Wednesday, November 7, 2012
Bwana, Anatufundisha ,Nasisi Tusali.......
Zipo Silaha mbalimbali za Kiroho alizovaa Yohane Mbatizaji nazo ni Sala,.. kufunga na sadaka. Kwa leo tutafakari silaha ya kwanza: Ambayo ni
................SALA.....
Tumeitwa na Kirsto. Tumeitika wito wake. Hivyo, tunafanya kazi yake. Yeye alikuwa mtu wa sala. Aliwafundisha watu namna ya kusali kwa mafundisho yake na tendo halisi la kusali. Sisi kama wafuasi wake na tulioitika mwito wake wa kuwa viongozi wa taifa lake, tuige mfano wake. Katika tafakari hiyo, tusaidiwe na Yesu wa Mwinjili Luka.... Mwinjil Luka, anatilia mkazo mkubwa katika umuhimu wa sala. Kwa yakini, umuhimu huo unaonekana bayana. Kwanza jinsi Yesu aliivyosali mara nyingi. Pili, alivyowahimiza watu wasali. Tatu, jinsi alivyota mifano bora ya kusali.
Injili ya Luka inaonesha dhahiri kuwa kabla ya kuchukua hatua kubwa na muhimu, yesu anaanza kwa sala. Tuzitazame fasuli zifuatazo:
l1. Ubatizo wa Yesu (Lk 3:21-22)
Katika nafasi ya kubatizwa kwa Yesu, Luka anasema kuwa watu wote walipokuwa wamebatizwa, naye Yesu alibatizwa. Na alipokuwa anasali, mbingu zilifunguka, na Roho Mtakatifu alimshukia akiwa katika umbo la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni: "Wewe ndiwe Mwanangu, nimependezwa nawe".
Hatua hiyo ya kubatizwa ilikuwa ya maana sana. yesu alithibitishwa kuwa Mwana tena mpenzi wa Mungu. Alijiunga na foleni ya wadhambi ili apokee ubatizo wa toba, toba iletaya ondoleo la dhambi. Lakini yeye hakuwa na dhambi. Alihakikishiwa kuwa njia aliyochukua yaani utume wake ilikuwa sahihi, na kwa kweli yalikuwa mapenzi ya Mungu.
l2. Yesu anawateua mitume kumi na wawili (Lk 6:12-16).
Tendo lilitanguliwa na sala. Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku kucha akisali. Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, miongoni mwao akawachagua kumi na wawili ambao aliwaita mitume. Alijitenga na watu ili awe karibu na Mungu baba yake. Kwa hiyo, uteuzi wa mitume uliongozwa na Baba. Hatua hiyo ilibeba umuhimu mkubwa sana - kuwateua viongozi wanaofaa. tunasoma pia uteuzi wa mitume ukitanguliwa na sala katika Mdo 13:1-3. Katika kanisa la Antiokia kulikuwepo na watu wengine waliokuwa manabii na walimu. Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema: :Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia." Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawekea mikono, wakawaacha waende zao.
l3. Petro anamkiri Yesu Kristo (Lk 9:!8-20) Yesu alikuwa akisali peke yake na wanafunzi wake walikuwa karibu kabla hajaanza kuwauliza: :Eti, watu wanasema mimi ni nani?" Baada ya kutoa majibu mbali mbali, Yesu anawauliza wanafunzi wenyewe: "Ninyi je, mwasema mimi ni nani?" Petro kwa niaba ya wanafunzi wenzake alitoa jibu sahihi: "Wewe ndiwe kristo wa Mungu." Hiyo ilikuwa hatua kubwa, yaani azma ya Yesu kujua kama watu na wanafunzi wake wanamfahamu: Yeye ni nani na utume wake ni upi. Kumfahamu ni sharti muhimu ili utume wake uzae matunda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
No comments:
Post a Comment