WARENO 1500 – 1800
Ukiristo uliletwa kwa mara ya mwanzo Zanzibar na Wareno.
Wareno wakielekea juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya
matumaini mema – Cape of Good Hope katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu
la kudai bandari, njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2000 za mwambao
wa Afrika.
Mara tu ya kuwasili Zanzibar Wareno katika mwaka 1499
walianzisha Ujumbe wa Kanisa la Kikatoliki na kituo cha biashara ndani ya mji wa
Zanzibar. Wareno kwa miaka 200 iliyofuata walihodhi njia za baharini za meli za
Afrika Mashariki na walijitahidi kuanzisha msururu wa makaazi katika eneo la
mwambao. Mabaki ya makaazi ya Wareno bado yanaweza kuonekana karibu na
Fukuchani Kaskazini Unguja na Kisiwani Pemba. Ngome Kongwe ambayo ipo karibu na
bandari ya mji wa Zanzibar ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa dogo la
kikatoliki la mwanzo baada ya kutekwa na Jeshi la Oman. Jeshi hili la Oman
inasemekana liliitwa na wenyeji wa Zanzibar na Pemba ili kuwasaidia kuwangóa
Wareno waliokuwa makatili na madhalimu.
Baada ya miongo ya vita na maangamizo ambayo yaliyoshuhudi
kuwaka moto mji wa Mombasa, Wareno walirudi nyuma, na kurejea kuendea kusini,
mbali na mafikio ya mashambulizi ya moja kwa moja ambayo yaliyotokana na pepo za
miongo za jahazi (waarabu).
OASISI YA UVUMILIVU (OASIS OF TOLERANCE)
Katika mwaka 1841 mpiganaji wa Kioman/Oman Sultan, Seyyid
Said alivutiwa sana na visiwa hivyi vya Zanzibar kwa hiyo alihakikisha
anahamishia makao makuu yake Zanzibar kama ni mji mkuu. Malezi yake katika
maisha ya Jangwani yalimshajiisha yeye kwa nguvu zake zote kuviendeleza visiwa
hivyi vyenye ustawi. Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar kama kama ni Oasisi
katika bahari. Alisimamia mipango mikubwa ya upandaji miti, alichimba visima
vya maji vyingi tu na kujenga nyumba nyingi ambazo zilitosha mamia ya wageni.
Sultan alitambua wageni watakaa na kujiliwaza katika Oasisi. Na alijua kwamba
biashara itakuwa na kufanyika katika eneo hili ikiwa litaimarishwa kwa vitu na
mambo mengine pamoja na usalama. Vile vile alitarajia na kutambua kwamba
angelipata asilimia fulani inayotokana na shughuli za kibiashara zitakazo
endeshwa Visiwani kama ni malipo ya kuviimarisha visiwa hivyi. Aliwakaribisha
na kuwaomba wafanyabiashara kutoka India kufungua matawi ya ofisi zao ndani ya
Zanzibar ili kuimarisha biashara. Wafanyabishara hawa wengi kutoka India
walikuwa ni raia wa kiingereza hii ilikuwa ni kwa sababu ya kutekwa India na
Uingereza. Kwa maana hiyo, alianza kuwakaribisha maofisa wa kiingereza visiwani
ili kuwakilisha maslahi ya raia hawa wahindi wa kiingereza. Mara tu tena baadae
alianza kuingia katika mikataba rasmi ya kibiashara na Serikali ya kiingereza na
Serikali nyengine za Magharibi.
Majengo ya biashara yalijengwa ndani ya Mji Mkongwe na
Kampuni za Kimarekani, Kijerumani, Ufaransa na na Kiingereza. Bandari ya
Zanzibar ilitoa huduma za fueli na kufanyia
matengenezo
Meli za kivita na vyombo vya usafiri vya wafanyabiashara. Meli hizi zilileta
mapote ya ziada ya watu wa magharibi ndani ya Zanzibar. Kama ni makaribisho
mema ya wageni wengi katika Oasisi yake. Sultani aliruhusu watu wa imani zote
kuendesha shughuli zao za kidini walivyopenda.
Akiwa
Muislamu mwenye imani kamili, Sultani alionyesha mfano bora wa uvumilivu juu ya
mahitajio ya kidini ya watu wengine. Wakati huo huo akijenga furaha na imani
katika dini ya mababu zake, kwa bidii zote. Warithi wake alifuata utaratibu wa
Sultani Seyyid, wakiruhusu kuanzishwa mahekalu mengi tu ya kihindi, makanisa
mawili, moja la kikatoliki na kiprostanti, sehemu za kimazishi za zoroastriani
na misikiti kwa kila dhehebu kuu au dogo la kiislamu ndani ya mji mmoja.
