Jumatano ya Majivu ni
siku ya kwanza ya kwaresima.
Jumatano ya Majivu
Waamini hupakwa Majivu kichwani pamoja na kutamkiwa maneno ya kuhimizwa kufanya
toba “ulitoka mavumbini na mavumbini utarejea.
Kwa kawaida siku hii
ndiyo Kipindi cha kwaresima huanza rasmi . Waamini hufunga, mfungo unaofuata
kilelezo cha Yesu kufunga siku Arobaini jagwani baada ya kubatizwa na Yohane
Mbatizaji na kabla ya kuunza utume wake mwenyewe
UMUHIMU WA JUMATANO YA MAJIVU.
Ili kuelewa vizuri maana na umuhimu wa kipindi hiki, tutazame kwa
ufupi haya yafuatayo:
Sala ya mwanzo:
“Ee Bwana utujalie sisi waamini wako tuanze vita vya roho kwa
mfungo Mtakatifu. Nasi tulio tayari kupigana na pepo wabaya, tujipatie nguvu
kwasababu ya kufunga…”
Majivu’ tunayopakwa siku ya leo ni ishara ya kufanya toba, ni
ishara ya kumrudia Mungu! Tukitazama kwa ufupi baadhi ya vifungu katika Biblia
tunaona ukweli huu:
- Jer 6:26
- Daniel 9:3
- Yona 3:6
- 1Wamakabayo
3:46, ambapo Mathatia pamoja na wenzake walijipaka majivu kichwani kabla ya
kuanza vita dhidi ya ukoloni. Ilikiwa ishara ya kumrudia Mungu ili awe nguvu ao
katika mapambano waliokusudia kuyaanza dhidi ya ukoloni/ukandamizaji
waliokuwemo!
- Mt 10:13,
Kristu naye alijua utamaduni huu wa toba wa kujipaka majivu pale alipoionya
Korazin na Betsaida!
Mapokeo ya Kanisa Katoliki yameendeleza utamaduni huu wa toba:
- Mnamo Karne
ya 6 hadi ya 11 utamaduni huu ulifanyika, hata karne ya 12, papa Urbano wa Pili
aliidhinisha majivu yatumike yale yatokanayo na matawi ya mizeituni
yaliyotumika katika Jumapili ya Matawi.
Nabii Yoeli katika somo la kwanza (Yoe 2:12-18) anasistiza turarue
mioyo wala si mavazi yetu…yaani, tufanye mabadiliko ya ndani na siyo ya nje
tu!, kwa maneno mengine, mapinduzi ya kweli yaanze na yatoke mioyoni mwetu na
si maonyesho ya njenje tu!
Injili ya leo (Mt 6:1-6, 16-18) iametuasa juu ya suala hilohilo la
kufanya mfungo wenye msukumo wa kiroho unaotoka ndani ya moyo wa toba wa mtu na
si kufanyakama Mafarisayo walivyokuwa wakifanya. Wao walifunga na kusali
ili watazamwe na watu.
Tunapoanza kipindi cha Kwaresma kwa kupakwa majivu siku hii ya
leo, tukumbuke wajibu wetu; -kufunga
- Kusali
zaidi na
- kutenda
matendo mema (matendo ya huruma) kwa jirani zetu!
Basi, Tumwombe
Mungu ili zoezi la mfungo wa Kwaresima lisiwe la historian na la kupita tu,
bali lizae matunda ya kiroho ndani mwetu, tufanye mapinduzi ya kweli ya kiroho Na hatimaye atustahilishe
kushiriki utukufu wake.
No comments:
Post a Comment