Sunday, January 11, 2015

Masomo ya Tarehe 11/01/2015 mwaka B, wa Kanisa Dominika ya sikuku ya Ubatizo wa Bwana2015

11

 Januari
 Jumapili: ya Ubatizo wa Bwana.
SOMO  1. Isa. 42:1-4, 6-7

 Bwana asema: Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hautavunjika, wala utambi utokao moshi hautazima; atatokeza hukumu kwa kweli. Hatazimia , wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufugwa.

 Read More
somo 2. Mdo. 10:34-38. 

Siku ile; Petro aakafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo, bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli, akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote). Jambo lile ninyi mmelijua, lilionea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliohubiri Yohane; habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa roho Mtakatifu na nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.


  INJILI.Mk. 1:7-11
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Marko.

Siku ile: Yohane alihubiri akisema, yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu. Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohane katika Yordani. Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; na sauti ikatoka mbinguni, wewe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR