Thursday, March 7, 2013

MAISHA YA MH.ISIDORI BAKANJA

KAMA VIJANA YATUPASA TUJIFUNZE KUTOKA KWA MH. ISIDORI BAKANJA



Mwenyeheri Isidori Bakanja, msimamizi wa Parokia yetu ya Boko, aliyeuwawa kikatili kati ya tarehe 8 na 15 Agosti, 1909, akiwa amevalia shingoni mwake, Skapulari ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli. Alifariki dunia akiwa katika mateso makali, lakini kwa ajili ya imani yake kwa Kristo na Kanisa lake aliyapokea hayo yote kwa imani na matumaini katika maisha ya uzima wa milele.

Mapadre waliokuwa wanampatia Mpako wa Wagonjwa walimwomba, kusamehe na kusahau, bali kwa imani na matumaini aendelee kuubeba vyema Msalaba wake kwa kumfuasa Kristo hata katika njia ya mateso na madhulumu.

Huyu ndiye Mwenyeheri Isidori Bakanja msimamizi wa Parokia yetu ya Boko, ambaye tunamwomba kwa sala na maombezi yake, asaidie juhudi zetu zauinjilishaji na harakati za maendeleo endelevu, Yeye ambaye kwa miaka kumi na nane ya ujana wake na miaka mitatu tu, tangu alipoikumbatia Habari Njema ya Wokovu na kupata tuzo la maisha ya milele mbinguni awe kweli ni mwombezi wa Vijana na Waamini wote wa Parokia yetu.

Changamoto wanayokabiliana nayo wakristo ni kuhakikisha kwamba, hata katika madhulumu na magumu ya maisha, wanajitahidi kujenga misingi ya haki, amani na upatanisho. Mapambano haya yanakwenda sanjari na vita dhidi ya dhuluma, nyanyaso, uonevu, rushwa, wizi na ufisadi; ili kukoleza moyo wa majitoleo kwa ajili ya mafao ya wengi ndani ya jamii. Ni mwaliko wa kujenga na kuendeleza misingi ya uadilifu na maadili mema ndani ya jamii kwa kukazia pia elimu ya uraia pamoja na matumizi ya rasilimali ya nchi kwa ajili ya mafao ya wengi.



No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR