Saturday, September 15, 2012

CHANGAMOTO ZA VIWAWA


CHANGAMOTO KUBWA KWA VIWAWA.

1. Utume Wetu
Changamoto tuliyonayo ni kuona namna gani tunaweza kuendeleza au
kuanzisha utume wa Viwawa katika ngazi ya Kigango, Parokia na Jimbo
hasa kwa vijana ambao ni walengwa wakuu, hivyo kufanya vijana wengi
kujiunga na kujua utume halisi wa Viwawa.
Utume halisi wa Viwawa ni Tafakari ya Maisha kwa kutumia njia ya
Kuona, Kuamua, Kutenda na Kutafakari, hufanyika katika vikundi vya
watu wasiozidi watano kwa kila wiki mara moja.
Kuna njia tatu za kufanya Tafakari ya Maisha (i)Tafakari ya wazi
(ii) Tafakari ya Injili (iii) Tafakari ya mada.
Lazima tutambue Tafakari ya Maisha ni Utume halisi wa Viwawa Duniani
kote.Mwanzilishi wa Viwawa Joseph kardinali Cardijn alisema pasipo
Tafakari ya Maisha hakuna Viwawa hai
Kwa kutotumia njia ya Tafakari ya Maisha kama alivyosema mwanzilishi
tunapoteza ladha ya kukubalika na Vijana na kuonekana kama chama
kisicho na malengo au kukosa mwelekeo.
Wengine wanadiliki kutuita waimba kwaya,wacheza ngoma,wababishaji.
sisi atutambuliki kwa shughuri zetu tu tunazofanya bali kwa mang’amuzi
ya utume wetu.Vijana wengi wana matatizo ya Kiroho na Kimaisha
lengo la Tafakari ya Maisha ni kutatua matatizo ya vijana kupitia njia
ya Kuona,Kuamua,Kutenda na Kutafakari.Tafakari ya Maisha hutoa
ufumbuzi wa kina, endelevu na uponyaji wa ndani.



No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR