Meneja wa kilabu ya Manchester
United Louis Van Gaal anaamini kwamba timu yake itatumia fursa ya
kushuka kwa soka ya kilabu ya Manchester City katika uwanja wa Etihad
kuishinda kilabu hiyo.
Kilabu ya Manchester City imepoteza mechi zake mbili za mwisho baada ya kushindwa na West Ham na Newcastle.''Kile tulichokiona katika mechi mbili za mwisho si matokeo ya kuridhisha,alisema Van Gaal.
''Tuna hisia njema kuhusu mechi hii''.''Tunahitaji matokeo mazuri na huenda yakawa dhidi ya Manchester City''.Aliongezea Van Gaal.
Tangu ipoteze kwa mabao 5-3 dhidi ya Leicester mnamo Septemba 21,Manchester United haijapoteza na huenda ikaikaribia Mancity katika nafasi ya nne iwapo itashinda mchuano huu wa 'Derby'.
Hatahivyo ushindi dhidi ya Manchester United utakuwa wa nne kati ya timu hizo mbili hatua ambayo haijaafikiwa kwa takriban miaka 44 na timu hiyo.
No comments:
Post a Comment