Friday, March 6, 2015

Masomo ya Dominika ya 3 ya Kwaresima, Jumapili ya tarehe 08/03/2015

08

 Marchi
 Jumapili ya 3 ya Kwaresima Masomo ya Mwaka "B".
Mwanzo

Macho yangu humwelekea Bwana daima, naye atanitoa miguu yangu katika wafu. uniangalie na kunihifadhi, Maana mimi ni Mkiwa na mteswa.
SOMO  1: Kut. 20:1- 17
Somo katika kitabu cha Kutoka.
Mungu alinena maneno haya yote akasema, mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu ya mbinguni, wala kilicho chini duniani. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu wenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wananichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe wala mwanawako, wala binti yako, wala mtumwa wako,  wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, bahari , na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato akaitakasa. Waheshimu baba na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. Usiue. Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

WIMBO WA KATIKATI. 
Zab. 19:7-10. 
Kiitikio. Wewe, Bwana, Ndiwe Mtakatifu wa Mungu..

read more....
SOMO  2: 1Kor. 1:22 - 25
Somo katika Waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho.

Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima, bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya mwanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya mwanadamu.
  INJILI.Yn. 2:13-25.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Yohane.
Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Akafanya kikoto cha kamba, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni  haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya Biashara. Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila. Basi Wayahudi wakajibu wakamwambia, Ni ishara gani unatuonyeshayo, kwamba unafanya haya? Yesu akajibu akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijegwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilonena Yesu. Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikuku wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizofanya. Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwasababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.

1 comment:

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR