Saturday, October 31, 2015
WATU SITA WAFA KWA AJALI MIKUMI MOROGORO
Watu sita wamepoteza maisha baada ya gari waliyokuwa
wanasafiria kugongana uso kwa uso na basi linalomilikiwa na kampuni ya
Prince Muro.
Ajali hiyo imetokea leo eneo la Mikumi majira ya saa sita kasorobo baada
ya gari aina ya Noah lenye nambari za usajili T339 DDA lililokuwa
linatoka mikumi kwenda Morogoro kupasuka tairi la mbele (kulia),
kupoteza mwelekeo na kisha kugongana na basi la Prince Muro lenye
nambari za usajili T160 DCC lililokuwa linatoka Dar es Salaam kuelekea
Tunduma mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Paul amewaambia waandishi wa
habari mjini humo kuwa katika ajali hiyo watu wote sita waliokuwa
wanasafiri kwa Noah hiyo walifariki dunia papo hapo huku baadhi ya
abiria wa basi la Prince Muro wakipata majeraha madogo.
Kamanda Paul amesema kati ya marehemu sita wa ajali hiyo, wanne ni
wanaume na wawili ni wanawake.
Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa
Morogoro ikisubiri utambuzi na kwamba majeruhi wametibiwa katika
hospitali ya Mtakatifu Kizito iliyopo mjini Mikumi na kuruhusiwa
kuendelea na safari.
Amesema baada ya ajali kutokea jeshi lake lilifanya upekuzi kwenye Noah
na kufanikiwa kupata vitambulisho vinne lakini akasema utambuzi wa ndugu
ndiyo utakaobainisha uhusiano wa vitambulisho hivyo na marehemu.
Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo, Kamanda Paul amesema mashuhuda wa
ajali hiyo wamesema dereva wa Noah alikuwa kwenye mwendo kasi hivyo
tairi lilipopasuka alishindwa kulimudu na kusababisha kutokea kwa ajali
hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
No comments:
Post a Comment