Thursday, February 19, 2015

Masomo ya Alhamisi ya Majivu Mwaka B wa kanisa Tarehe 19/02/2015

19

 FEBRUARY
 Kipindi cha Kwaresima: Alhamisi ya Majivu. Mwaka "B".
SOMO  1: Kumb. 30:15 - 20

Musa aliwaambia watu akisema: Angalia, nimekuweka leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; kwa hivi nikuagiziayo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zae upate kuwa hai na kuongezaka; Bwana Mungu wako apate kukubarikia katka nchi uingiayo kuimiliki. Lakini moyo wako ukigeuka, usipotaka kusikiza, laini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia; nawahubiri hivi leo hakika mtaangamia, hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukayo Yordani, uingie kuimiliki. Zasishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako kuitii sauti yake, na kushikamana naye, kwani hivyo ndivyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi ya Bwana aliyowaapia baba zako. Ibrahimu na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.

WIMBO WA KATIKATI. Zab. 1:1-4, 6. 
K. Heri mtu aiyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.

read more....
  INJILI.Mk. 1:40-45.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Luka.
 Siku ile: Yesu aliwaambia wafuasi wake kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso Mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka. Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane Mwenyewe, Ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate, kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha, kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR