15
Marchi
Mwanzo
Furahi, Jerusalemu, mshangilie ninyi nyote mmpendao; furahini, ninyi nyote mliao kwa ajili yake, mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa na faraja.
SOMO 1: 2Nya. 36:14- 16, 19-23
Somo katika kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati.
Wakuu wote wa makuhani, na watu,wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu. Naye Bwana, Mungu wa baba zao akatuma kwao kwa mikono wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake; lakini walidhiaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake; na kuwacheka manabii wake, hata alipozidi ghadhabu ya Bwana juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
wakaiteketeza nymba ya Mungu wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, wakaviharibu vyombo vyake vyote vya thamani. Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi; ili kulitimiza neno la Bwana kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ikiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini.
Ikiwa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa. Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia akisema. Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika nyinyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee.
WIMBO WA KATIKATI.
Zab. 19:7-10.
Kiitikio. Ulimi wangu na ugandamane
Na kaakaa la kichwa changu, nisipokumbuka..
read more....
SOMO 2: Efe. 2:4-10
Somo katika Waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Waefeso.
Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu alitupenda: hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhisha pamoja na Kristo; yaani, mmeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. kwa maana mmeokolewa kwa neema. Kwa njia ya imani; ambayo hiyo hailutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
INJILI.Yn. 3:14-21.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Yohane.
PYesu alimwambia Nikodemo: kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma nwana ulimwenguni ili ahukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiye amini amekwisha hukumiwa; kwa sababu hakiliami jina la mwana pekee wa Mungu.
Na hili ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. maana kila mtu atendaye mabaya huichukua nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.
Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu..
No comments:
Post a Comment