Wednesday, October 10, 2012

.Bikira Maria anapewa heshima zaidi

Bikira Maria kati ya Waorthodoksi

Kwa kiasi kikubwa imani ya Waorthodoksi kuhusu Maria inalingana na ile ya Wakatoliki, ingawa hawakubali jinsi baadhi ya dogma hizo zilivyotangazwa na jinsi zinavyofafanuliwa.

Bikira Maria katika Uprotestanti

Martin Luther alipoanza Matengenezo ya Kiprotestanti aliandika kwa heshima juu ya Bikira Maria, lakini kadiri mabishano yalivyozidi kati ya madhehebu ya Kikristo, Waprotestanti walizidi kupinga mafundisho ya Kanisa Katoliki juu ya Mama wa Yesu. Siku hizi baadhi yake, hasa Waanglikana na Wamethodisti wanamrudishia Maria nafasi yake kama kielelezo cha imani na cha kupokea neema ya Mungu.

Bikira Mariamu katika Uislamu

Kurani inamtaja mwanamke mmoja tu, tena mara 34: ni Mariamu, mama wa nabii Isa. Akichanganywa na dada wa Haruni na Musa, aliyekuwa na jina hilohilo, anatajwa kama binti Imrani. Pia habari nyingine kadhaa zinapishana na zile za Injili.

Hata hivyo anapewa heshima ya pekee, kama inavyoonekana katika sura ya 3:43: “Na kumbukeni malaika waliposema, ‘Ewe Mariamu, kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa walimwengu”. Tena katika aya 3:46: “Na kumbukeni waliposema malaika: ‘Ewe Mariamu, bila shaka Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za Neno litokalo kwake, jina lake Masihi Isa mwana wa Mariamu, mwenye heshima katika dunia na ahera, na yu miongoni mwa waliokaribishwa’”.

Aliambiwa amefanywa “ishara” pamoja na mwanae, ingawa haisemwi ni ishara ya nini. Sura ya 19, yenye jina lake, inaeleza kwamba Malaika Jibrili (Gabrieli) akimpasha habari ya mimba alisema, ‘Hakika mimi ni mjumbe wa Mola wako ili nikupe mwana mtakatifu’. 

Akasema, ‘Ninawezaje kupata mtoto hali hajanigusa mwanamume yeyote, wala mimi si mwasherati?’ Akasema, ‘Ni kama hivyo; Mola wako amesema: Haya ni rahisi kwangu, na ili tukufanya ishara kwa mwanadamu na rehema itokayo kwetu, na ni jambo lililokwisha hukumiwa’ ” (19:19-21). “Na mwanamke yule aliyejilinda tupu yake na tukampulizia roho yetu na tukamfanya yeye na mwanawe ishara kwa walimwengu” (21:91).

Pamoja na kusifiwa kwa usafi wake, anaongezewa sifa za imani na unyenyekevu: “Na Mariamu binti Imrani aliyejilinda uchi wake, na tukampulizia humo Roho yetu na kayasadikisha maneno ya Mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu” (66:12).

2 comments:

  1. huu ni mwezi wa rozali tusisahau kwenda kusali

    ReplyDelete
  2. SAFI SANA MDOGO WANGU KATIKA KRISTO. WAHELIMISHE VIJANA KATIKA KUMJUA B. MARIA, KWANI PASIPO MARIA HAKUNA KANISA KATOLIKI. TUSALI ROZARI. MIMI NIMEFIKA SALAMA, TUOMBEANE. NITAJITAHIDI KUMTAFUTA PD. MAJETHA NIKIWA FREE. KAMA KUNA E-MAIL YAKE NITUMIE. SIKU NJEMA KATUBU WETU, UTUME MWEMA KATIKA VIJANA. FRT. PAUL

    ReplyDelete

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR