Sunday, February 8, 2015

Masomo ya dominika ya 5 mwaka B wa kanisa(tarehe 08/02/2015


08

 FEBRUARY
 Jumapili: Dominika ya 5 ya Mwaka "B".
SOMO  1. Ayu. 7:1-4,6-7
 Ayubu alianza kusema:Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je!si kama siku za mwajiri? Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, kama mwajiri anayetazamia mshahara wake; ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha. Hapo nilalapo chini,nasema, nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, nazo zapita pasipokuwa na matumaini. kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; jicho langu halitaona mema tena.

Read More 
SOMO  2. 1Kor. 9:16-19, 22-23
 Ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipohubiri Injili! Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu , nimeaminiwa uwakili. Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili. Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu. Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishirikisha pamoja na Wengine.

INJILI. Mk. 1:29-39
 Walipotoka katika sinagogi, Yesu pamoja na Yakobo na Yohane, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkwewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake. Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia. Hata kulupokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni. Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua. Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwona wakawaambia, Watu wanakutafuta. Akawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hilo nalitokea. Akaenda akihubiri katika masinagogi yao. katika nchi ya Galilaya, na kutoa pepo.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR