Mkuu wa Shirika la Consolata Tanzania amezikwa jana huko Tosamaganga Iringa
Picha
inayoonekana ni marehemu Padre Salutaris Lello Masawe aliyekuwa Mkuu wa
Shirila la Wamisionari wa Consolata Tanzania ambaye amezikwa leo katika
makaburi ya Jimbo la Iringa yaliyopo Tosamaganga. |
Add caption |
Wakristo Wakatoliki wameshauriwa
kujiuliza kuwa wanahusiana na wengine vipi kama
ishara ya kujiandaa kuufikia uzima wa milele mbinguni.
Hayo yamezungumzwa leo na Askofu
wa Jimbo Katoliki la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa alipokuwa
akihubiri wakati wa Misa ya Mazishi ya Padre Salutaris Lello Massawe
ilifofanyika katika Kanisa la Moyo Mt. wa Yesu Parokia ya Tosamaganga jimboni
humu.
Amesema binadamu hataulizwa
endapo alitenda matendo ya upendo bali ataulizwa kama
alikuwa na roho ya ubinadamu na haki katika kuwajali wengine.
“Swali la kujiuliza kila wakati
katika maisha ni kwamba, umehusiana na watu wangapi wakakubariki? Na tena
hatutaulizwa endapo tulitenda upendo bali tutaulizwa kama
tulikuwa na roho ya ubinadamu na haki katika kuwajali wengine” amesema
Amesema Mungu ana mzaha katika
kuvichukua viumbe wake kwani huchukua muda anaoutaka ambao binadamu haujui
lakini jambo la msingi ni kujiandaa kiroho ili kuwa tayari wakati wowote.
“Munu ana mzaha pia. Mzaha
wenyewe ni kiama huu ambao kila mtu anajiuliza kwa nini Massawe ameondoka
wakati ambao hakutarajiwa? Kila mtu anajiuliza, kwa nini mapema? Kwa nini
ghafla? Huo ndiyo mzaha wenyewe ila yeye anajua kila mtu atamchukuaje na kwa
wakati gani” amesema.
Akimzungumzia Massawe Mhashamu
askofu Ngalalekumtwa amesema alikuwa ni mtu mwenye bidii, uaminifu katika
kuwajibika na alikuwa na maneno ya kutia moyo.
“Kazi za kitume alizitenda kwa
bidii na kwa uaminifu. Pia alikuwa na maneno ya kutia moyo. Aliadhimisha
matendo ya wokovu kwa nidhamu. Tunaimani kabisa kuwa huko alikokwenda ni
kuzuri” amesema.
Amewataka Wakristo kuwa ni watu
wa kutenda haki na kujituma katika kuwasaidia wanaohitaji msaada kwa kutenda
matendo ya upendo wakijua kuwa maisha ya mwanadamu ni safari ya kumtafuta
Mungu.
“Tendeni matendo ya haki, matendo
ya upendo kwa kuwasaidia wahitaji kwa kujua kuwa safari ya mwanadamu ni
kumtafuta Mungu; binadamu kajaliwa moyo mkubwa wa kuweza kumwelekea Mungu”
amesema.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya kidini kutoka ndani na nje ya
nchi ambapo jumla maaskofu wanne walihudhuria mazishi hayo.
Maaskofu hao ni pamoja na
Mhashamu Desderius Rwoma wa Jimbo Katoliki la Singida, Mhashamu Alfred Maluma
wa Njombe, Mhashamu Evaristo Chengula wa Mbeya pamoja na Mhashamu Tarcisius
Ngalalekumtwa wa Iringa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania..
Mungu ailaze roho ya marehemu Pd. Massawe mahali pema Mbinguni. Amina
ReplyDeleteRIP PD Massawe
ReplyDelete