JUMAPILI DOMINIKA YA 31 ya Mwaka C.
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA MH. ISIDORI BAKANJA- BOKO.
MISA YA KWANZA 12:15-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. FRANCIS WA ASIZ-MBWENI
MISA YA KWANZA SAA 1:10-3:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 3:00-4:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
IBADA NI MOJA TU ITAANZA SAA 3:00-5:00 ASUBUHI.
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA-MBWENI TETA
MISA NI SAA 3:00-5:00.
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA-MBWENI TETA
MISA NI SAA 3:00-5:00.
DOMINIKA 31 ya mwaka C (masomo)
SOMO
1. HEK. 11:22- 12:2
Ulimwengu wote mbele zako Bwana, ni kama
chembe moja katika mizani, na mfano wa tone moja la umande lishukalo asubuhi
juu ya ardhi. Lakini wewe unawahurumia watu wote, kwa sababu unao uweza wa
kutenda mambo yote; nawe wawaachilia wanadamu dhambi zao, ili wapate kutubu.
Kwa maana wewe wavipenda vitu vyote vilivyopo, wala huchukii kitu cho chote
ulichokiumba. Kwa kuwa hungalifanya kamwe kitu cho chote kama ungalichukia;
tena kitu cho chote kingaliwezaje kudumu, ila kwa mapenzi yako? Au kitu
kisichoumbwa nawe kingaliwezaje kuhifadhika? Lakini wewe unaviachilia vyote,
kwa kuwa ni vyako, Ee Mfalme mkuu, mpenda roho za watu; maana roho yako
isiyoharibika imo katika vyote. Kwa hiyo wawathibitishia kidogo kodogo hatia
yako, wale wanaokengeuka kutoka katikala
njia njema; wawaonya, ukiwakumbusha kwa mambo yale yale wanayokosa, ili
waokoke katika ubaya wao, na kukuamini wewe Bwana.
SOMO
2. 2THE. 1:11- 2:2
Kwa hiyo twawaombea ninyi sikuzote, ili
Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya
wema na kila kazi ya imani kwa nguvu; jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani
yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo. Basi,
ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na
kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba usifadhaishwe upesi hata kuicha nia yenu,
wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni
wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.
INJILI.
LK. 19:1-10
Yesu alipoingia Yeriko alipita katikati
yake. Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza
ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna
gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia
mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kupita njia ile. Na
Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi,
kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani kwako. Akafanya haraka, akashuka,
akamkaribisha kwa furaha. Hata watu walipoona, walinung’unika wote, wakisema,
ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana nusu ya mali
yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang’anya mtu kitu kwa hila namrudishia
mara nne. Yesu akamwambia, leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu
naye ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuoka
kile kilichopotea.
- Jumapili ya tarehe 03/11/13 tutakuwa na kikao cha halmashauri ya VIWAWA Parokia, kikao kitaanza mara baada ya misa ya pili...mahali na parokiani boko fika bila kukosa.
- Kigango cha mt. Raphael jumapili tarehe 3/11/2013 ni siku ya mnada wa mavuno waamini wote, ndugu jamaa na marafiki unaalikwa kuungano nao.
- jiandae na semina ya vijana wote wa parokia ya boko pamoja na parokia jirani tarehe 23/11/2013 taarifa kamili utazipata jumapili.
- tunawakumbusha vijana wote kuendelea kulipa ada kwa maendeleo ya chama chetu..... mapendo sana malipo kwa njia ya benk kwa jina na number hii :viwawa parokia ya boko account no 01524526820100 crdb bank tegeta branch
No comments:
Post a Comment