Wednesday, February 18, 2015

Masomo ya Jumatano ya Majivu

18

 FEBRUARY
 Kipindi cha Kwaresima: Jumatano ya Majivu. Mwaka "B".
SOMO  1: Yoe. 2:12 - 18

 Somo katika kitabu Cha Nabii Yoel
Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia , na kwa kuomboleza; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye haghairi mabaya. N'nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke, chumbani mwake, na bibi arusi katika hema yake.
 Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie kati ya patakatifu na madhabahu na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, hata mataifa watawale juu yako; kwani wasema kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
 Hapo ndipo Bwana alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake. 

WIMBO WA KATIKATI. Zab. 51:1-4, 10-12, 15. 
K. Utuhurumie, ee Bwana kwa kuwa tumetenda dhambi 

read more.... 
somo 2. 2Kor. 5:20-6:2.  

Somo katika Waraka wa pili wa mtume Paulo kwa Wakorintho 

Ndugu zangu, basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyenu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.
  Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. Kwa maana asema, wakati mliokubali nalikusikia, Siku ya wokovu nilikusaidia; tazama wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.
.

  INJILI.Mk. 1:40-45.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.
 Siku zile, Yesu aliwaambia wafuasi wake: Angalieni msifanye wema machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye Mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige pande mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nnawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe mtoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe siri; na Baba yako aonaye sirini atakujaza.
 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wanapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pande za njia ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha funga mlango wako, usali mbele za Baba yako aonaye sirini atakujaza.
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga, Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujaza.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR