05
October
JUMAPILI YA 27 YA MWAKA "A" 2014.RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
Kutakuwa na ibada ya Kipaimara itakuwa saa 5:00 asubuhi na itaongozwa na Askofu Mdoe.
Kutakuwa na ibada ya Kipaimara itakuwa saa 5:00 asubuhi na itaongozwa na Askofu Mdoe.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI.
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI.
KIGANGO CHA MBWENI.
Kutakuwa na Ibada moja saa: 1:15 – 2:55 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
Ibada itakuwa Moja tu: 1:00 – 2:55 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA itakuwa asubuhi;SOMO 1. Isa. 5:1-7
Somo katika kitabu cha Nabii Isaya.
Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi
wangu katika habari za shamba lake la mizabibu.
Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu,
Kilimani penye kuzaa sana;
Akafanya handaki kulizunguka pande zote,
Akatoa mawe yake,
Akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri,
Akajenga mnara katikati yake,
Akachimba shinikizo ndani yake;
Akatumaini ya kuwa utazaa mzabibu,
Nao ukaza zabibu-mwitu.
Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu. Je! ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu? Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa; nami nitaliharibu, wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake. kwa maana shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! alisikia kilio.
SOMO 2. Flp. 4:6-9
Somo katika waraka wa mtume Paulo kwa Wafilipi.Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zujulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote. yatafakarini hayo. Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
INJILI.Mt. 21:33-43
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.
Yesu aliwaambia wakuu wa makuhani na wazee wa watu, Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe, Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanae kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. wakamkamata wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi atakapokuja yule Bwana wa shamba la mizabibu. atawatendaje wale wakulima? wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,
Jiwe walilolikataa waashi,
Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu?
kwa sababu hiyo nawaambia, ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
Matangazo
No comments:
Post a Comment