29
JUNI
JUMAPILI YA 14 YA MWAKA "A"
2014 (KIJANI)
2014 (KIJANI)
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI
SOMO 1:Zek.9:9-10
SOMO 1:Zek.9:9-10
Furahi
sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme
wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokuvu; ni mnyenyekevu,
amepanda Punda; naam, mwana-punda, mtoto wa Punda. Na gari la vita
nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na Farasi awe mbali na Yerusalemu, na
upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari
za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka mto
hata mwisho wa dunia.
SOMO 2:1Rum. 8:9, 11-13
Roho
wa Mungu anakaa ndani yetu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata
roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na roho wa Kristo, huyo si wake.
Lakini ikiwa roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani
yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu
iliyo katika hali ya kufa, kwa roho wake anayekaa ndani yenu. Basi, kama
ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya
mwili; kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa;
bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa roho, mtaishi.
INJILI: Mt.11:25-30
Wakati
ule Yesu alijibu, akasema, Nashukuru, Baba, Bwana wa mbingu na Nchi,
kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia
watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.
Akasema, nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuae mwana,
ila Baba; wala hakuna amjuae Baba, ila mwana, na ye yote ambaye mwana
apenda kumfunulia. Nyoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye
kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze
kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata
raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini; na mzigo wangu ni
mwepesi.
No comments:
Post a Comment