Saturday, October 18, 2014

Kesho Dominika ya tarehe 19/10/2014, Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI anatarajiwa kushiriki katika Ibada ya Misa Takatifu mjini Vatican

Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI ni kati ya viongozi wakuu wa Kanisa wanaotarajiwa kuhudhuria katika ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumtangaza Mtumishi wa Mungu Papa Paulo VI, Jumapili, tarehe 19 Oktoba 2014 majira ya asubuhi kwa saa za Ulaya. Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu Benedikto XVI aliteuliwa na Papa Paulo VI kuwa Kardinali.

Hadi sasa kuna Makardinali wawili ambao bado wako hai, hawa ni wale walioteuliwa na Papa Paulo VI wakati alipokuwa analiongoza Kanisa. Hawa ni Kardinali Evaristo Arns na Kardinali wakefield Baum. Haya yamesemwa na Padre Federico Lombardi Msemaji mkuu wa Vatican, siku ya Ijumaa alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mjini Vatican.

Hili litakuwa ni tukio la pili la aina yake kwa Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kushiriki hadharani katika Ibada zinazoongozwa na Papa Francisko, tangu alipong'atuka kutoka madarakani.


 

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR