Heri
wenye rehema maana hao watapata rehema, ndiyo kauli mbiu itakayoongoza
maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itakayofanyika
Jimbo kuu la Cracovia, Poland. Kamati kuu ya maandalizi imechapisha
nembo itakayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani
ambayo Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuhudhuria na kushiriki
kikamilifu.
Nembo ina rangi kuu tatu: Bluu, Nyekundu na Njano;
inaonesha ramani ya Poland na ndani yake kuna Msalaba inayomwonesha Yesu
Kristo, kiini cha mkutano huu. Nembo hii inawaalika vijana kujiaminisha
mikononi mwa Mungu, utekelezaji wa maneno ya Mtakatifu Faustina
Kowalska aliyeeneza Ibada ya Huruma ya Mungu.
Siku ya Vijana
Duniani kwa Mwaka 2016 itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 26 hadi
Julai 2014. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuwasili nchini Poland
hapo tarehe 28 Julai 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
No comments:
Post a Comment