1800 – 1900
WAKATOLIKI, MAKUNDI YA WAKIRISTO WASIOPENDA MIKUTANO ASMI, VITA AU GHASIA (QUAKERS) NA UJUMBE WA VYUO VIKUU KWA AFRIKA YA KATI ( UMCA)
Baada ya Wareno kurudi nyuma Wakiristo kidogo tu Wakigoa
ndio waliobakia Zanzibar.
Wakiristo
hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada lakini waliweza kuifanya hai jumuia
yao kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi. Baadae katika miaka 1800 makundi ya
watu wa wamagharibi yalianza kujumuisha wamisionari na wachungaji wamisionari
waliokuwa wakipita pita mara chache na wachungaji katika meli bandarini. Katika
mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo zaidi wa kudumu waliwasili Afrika mashariki
kwa kupitia mchungaji wa kilutheri Joseph Krapf na wafuasi wawili ambao
walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya kimisheni ya kanisa la kiingereza (English
Church Missionary Society). Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na
miaka michache mbeleni walitoa kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi
kuanzisha kanisa ndani ya visiwa hivyi.
Ukuwaji
wa harakati dhidi ya utumwa ndani ya Uingereza ulishajiisha raghba ya
wamisionari wakiristo, ikikuzwa na hotuba ya David Livingstone aliyoitoa mwaka
1857 akiomba Uingereza kupeleka wamisionari na wafanyakazi Afrika. David
Livingstone alilingania kwamba mwisho wa utumwa utakuwepo tu kupitia “ biashara
na ukiristo”. Baadae Livingstone alitumia siku nyingi tu Zanzibar ambao
alipatiwa nafasi ya kutumia nyumba ya Sultani.
Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu
kwa Afrika ya Kati (UMCA). Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati ulikuwa ni
mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo vikuu vya Oxford and
Cambridge, ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham
na Dublin. Katika mwaka 1860 walimchagua Charles Mackenzie kama ni “Askofu wa
Afrika ya kati” na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea
huko Afrika ya Kati.
Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA)
lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya
Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi. Kwa
ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa
nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi na baadae hadi mto shire kuasisi
ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya Kati katika Afrika katika
sehemu iliyojulikana kama Magomero.
Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana na jina na ari
ya jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia kushindwa kwa aina yake kutekeleza
malengo yake. Maradhi na njaa na ukame uliwakumba wamisionari wa mwanzo na
kupelekea kufa kwa askofu. Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo
ndani ya kipindi
cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo lilikuwepo mbali sana
na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya mawasiliano, eneo hilo halikuwa
na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao hawana uzoefu na mazoea na hali ya
hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu wa kisiasa. Askofu mpya, George
Tozer, kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya mtiririko wa mto
kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu liligundulika kuwa
halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo lilihamwa kwa miezi hivi tu.
Wakichukua bidii za makusudi, ili kutorejea makosa
yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA)
waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza kufika
kati kati ya Afrika. Maeneo mbali mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha
Johanna, maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini kwa bahati Zanzibar
ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za mawasiliano,
upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji nguvu kazi bora.
Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar
tarehe 31/08/1864.
Ujumbe
huu ulipowasili ulipokewa na wamisionari wakatoliki wa Kifaransa. Wamisionari
wa kikatoliki waliwasili mwanzo Zanzibar kwa kiasi ya miaka minne kabla ya
wamisionari wa kiingereza. Katika mwezi Septemba mwaka 1860 Abbe Favat ambaye
alikuwa Mfaransa mdini maarufu mwenye nguvu alitiliana mkataba na Seyyid Said
kumruhusu yeye Abbe Favat kuhamishia Makao Makuu yake katika Kisiwa cha Reunion
na kuwa Zanzibar kufikia mwezi Disemba kikundi chake cha “mapadri wawili wasio
watawa na watawa sita wa kike” (“Filler de Marie”) walikuwa wakiishi katika
makaazi ya watawa ambayo pia yalikuwa na kanisa dogo hapo Shangani. Jengo hili
la watawa linasemekana na lilijengwa katika mwaka 1860, lakini ujenzi huu
inawezekana ulikuwa ni matengenezo makubwa ya nyumba iliyokuwepo kabla. Kanisa
dogo katika jengo hili lilikuwa ni kanisa la kwanza lililojengwa Zanzibar kwa
miaka 200.
Click here: Kuendelea ..........
Click here: Kuendelea ..........
No comments:
Post a Comment