Thursday, January 22, 2015

18

 Januari
 Jumapili: Dominika ya 2 ya Mwaka "B".
SOMO  1. 1 Sam. 3:3b-10, 19

 Samueli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu; basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, mimi hapa. Akamwendea Eli kwa haraka, akasema mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, sikukuita, mwanangu; kalale tena. Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akamtambua ya kuwa Bwana ndiye alimwita yule mtoto. Kwa hiyo Eli akamwambia Samweli, enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena Bwana; Samweli akaenda akalala mahali pake. Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Samweli akakua, naye Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini.

Read More
somo 2. 1Kor. 6:13c-15a, 17-20. 

Somo katika Waraka wa kwanza wa mtume Paulo kwa Wakorintho

Mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana naye Bwana ni kwa mwili. Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni Roho moja naye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
.

  INJILI.Yn. 1:35-42
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Yohane.
Yohane alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, mwana kondoo wa Mungu! Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, mnatafuta nini? wakamwambia, Rabi (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? Akawaambia, Njooni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. Andrea, Nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohane na kumfuata Yesu. Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, tumemwona Masiha (maana yake, Kristo). Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, wewe u Simoni. mwana wa Yohane; nawe utaitwa kefa( tafsiri yake Petro au jiwe).

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR