Saturday, November 1, 2014

Msomo ya Dominika ya Kumbukumbu ya Marehemu wote, Jumapili ya Tarehe 02/11/2014

02
 November
 Jumapili: Kuwakumbuka Marehemu wote.
SOMO  1. Hek. 3:1-9

Somo katika  Hekima. 
 Roho zao mwenye haki zimo mikononi mwa Mungu, wala maumivu hayatawagusa. Machoni pa watu walio wajinga walionekana kwamba wamekufa, na kufariki kwao kulidhaniwa kuwa ni hasara yaom na kusafiri kwao kutoka kwetu kuwa ni uharibifu wao; bali wao wenyewe wamo katika Imani....
somo 2. Rum. 6:3-9 

Somo katika kitabu cha Warumi. 
Hamfahamu ya kuwa sis sote tulibatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Bazi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya........


  INJILI.Mt. 25:31-46
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: hapo atakapokuja mwana wa Adamu katika utukufu wake, na Malaika Watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume na Mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wa wake wa kuume, njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme, mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu mkanunywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi ukanivika; nalikuwa mgojwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia, ndipo mwenye haki watakapomjibu, wakisema Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha au una kiu tukakunywesha,? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u Mgojwa, au kifungoni, tukakujia? Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amini nawaambia, Kadri mlivyomtendea mmoja wapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika Moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na Malaika zake; kwa maana, nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, usininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgojwa, na kifungoni, usije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana ni lini tulipokuona wewe una njaa  , au una kiu, au u mgeni au u uchi, au mgojwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu akisema, Amini, nawaambia, kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda  zao kuingia katika Adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele. 
Ratiba ya Ibada ya Jumapili ya tarehe 02/11/2014
Kigango cha Boko
Misa ya Kwanza- saa 12:15 Mpaka saa 1:45 Asubuhi.
Misa ya Pili        -  saa 2:00 Mpaka saa 3:50 Asubuhi.
Misa ya Tatu     -   saa 4:00 Mpaka saa 5:30 Asubuhi.

Kigango cha  Mt. Rafael Mbweni Malindi

Misa ya Kwanza   - saa 1:00 Mpaka saa 2:50 Asubuhi
Misa ya Pili            - saa 3:00 Mpaka saa 4:50 Asubuhi.

Kigango cha Mt. Fransisco wa Asizi - Mbweni
Misa ya Kwanza - saa 1:15 mpaka saa 2:50 Asubuhi.
Misa ya pili          - saa 3:00 mpaka saa 4:50 asubuhi

Kigango cha Mt. Anthony wa Padua - Mbweni Mpiji
Misa ni saa 3:00 mpaka saa 5:00 asubuhi

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR