Padre Massawe, alikufa kwa kuzama baharini Oktoba 25 katika ufukwe wa Bagamoyo mkoani Pwani.
Padre massawe na mapadre wenzake washirika la consolata kutoka mataifa mbali mbali barani afrika walikwenda Bagamoyo kupumzika baada ya mkutano wa wakuu wa
Shirika la Waconsolata Barani Afrika, uliokuwa unafanyika consolata mission centre bunju, Jiji la Dar es Salaam.
Septemba 7, 2011 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Waconsolata
nchini Tanzania hadi alipokufa Oktoba 25, 2012.
Kabla ya kuwa mkuu wa shirika hilo, Padre Massawe alifanya kazi za umissionari katika nchi za Ethiopia na Italy.
HISTORIA YA MAREHEMU
Marehemu Padre Salutaris Massawe alizaliwa tarehe 8 Julai 1962, katika kijiji cha kibosho wilaya ya moshi vijijini.
Alisoma shule ya Msingi
Singachini kuanzia mwaka 1971 hadi mwaka 1978
mwaka 1979-1985 alikuwa akisoma katika Sekondari Maua Seminari iliyoko mkoani kilimanjaro.
Aliendelea na masomo ya Falsafa na Taalimungu kwenye Chuo cha
Waconsolata kilichoko mjini Nairobi kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1988.
Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, kunako tarehe 27 Juni 1993 alipewa daraja takatifu la Upadre katika kanisa la Kristo Mfalme na Askofu Amedeus Msarikie wa Jimbo la Moshi wakati huo.
Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, kunako tarehe 27 Juni 1993 alipewa daraja takatifu la Upadre katika kanisa la Kristo Mfalme na Askofu Amedeus Msarikie wa Jimbo la Moshi wakati huo.
Mungu alimpa maisha ya duniani na sasa amemwita, ili ampe maisha ya mbiguni yasiyo na mwisho....
Raha ya milele umpe, ee bwana...
na mwanga wa milele umwangazie
apumzike kwa amani
amina,
ASANTE KATIBU, NIPO NAFUATILIA MISA KUPITIA RADIO MARIA. INASIKITISHA, LAKINI HATUNA BUDI KUMUOMBEA DAIMA MPENDWA WETU. MUNGU AMWEKE MAHALI PEMA PEPONI. FRT. PAUL
ReplyDeleteAmina... FRT kwa mpande wetu sisi vijana tumepoteza padre amabaye alitupenda sana hakuna asiyejua kuwa CMC ilikuwa ni center yenye kutoa malezi ya vijana semina nyingi sana walituandalia TUTAMKUMBUKA MILELE
ReplyDeletemungu amempenda zaidi ni masikitiko makubwa kwa vijana wote wa CMC haswa Mabolozi....Mungu aiweke mahala pema peponi.
ReplyDeletehonest me until now siamin kama PD.Massawe hatunae poleni sana wana CMC Mungu akipenda nitaenda siku moja Iringa Hata niione 2 nyumba yake ya milele
ReplyDeletekristu alisema:"mimi ndimi ufufuo na uzima" twakuomba umuweke PD: wetu mpedwa massawe miongoni mwa watakatifu wako
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi. Amen, alikuwa nguzo ya shirika huyu jamaa....basi tena ndo MUNGU Ametaka.........Frank Mwombeki:
ReplyDeleteMungu Ampuzishe kwa amani.
ReplyDeleteamina.......
ReplyDeleteNAMWOMBEA KWA MUNGU APATE MAKAO YALE MUNGU ALIYOYAANDAA KWA WALE WATEULE WAKE kwani waitwao ni wengi lakini wateule ni wachache, naomba padre huyu awe kati ya wateule.
ReplyDelete