kutokea mafuriko na maafa wakati wa mvua nyingi;Kuzuia milipuko ya magonjwa, hasa ya kipindupindu, hasa wakati wa mvua;

Kuzuia eneo hilo kuendelea kutumika kama maficho ya wahalifu na uhalifu;

Kutoa nafasi kwa Serikali kuandaa na kuendeleza eneo hilo kwa mujibu wa sheria za nchi na mipango miji;

Utaratibu wa Zoezi
Kabla ya nyumba kubomolewa, taasisi hizi zinashirikiana kuhakiki iwapo nyumba anayokaa mkazi ina nyaraka za umiliki na vibali vya ujenzi na iwapo nyaraka hizo zina uhalali wowote. 
 
Nyumba ambazo zimethibitika kuwepo katika maeneo yasiyostahili ndio zinawekwa alama X kuashiria kwamba wakazi wanapaswa kuhama au kubomoa. Baada ya hapo, mkazi hupewa muda wa kubomoa na kuhama mwenyewe.

Kutokana na utaratibu huu, sehemu kubwa ya nyumba zinazobomolewa ni zile ambazo watu wamekwishaamua kubomoa wenyewe. 
 
Baada ya hapo, alama huwekwa kuonyesha mpaka wa bonde. Katika zoezi hili, imebainika kwamba sehemu kubwa ya wakazi wa maeneo ya mabondeni ni wapangaji huku wamiliki wakikaa sehemu nyingine salama.
 Serikali pia imeweka Dawati la Malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tathmini ya Zoezi
Jana, terehe 7 Januari 2016, Mawaziri watatu (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI; na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais; pamoja na Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii), walifanya mkutano wa kutathmini zoezi la kuhamisha wakazi wa mabondeni katika Jiji la Dar es Salaam. 

Mkutano huo ulipokea ripoti ya timu ya wataalam wa Wizara mbalimbali, inayoongozwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambayo, pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba sehemu kubwa ya kubaini makazi yaliyojengwa kinyume cha Sheria katika Bonde la Mto Msimbazi imekamilika. 
Ripoti ilieleza kwamba, hadi sasa, wananchi katika nyumba 774  wamehama na nyumba hizo kubomolewa. Ilielezwa pia kwamba kabla ya mkazi kuombwa  kuhama, uhakiki kuhusu uhalali wa makazi anayoishi hufanywa. 
Kutokana na uhakiki huo, jumla ya wakazi 20 walikuwa na hati halali za makazi na wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi. 
Hawa watu hawakuhamishwa. Mawaziri walipokea maelezo kuhusu changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika zoezi hilo.  
Baada ya tafakuri na mjadala, Mawaziri hao walitoka na msimamo ufuatao, kama uamuzi wa Serikali: -

1.Zoezi la kuwaondoa wananchi waishio katika bonde la Mto Msimbazi (eneo hatarishi) litaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta mateso na usumbufu kwa wananchi;

2.Katika awamu hii, zoezi litajikita katika Bonde la Mto Msimbazi tu.

3.Kwa wakati huu, watakaohitajika kuhama ni wale tu ambao makazi yao yamo NDANI kabisa ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia bondeni na kwenye KINGO za mto;

4.Wale watakaokuwa na nyaraka halali walizopewa na mamlaka za umma, zilizowamilikisha na kuwaruhusu kujenga katika bonde hilo, hawatahamishwa bila kupewa sehemu nyingine za kujenga. Na watumishi wa umma waliowamilikisha maeneo hayo watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria;

5.Serikali, ndani ya siku tatu zijazo, itaanza zoezi la kuzoa kifusi na kusafisha maeneo ambapo ubomoaji umefanyika.

6.Serikali itaheshimu amri za mahakama kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na baadhi ya wakazi wa mabondeni lakini pia itafuatilia kesi hizi ziishe haraka ili taratibu zinazofuatia zifanyike;

7.Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wake wanaoendesha zoezi hili kinyume na misingi ya sheria zinazotekelezwa, na kinyume na misingi ya haki na uwazi, ikiwemo wanaoweka alama za X zaidi ya mita zilizowekwa kisheria. Limeanzishwa dawati la malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupokea malalamiko au maswali kuhusu zoezi hili.

8.Nyumba na majengo ya miaka mingi, yaliyokuwepo miaka mingi kabla ya kutungwa kwa Sheria zinazotekelezwa kwa zoezi hili, hayatabomolewa isipokuwa tu pale maisha ya wakazi yapo hatarini. Wanaoishi katika makazi hayo watapewa miongozo ya hatua za kuhifadhi mazingira na kujiokoa na maafa;

9.Serikali haina dhamira ya kubomoa mahoteli makubwa ya siku nyingi yaliyo karibu na fukwe katika maeneo ya Masaki. Wamiliki wa mahoteli haya watapewa masharti na miongozo ya kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria.

10.Serikali inaweka uratibu wa karibu zaidi miongoni mwa taasisi zake ili hatua za utekelezaji wa sheria za nchi zisiwe chanzo cha taharuki katika jamii.

11.Serikali haina dhamira ya kuwatesa wananchi wake kwa kuwalazimisha kuhama katika makazi yao bila sababu za msingi. Lakini pia Serikali haiwezi kuruhusu wananchi waendelee kukaa katika maeneo ambayo ikinyesha mvua kubwa maisha yao yapo hatarini.
 Itakumbukwa kwamba katika mafuriko ya mwaka 2011, wananchi 49 waishio mabondeni walipoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Hali ya Hewa, mwaka huu zinatarajiwa kunyesha mvua kubwa kuliko zilizowahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

12.  Serikali inafuatilia kwa karibu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya taarifa za wananchi wanaohitaji msaada maalum wa kibinadamu.

Suala la Mchungaji Getrude Rwakatare
Mkutano ulipokea taarifa kuhusu suala linaloongelewa sana la nyumba ya Mchungaji Rwakatare.  Ilielezwa kwamba Mchungaji Rwakatare amejenga nyumba yake pahali ambapo amezuia mtiririko wa mto kwa kujaza kifusi ili kupata eneo zaidi katika eneo la miti ya mikoko, kinyume kabisa na Sheria tatu muhimu.  
Pia ilielezwa kwamba tangu wakati ujenzi unaanza jitihada za kumsimamisha zilifanyika na mamlaka za Serikali za Mitaa lakini ikashindikana kutokana na sababu mbalimbali. Pale Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira lilipoingilia kati na kutaka kuibomoa nyumba hiyo, Baraza lilishtakiwa mahakamani. 
Wakati kesi inataka kuanza kusikilizwa, mwanasheria mdogo wa Baraza, yeye mwenyewe bila kuagizwa wala kuwaarifu wakubwa zake, mnamo tarehe 11 Mei 2015, aliingia makubaliano na mawakili wa Mchungaji Rwakatare kwa niaba ya Baraza ya kuondoa kesi hiyo mahakamani na kukubali, kwa niaba ya Baraza, kutombughudhi kabisa Mchungaji Rwakatare.  
Makubaliano hayo yalisajiliwa na Mahakama kama hukumu tarehe 13 Mei 2015. Mwanasheria huyo alificha makubaliano hayo kwa miezi mitano hadi Oktoba 2015, yalipogundulika na mtumishi mwingine wa Baraza. Mkutano ulielezwa kwamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kufuata taratibu zote, alishaagiza kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mwanasheria huyo. 
Mwanasheria huyo alifukuzwa kazi siku ya juzi tarehe 6 Januari 2016 na taarifa zake zimekwishafikishwa TAKUKURU. 
Vilevile, Ofisi ya Makamu wa Rais, iliiagiza Baraza kufungua shauri mahakamani la kuomba “makubaliano” kati yake na Mchungaji Rwakatare yawekwe pembeni kwasababu yalipatikana na njia ya udanganyifu. Shauri hilo lilifunguliwa tarehe 29 Disemba 2015.

Kuhusu Karakana ya Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Kasi (DART)
Mkutano pia ulijulishwa kuhusu hoja inayozungumzwa kwamba wananchi wanaondolewa katika maeneo ya kuishi mabondeni lakini mradi wa DART umeachwa.
 Mkutano ulielezwa kwamba Sheria ya Mazingira (kifungu 57 (2)) inatoa nafasi ya kutolewa ruhusa kwa miradi/shughuli zenye maslahi ya taifa kufanyika katika maeneo ya mabondeni, na kwamba Waziri mwenye dhamana ya mazingira anaruhusiwa kutoa miongozo ya namna ya shughuli hizo zinavyoweza kufanyika bila kuathiri mazingira.
 Mradi wa DART ulipata kibali hicho na una mkataba na Baraza la Mazingira kuhusu hatua za hifadhi ya mazingira zinazopaswa kutekelezwa katika mradi huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
08.01.2016

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR