HABARI ZA NYUMBANI

RAISI JAKAYA KIKWETE AMEFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA NA KUTEUA WENGINE WAPYA 27.

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi. Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishirini na saba (27) zilizotokana na:   a) Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3; b) Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa Wakuu wa Mikoa; c) Kupangiwa majukumu mengine Wakuu wa Wilaya 7; na d) Kutengua uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 12.   Katika mabadiliko hayo, Mheshimiwa Rais amewateua Wakuu wapya wa Wilaya 27 ili kujaza nafasi hizo wazi. Aidha, Wakuu wa Wilaya sitini na nne (64) wamebadilishwa vituo vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vya sasa.
1) Wakuu wa Wilaya waliofariki dunia NA JINA WILAYA   1. Capt. (mst) James C. Yamungu Serengeti 2. Anna J. Magoha Urambo 3 Moshi M. Chang’a Kalambo
2) Wakuu wa Wilaya waliopandishwa cheo Wakuu wa Wilaya wafuatao wamepandishwa cheo kuwa Wakuu wa Mikoa NA JINA WILAYA MKOAALIOPANGIWA   1. John Vianney Mongela Arusha  Kagera 2. Amina Juma Masenza Ilemela  Iringa 3.Dkt. Ibrahim Hamis Msengi Moshi  Katavi 4 Halima Omari Dendego Tanga Mtwara 5 Daudi Felix Ntibenda Karatu Arusha
3) Wakuu wa Wilaya waliopangiwa majukumu mengine Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa na watapangiwa kazi nyingine ni hawa wafuatao;
NA. JINA WILAYA 1 Brig. General Cosmas Kayombo Simanjiro 2 Col. Ngemela Elson Lubinga Mlele 3 Juma Solomon Madaha Ludewa 4 Mercy Emanuel Silla Mkuranga 5 Ahmed Ramadhan Kipozi Bagamoyo 6 Mrisho Gambo Korogwe 7. Elinas Anael Pallangyo Rombo 3 4) Wakuu wa Wilaya Wanaotenguliwa Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na nyinginezo na vituo vyao ni kama inavyoonekana hapa chini:
NA JINA WILAYA   1. James Kisota Ole Millya Longido 2. Elias Wawa Lali Ngorongoro 3. Alfred Ernest Msovella Kongwa 4. Dany Beatus Makanga Kasulu 5. Fatma Losindilo Kimario Kisarawe 6. Elibariki Emanuel Kingu Igunga 7. Dr. Leticia Moses Warioba Iringa 8 Evarista Njilokiro Kalalu Mufindi 9. Abihudi Msimedi Saideya Momba 10. Martha Jachi Umbula Kiteto 11 Khalid Juma Mandia Babati 12 Eliasi Goroi Boe Boe Goroi Rorya
5) Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Wilaya zao ni wafuatao;
NA. JINA JINSI WILAYA 1. Mariam Ramadhani Mtima KE Ruangwa 2. Dkt. Jasmine B. Tiisike KE Mpwapwa 3. Pololeti Mgema ME Nachingwea 4. Fadhili Nkurlu ME Misenyi 5. Felix Jackson Lyaniva ME Rorya 6. Fredrick Wilfred Mwakalebela ME Wanging’ombe 7. Zainab Rajab Mbussi KE Rungwe 8. Francis K. Mwonga ME Bahi 9. Col. Kimiang’ombe Samwel Nzoka ME Kiteto 10. Husna Rajab Msangi KE Handeni 11. Emmanuel Jumanne Uhaula ME Tandahimba 12. Mboni Mhita KE Mufindi 13. Hashim S. Mngandilwa ME Ngorongoro 14. Mariam M. Juma KE Lushoto 15. Thea Medard Ntara KE Kyela 16. Ahmad H. Nammohe ME Mbozi 17. Shaban Kissu ME Kondoa 18. Zelote Stephen ME Musoma 19. Pili Moshi KE Kwimba 20. Mahmoud A. Kambona ME Simanjiro 21. Glorius Bernard Luoga ME Tarime 22. Zainab R. Telack KE Sengerema 23. Bernard Nduta ME Masasi 24. Zuhura Mustafa Ally KE Uyui 25. Paulo Makonda ME Kinondoni 26. Mwajuma Nyiruka KE Misungwi 27. Maftah Ally Mohamed ME Serengeti
6) Wakuu wa Wilaya waliobadilishwa Vituo Wakuu wa Wilaya wafuatao wamebadilishwa vituo vya kazi kama ifuatavyo;   JINA JINSIA WILAYA ATOKAYO AENDAYO  
1. Nyerembe Deusdedit Munasa ME Arumeru  Mbeya 2 Jordan Mungire Obadia Rugimbana ME Kinondoni Morogoro 3 Fatma Salum Ally KE Chamwino Mtwara 4 Lephy Benjamini Gembe ME Dodoma Mjini Kilombero 5 Christopher Ryoba Kangoye ME Mpwapwa Arusha 6 Omar Shaban Kwaang’ ME Kondoa Karatu 7 Francis Isack Mtinga ME Chemba Muleba 8 Elizabeth Chalamila Mkwasa KE Bahi Dodoma 9 Agnes Elias Hokororo (Mb) KE Ruangwa Namtumbo 10 Regina Reginald Chonjo KE Nachingwea Pangani 11 Husna Mwilima KE Mbogwe Arumeru 12 Gerald John Guninita ME Kilolo Kasulu 13 Bi Zipporah Lyon Pangani KE Bukoba Igunga 14 Col. Issa Suleimani Njiku ME Missenyi Mlele 16 Bw. Richard Mbeho ME Biharamulo Momba 17 Bw. Lembris Marangushi Kipuyo ME Muleba Rombo 18 Ramadhani Athuman Maneno ME Kigoma Chemba 19 Venance Methusalah Mwamoto ME Kibondo Kaliua 20 Gishuli Mbegesi Charles ME Buhigwe Ikungi 21 Novatus Makunga ME Hai Moshi 21 Anatory Kisazi Choya ME Mbulu Ludewa 22 Christine Solomoni Mndeme KE Hanang’ Ulanga 23 Jackson William Musome ME Musoma Bukoba 24 John Benedict Henjewele ME Tarime Kilosa 25 Dkt. Norman Adamson Sigalla ME Mbeya Songea 26 Dr. Michael Yunia Kadeghe ME Mbozi Mbulu 27 Crispin Theobald Meela ME Rungwe Babati 28 Magreth Ester Malenga KE Kyela Nyasa 29 Said Ali Amanzi ME Morogoro Singida 30 Antony John Mtaka ME Mvomero Hai 31 Elias Choro John Tarimo ME Kilosa Biharamulo 32 Francis Cryspin Miti ME Ulanga Hanang’ 33 Hassan Elias Masala ME Kilombero Kibondo 34 Angelina Lubalo Mabula KE Butiama Iringa 35 Farida Salum Mgomi KE Masasi Chamwino 36 Wilman Kapenjama Ndile ME Mtwara Kalambo 37 Ponsian Damiano Nyami ME Tandahimba Bariadi 38 Mariam Sefu Lugaila KE Misungwi Mbogwe 39 Mary Tesha Onesmo KE Ukerewe Buhigwe 40 Karen Kemilembe Yunus KE Sengerema Magu 41 Josephine Rabby Matiro KE Makete Shinyanga 42 Joseph Joseph Mkirikiti ME Songea Ukerewe 43 Abdula Suleiman Lutavi ME Namtumbo Tanga 44 Ernest Ng’wenda Kahindi ME Nyasa Longido 45 Anna Rose Ndayishima Nyamubi KE Shinyanga Butiama 46 Rosemary Kashindi Kirigini (Mb) KE Meatu Maswa 47 Abdallah Ali Kihato ME Maswa Mkuranga 48 Erasto Yohana Sima ME Bariadi Meatu 49 Queen Mwanshinga Mulozi KE Singida Urambo 50 Yahya Esmail Nawanda ME Iramba Lindi 51 Manju Salum Msambya ME Ikungi Ilemela 52 Saveli Mangasane Maketta ME Kaliua Kigoma 53 Bituni Abdulrahman Msangi KE Nzega Kongwa 54 Lucy Thomas Mayenga KE Uyui Iramba 55 Majid Hemed Mwanga ME Lushoto Bagamoyo 56 Muhingo Rweyemamu ME Handeni Makete 57 Hafsa Mahinya Mtasiwa KE Pangani Korogwe 58 Dr. Nasoro Ali Hamidi ME Lindi Mafia 59 Festo Shemu Kiswaga ME Nanyumbu Mvomero 60 Sauda Salum Mtondoo KE Mafia Nanyumbu 61 Seleman Mzee Seleman ME Kwimba Kilolo 62 Esterina Julio Kilasi KE Wanging’ombe Muheza 63 Subira Hamis Mgalu KE Muheza Kisarawe 64 Jacqueline Jonathan Liana KE Magu Nzega
7) Wakuu wa Wilaya wanaobaki katika vituo vyao vya sasa Wakuu wa Wilaya wafuatao wanaendelea kubaki katika vituo vyao vya sasa; NA JINA JINSIA WILAYA 
1 Jowika Wilson Kasunga ME Monduli 2 Raymond Hieronimi Mushi ME Ilala 3 Sophia Edward Mjema KE Temeke 4 Bw. Amani Kiungadua Mwenegoha ME Bukombe 5 Bw. Ibrahim Wankanga Marwa ME Nyang’wale 6 Bw. Rodrick Lazaro Mpogolo ME Chato 7 Bw. Manzie Omar Mangochie ME Geita 8 Bi. Darry Ibrahim Rwegasira KE Karagwe 9 Lt. Col. Benedict Kulikila Kitenga ME Kyerwa 10 Constantine John Kanyasu ME Ngara 11 Paza Tusamale Mwamulima ME Mpanda 12 Peter Toima Kiroya ME Kakonko 13 Hadija Rashid Nyembo KE Uvinza 14 Dkt. Charles O. Mlingwa ME Siha 15 Shaibu Issa Ndemanga ME Mwanga 16 Herman Clement Kapufi ME Same 17 Ephraim Mfingi Mbaga ME Liwale 18 Abdallah Hamis Ulega ME Kilwa 19 Joshua Chacha Mirumbe ME Bunda 20 Deodatus Lucas Kinawiro ME Chunya 21 Rosemary Staki Senyamule KE Ileje 22 Gulamhusein Kifu Shaban ME Mbarali 23 Christopher Edward Magala ME Newala 24 Baraka Mbike Konisaga ME Nyamagana 25 Sarah Philip Dumba KE Njombe 26 Hanifa Mahmoud Karamagi KE Gairo 27 Halima Meza Kihemba KE Kibaha 28 Nurdin Babu ME Rufiji 29 Mathew Sarja Sedoyeka ME Sumbawanga 30 Idd Hassan Kimanta ME Nkasi 31 Chande Bakari Nalicho ME Tunduru 32 Bibi Senyi Simon Ngaga KE Mbinga 33 Wilson Elisha Nkambaku ME Kishapu 34 Benson Mwailugula Mpesya ME Kahama 35 Paul Chrisant Mzindakaya ME Busega 36 Georgina Elias Bundala KE Itilima 37 Fatuma Hassan Toufiq KE Manyoni 38 Lt. Edward Ole Lenga ME Mkalama 39 Hanifa Mohamed Selengu KE Sikonge 40 Suleman Omar Kumchaya ME Tabora 41 Mboni Mwanahamis Mgaza KE Mkinga 42 Seleman Salum Liwowa ME Kilindi
Mabadiliko haya yameanza tarehe 18.02.2015 na ninawatakia wote utendaji kazi

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Jukwaa la Wakristo lapinga Mahakama ya Kadhi kujadiliwa bungeni

Dar es Salaam. Wakati macho na masikio ya Watanzania wengi yakielekea mjini Dodoma kesho katika vikao vya Bunge vinayotarajia kujadili Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali, Jukwaa la Wakristo nchini limeitaka Serikali isitishe kujadili marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria ya Kiislam ya mwaka 1964.
Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo leo inasema Muswada huo unaolenga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi utasabisha kuvunjika kwa misingi ya Taifa hili kama lisilo la kibaguzi na kufungamana na dini yeyote.
Taarifa hiyo pia ilisema mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ni mapendekezo makubwa yatakayokuwa na athari kubwa na nzito; kwani yanahoji msingi wa dola ya Tanzania kama dola isiyokuwa ya kidini.
“Kama ambavyo tumesema mara nyingi, masuala yanayohusu imani za dini na kujiingiza kwa Serikali katika masuala yanayohusu imani hizo yanahitaji mjadala mpana na maridhiano ya kitaifa,” inasema sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa TEC, Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa TEC, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa CPCT, Askofu Daniel Awet.
Kwa mujibu wa tamko hilo, Mahakama za Kadhi, pamoja na Mahakama za Wenyeji (Native Courts), zilizokuwepo wakati wa ukoloni zilifutwa na Sheria ya Mahakama za Mahakimu (Magistrates Courts Act) ya mwaka 1963 hivyo tangu wakati huo, mahakama hizi hazipo na hazitambuliwi na sheria yoyote. Hivyo, mapendekezo ya Muswada huu yakipitishwa ndiyo yatazianzisha.
“Kwa mapendekezo haya, Serikali inachukua jukumu la kuanzisha yenyewe taasisi za kidini kinyume na utaratibu wa kikatiba ambapo Serikali imekuwa haijishughulishi na uanzishwaji na uendeshaji wa taasisi za kidini. Hii ni kwa sababu Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu haikuanzisha mahakama au taasisi nyingine yoyote ya kusimamia Sheria hiyo bali iliweka utaratibu wa mahakama za kawaida kuitambua na kuisimamia Sheria hiyo.”
Tamko hilo linaeleza zaidi kuwa mapendekezo ya Muswada huo yanaleta sintofahamu kama mamlaka za mahakama za sasa za kusikiliza na kuamua masuala ya hadhi ya mtu, mirathi na ndoa kwa mujibu wa Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu itaendelea kuwepo.
“Aidha mapendekezo ya Muswada huu yako kimya juu ya uhusiano wa Mahakama za Kadhi na mahakama za kawaida. Kwa mfano, haieleweki (haikuwekwa wazi) kama kutakuwa na utaratibu wa rufaa, marejeo na mapitio ya maamuzi ya mahakama hizo. Endapo, kwa mfano, mtu hataridhika na maamuzi ya Mahakama ya Kadhi, je, atakuwa na haki ya kukata rufaa? Kama atakuwa na haki hiyo, rufaa hiyo itapelekwa kwenye mahakama au chombo gani?”
“Mapendekezo hayo hayo, pamoja na kwamba wadaawa wataenda kwa hiari yao, yako kimya juu ya kesi zinazohusu Waislamu na watu wa imani nyingine. Na hata kwa wadaawa ambao ni Waislamu, ikiwa upande mmoja (tuseme wa Mdai) unakwenda kwa hiari ila upande mwingine (wa Mdaiwa) unataka shauri lisikilizwe na mahakama ya kawaida, Muswada hautoi jibu nini kifanyike.”
Taarifa hiyo inasema pia kuwa suala hilo la Mahakama ya Kadhi lilikataliwa na Bunge Maalumu la Katiba wakati wa kupitishwa kwa Katiba inayopendekezwa hivyo  kushangazwa na suala hili kuibuka kwenye Muswada huu baada ya kuwa limekataliwa.
“Sisi viongozi wa Makanisa wanachama wa Jukwaa la Wakristo Tanzania tunaamini kwamba sababu zilizopelekea kufutwa kwa mahakama hizi mwaka 1963; yaani, kujenga umoja wa kitaifa, kuondoa ubaguzi katika mfumo wa kisheria na utoaji haki sawa, bado ni halali na za msingi leo hii. Kwa sababu hiyo, kwa heshima kubwa, tunashauri  kwamba Serikali iondoe Muswada huu Bungeni ili kuepusha kuvunja misingi ya Taifa hili kama taifa lisilo la kibaguzi na lisilo fungamana na dini,” inasema taarifa hiyo.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Matukio mbalimbali ya picha kutoka Bungeni  leo Alhamisi Tarehe 29/01/2015, mjini Dodoma

PG4A9014
Spika wa Bunge Anne Makinda akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Januari 28, 2015
PG4A9034
Spika wa Bunge Anne Makinda akitoka Bungeni baada ya kulazimika kuahirisha kikao kabla ya muda wake.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>   Jana huenda ikawa  ni siku moja  ambayo itaingia kwenye headlines kubwa za siasa TANZANIA kwa mwaka 2014/2015 ambapo January 24 /2015 mchana kulikuwa na taarifa za kujiuzulu kwa waziri Muhongo aliyekua kwenye Wizara ya nishati na madini na jioni likatagazwa baraza la mawaziri.

Kubwa nyingine kwenye upande huohuo ni ishu ya Rais Kikwete kutangaza mabadiliko madogo ndani ya Baraza la Mawaziri ambako kuna waliohamishwa na wapo waliokuwa Manaibu Mawaziri sasa ni Mawaziri, list yote ni hii hapa;

Mawaziri

George SimbachaweneWaziri wa Nishati na Madini

Mary Nagu- Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais- Mahusiano na Uratibu

Christopher Chiza- Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji

Harrison Mwakyembe- Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

William Lukuvi- Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi

Steven Wasira- Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Samuel Sitta- Waziri wa Uchukuzi

Jenista Muhagama- Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

Manaibu Waziri

Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais- Muungano

Angela Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi

Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Anne Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Charles Mwaijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

 Kama una chochote cha kushare kuhusu madaliko haya unaweza kuniachia comment yako hapa chini mtu wangu.

Profesa Muhongo ajiuzulu, asema yeye ni mtu safi, ajisifia alipeleka umeme vijijini.

Kufuatia kuhusishwa na sakata la uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameamua kumuandikia barua Raisi ya kujiuzulu wadhifa wake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo ameelezea furaha yake ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka katika wizara yake kwa kipindi chake akisema kuwa nidhamu na uwajibikaji vilikuwa dira ya maendeleo wizarani hapo.
Profesa Muhongo amekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa anaamini kujiuzuru kwake kutaisaidia Serikali na Bunge kutuliza malumbano ya Sakata hilo ambalo linazidi kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Amesema yeye si mwizi na hawezi kuuza utu wake kwa kupewa rushwa ili kuwakandamiza watanzania.
“Nimeamua kujiuzuru kwa dhati kabisa bila kushinikizwa na mtu yeyeote, inaonekana mimi ndiyo nitamaliza mjadala huu wa sakata la Escrow, tuna mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kujadiliwa lakini watu wamekazana na Escrow, nimemuandikia Rais barua rasmi ya kujiuzuru wadhifa wangu, amesema Profesa Muhongo.
Amesema pamoja na kujiuzuru anatarajia mapema kuzungumza na watanzania ili kuwaeleza ukweli wa sakata la Escrow na kujiuzuru kwake ili kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa Tanzania na watu wake.
Amesema yeye amelelewa katika malezi yenye maadili mema na kwamba tokea alipomaliza masomo yake aliaswa kutopokea ama kutotoa rushwa hivyo hawezi akapokea rushwa kwa ajili ya kuutukana utu wa mtanzania hicho ndicho kinachomgharimu.

 >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Utulivu utawale mjadala wa Akaunti ya Escrow

Baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwasilisha bungeni ripoti kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow juzi, tunapenda kulipongeza Bunge kwa kuipa kamati hiyo ya PAC, chini ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jukumu la kuchunguza na kupata ukweli kuhusu Sh306 bilioni zinazodaiwa kuchotwa katika mazingira ya kutatanisha kutoka kwenye akaunti hiyo iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Tunaipongeza pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kuiwezesha PAC kupata taarifa muhimu katika kukusanya na kuandika ripoti iliyoiwasilisha bungeni.
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), nayo inastahili pongezi kwa kuandaa na kutoa taarifa za kina kwa PAC kuhusu Akaunti hiyo ya Tegete Escrow.
Kama wengi wanavyofahamu, ofisi hiyo ya CAG, kwa muda mrefu sasa imekuwa ikifanya kazi nzuri ya kuanika wizi na ubadhirifu wa fedha za umma, ingawa kazi yake hiyo imekuwa ikikwazwa na mamlaka husika kutotekeleza mapendekezo yaliyomo katika ripoti zake, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha wote wahusika.
Hapa hatuwezi kusahau pia kuipongeza Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA), kwani ripoti ya PAC imethibitisha kwamba tatizo la muda mrefu la upotevu wa fedha za Serikali kutokana na misamaha holela ya kodi limechochewa na wanasiasa kuingilia kazi za mamlaka hiyo.
Pengine yafaa tujiulize hapa kama ripoti ya PAC imeeleza ukweli, ukweli mtupu? Je, ni kweli kwamba fedha zilizowekwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow hazikuwa fedha za umma kama baadhi ya viongozi serikalini wamekuwa wakidai, licha ya vielelezo vilivyotolewa katika ripoti ya PAC?
Je, kuna watu watawajibishwa? Kuna viongozi watajiuzulu kutokana na ripoti hiyo kali iliyowasilishwa bungeni?
Tunauliza maswali hayo kutokana na kuwapo orodha ndefu ya watu wenye hadhi katika jamii ambao PAC imesema walilipwa fedha nyingi inayosemekana ilitoka katika akaunti hiyo ya Tegeta Escrow.
Kama itagundulika kwamba fedha walizolipwa zilikuwa za umma, kwamba zilipaswa kupelekwa Tanesco, waliolipwa fedha hizo watalazimishwa kuzirudisha? Maswali haya na mengine bila shaka yanaumiza vichwa vya Watanzania, hasa wakati huu ambao kuna mjadala mkali kuhusu jambo hilo ndani na nje ya Bunge.
PAC imetoa mapendekezo yake, hivyo mjadala wa mapendekezo hayo utakapomalizika, Bunge litajadili utetezi wa watu wote waliotuhumiwa katika ripoti hiyo na kufanya uamuzi. Wananchi wengi bila shaka watafuatilia maazimio ya Bunge kwa shauku kubwa.
Jambo la msingi hapa ni jinsi Serikali itakavyoipokea ripoti hiyo ya PAC na mapendekezo yake, hasa baada ya baadhi ya watendaji wake kupewa taswira hasi na kuonekana mbele ya jamii kama maadui wa taifa na wananchi, ambao wanapaswa kuwatumikia kwa uzalendo na moyo mkubwa? Hili ni jambo muhimu sana kwa Serikali, kwani mpira tayari umepigwa golini kwake.

<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

FAIDI KWA PICHA, JINSI SITTA ALIVYOWATULIZA WAPINZANI KUHUSU UFISADI WA ESROW,SOMA HAPA KUJUA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Mbunge wa Urambo, Mh. Samuel Sitta (katikati) akiwatuliza  na baadhi ya wabunge wa Upinzani, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizugumza na Mbunge wa Viti Maalum Rachel Mashishanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwenyekiti wa Bunge, Mh. Mussa Azan Zungu akiongozwa na Mpambe wa Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati alipositisha kikao cha Bunge cha asubuhi leo Novemba 26, 2014.




>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

Kiti moto! Bunge la Tanzania

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema mjadala ndani ya Bunge kuhusu sakata la akaunti ya Escrow upo pale pale na hakuna mhimili mwingine wowote unaoweza kulizuia Bunge kufanya hivyo. ‘’Wabunge msiishi kwa wasiwasi sisi kanuni zetu zipo wazi hakuna mtu au muhimili unaoweza kutuzuia kufanya kazi yetu ya kibunge, hiyo haipo,’’ alisema Makinda.

Spika alitoa mwongozo huo baada ya kuombwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP) mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu. Katika mwongozo wake kwa mujibu wa kanuni ya 68(7) Cheyo alisema kuna taarifa kuwa sula hilo la Escrow ambalo Bunge linatakakujadili kwa sasa limepelekwa Mahakamani ili kuzuia Bunge kuendelea kujadili suala hilo.

‘’Mheshimiwa Spika sasa naona hii tabia hapa nchini imekuwa imeshamili kukiwa na jambo ambalo Bunge linashughulikia watu wengine kiujanja unjanja wanakimbilia mahakamani kulizuia Bunge kufanya kazi yake naomba muongozo wako katika hili,’alisema Cheyo.

Akitoa muongozo wake Spika aliwataka wabunge kuacha kuishi kwa wasiwasi kwa kuwaeleza kuwa hakuna mtu anayeweza kulikataza bunge kufanya kazi yake. Spika alisema hapo awali waliambiwa kuwa kuna kesi nyingi mahakamani ambazo zinahusiana na suala hilo la akaunti ya Escrow. Alisema hata hivyo baada ya kufuatilia kesi hizo zote hakuna kesi mahususi inayohusu jambo ambalo Bunge linaenda kujadiliana juu ya sakata hilo la Escrow.

Spika Anne alisema Bunge lina sheria zake za kinga na kama kutakuwa na muhimili mwingine ambao unakuwa na uwezo wa kuzuia bunge kufanya kazi yake basi hakutakuwa na Bunge.’ ‘’Mjadala wetu upo pale pale na kwa sasa nasubiri kama Kamati yetu ya PAC imekamilisha kazi yake ili nao watuletee taarifa yao hapa bungeni tuijadili’’

Hata hivyo Spika alisema mpaka Jumatatu asubuhi alikuwa bado hajapata taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe kama wamekamlisha kazi yao kwani kikanuni ni lazima wakikamilisha kazi hiyo hutakiwa kumtaarifu Spika kwa barua ilinaye aingize katika shughuli za Bunge. Aidha Makinda alisema pamoja na kuendelea na mjadala huo pia wabunge jana watapewa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa majina.


Spika alisema nia ya kugawa taarifa hiyo ya CAG kwa majina ni kuepukana na taarifa hizo kuwafikia watu wengine ambao si wabunge. Alisema taarifa kutoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC itagawiwa leo mara baada ya kamati hiyo kuwasilisha bungeni taarifa yao.‘’Hatuwezi kuweka mezani taarifa ya CAG kwani tukiweka hivyo Kamati haiwezi kuleta tena taarifa yao hivyo tunagawa taarifa hiyo ya CAG kwa majina ili taarifa ya kamati ndiyo itawekwa mezani mara nitakapopata taarifa kuwa wamemaliza kazi yao,’’alisema. Alisema taarifa hiyo ya CAG itatumika kama kiambatanishi baada ya kutolewa kwa taarifa ya kamati ya PAC ambayo inatarajiwa kutolewa leo bungeni.

Naye kwa upande wa John Mnyika (Ubungo-Chadema) alimpongeza Spika kwa uamuzi wake wa kusisitiza kuingizwa bungeni kwa taarifa hizo mbili.Mnyika alisema hayo alipokuwa akioomba muongozo wa Spika kuhusiana na kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow. ‘’Kwanza nikupongeze kwa uamuzi wako wa kusema kwamba hakuna jambo ambalo litazuia bunge kuletewa hiyo ripoti na kuijadili lakini mheshimiwa Spika ningependa utuhakikishie hili’’.

‘’Mimi nina taarifa ndio maana nasema utuhakikishie,naomba nikusomee Pan African Power wamefungua kesi ‘’High court’’ kuzuia mjadala wa Escrow bungeni walengwa wakiwa ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, CAG, PCCB, na Wizara ya Nishati na Madini, mheshinmiwa spika mimi naomba muongozo wako,’’ alisema Mnyika.

Alisema ni vyema Ofisi ya Spika ikachunguza kama taarifa hiyo ni ya kweli au la lakini hata kama ikichunguza na hata kama jambo hili ni kweli bunge lisikubali kwa namna yoyote madaraka yake na mamlaka yake kuingiliwa. ‘’Mheshimiwa Spika naomba mwongozo mahususi kabisa katika eneo hili mjadala huu lazima ufanyike na ututangazie kwamba, mjadala huu unaanza kujadiliwa,’’alisema. Katika kujibu mwongozo huo Spika alirejea kauli yake kuwa hawezi kutamka rasmi kwamba leo Mjadala huo utaanza ila anasubiri taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa PAC kama wamemaliza kazi yao.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

Azimio la Arusha katika kupambana na ujangili Kusini mwa Ikweta!

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema inahitajika dhamira ya kweli kutoka kwa wadau wote katika kutekeleza Azimio la Arusha la kukabiliana na ujangili na kuendeleza hifadhi za wanyama katika nchi za Afrika Mashariki na zilizo Kusini mwa Ikweta.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi, Novemba 8, 2014 mara baada ya kufunga mkutano wa kikanda wa siku mbili uliojadili mbinu za kupambana na biashara haramu ya wanyamapori ulioandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha, Waziri Mkuu alisema: “Suala hili linataka uwajibikaji wa pamoja. Mashirika na taasisi, wananchi na viongozi sote kama wadau wakuu, kila mmoja anapaswa kushiriki vita hii kama kweli tunataka tuitokomeze.”
“Kwenye hili Azimio la Arusha na nyie waaandishi wa habari pia mna sehemu yenu mmetajwa... wamesema wanatafuta jinsi ya kushirikiana na vyombo vya habari ili visaidie kutoa elimu kwa jamii kama njia ya kuelimisha umma,” alisema. Waziri Mkuu aliwaeleza waandishi hao kwamba Azimio hilo lina vipengele 20 ambavyo vinataka utekelezaji katika ngazi ya nchi mojamoja, ngazi ya kanda na ngazi ya kimataifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
“Nimepata faraja kwamba mkutano huu haukuisha kijumlajumla tu, bali umekuja na maazimio 20 ambayo yametengwa kwa ajili yetu sisi wa ndani, mengine yanahusisha ushirikiano wa kikanda na yako mengine yanawahusisha wadau wa maendeleo,” alifafanua.
Ili kutekeleza azimio hili, nimeshauri iundwe timu itakayoshirikisha vyombo vingi zaidi badala ya kuiachia Wizara ya Maliasili na Utalii peke yake. Timu hii ikutane kila baada ya miezi sita ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio haya na ikibidi Waziri atoe taarifa bungeni kuhusu utekelezaji huo,” alisema Waziri Mkuu.
Mapema, akizungumza na washiriki wa mkutano huo wakati wa kuufunga, Waziri Mkuu alisema kuwepo kwa watu wa ngazi tofauti kwenye mkutano huo ni kielelezo tosha cha umakini wao na nia thabiti ya kutokomeza ujangili katika ukanda huu. “Tumeanzisha vita, tusisahau kwamba bado kuna kazi kubwa mbele yetu na vita haijaisha. Tuzidishe mapambano katika sehemu tatu: kwenye nchi unakofanyika ujangili, nchi ambazo nyara zinapitishwa na nchi zinazopokea ama kununua hizo nyara,” alisema Waziri Mkuu.
“Nakubaliana nanyi kwamba hakuna nchi inayoweza kukabili suala la ujangili ikiwa peke yake. Tunahitaji tuwe na sera mahsusi, sera ya pamoja ya kutuunganisha na kutuongoza wakati tukitekeleza Azimio hili kwa kusaidiana na wadau wa maendeleo,” alisema.
Alisema Azimio hilo litaipa kazi ya ziada ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo kazi kubwa itakuwa ni kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa wa Azimio hilo unakuwa wa ufanisi. Jumla ya nchi tisa zimetia saini azimio hilo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.

 >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>> 

UKAWA Matumaini Mapya kwa Watanzania.

 Nimesema sina jibu la moja kwa moja, kwa sababu sasa ni dhahiri umoja huu wa vyama vya siasa vya upinzani nchini ambao ulianzia Dodoma kwenye Bunge Maalumu la Katiba, umepevuka
Siku hizi Ukawa ni habari kubwa katika jamii yetu. Ni jina ambalo siyo geni tena katika masikio ya walio wengi kwani limekuwa likitajwa asubuhi, mchana na hata usiku.
Ni nadra siku hizi kupitisha siku bila kulisikia jina hilo likitajwa. Kwa maana hiyo, unaweza kujiuliza Ukawa ni nini hasa na kwa nini linatajwa kiasi hiki?
Ninajiuliza, hivi ni nani aliyebuni na kuanzisha jina hili la Ukawa hadi likawa kama ilivyo leo?
Hakuna shaka, viongozi wa Ukawa, kina Freeman Mbowe na Chadema yake, Profesa Ibrahim Lipumba na CUF, James Mbatia na NCCR- Mageuzi, wanatambua asili ya Ukawa na jinsi gani ya kuyaishi malengo ya kuasisiwa kwa umoja huo?
Nimeuliza swali hili, je, Ukawa ni nani au nini hasa? Ninasema sina jibu la moja kwa moja kwa nini Ukawa imegeuka kuwa gumzo kubwa siku hizi katika jamii yetu.
Nimesema sina jibu la moja kwa moja, kwa sababu sasa ni dhahiri umoja huu wa vyama vya siasa vya upinzani nchini ambao ulianzia Dodoma kwenye Bunge Maalumu la Katiba, umepevuka.
Ushahidi wa jinsi ambavyo Ukawa inafahamika hauhitaji mtu ama awe msomi au hata mchambuzi wa masuala ya siasa, uchumi, ndipo akubali kwamba Ukawa ni kazi nyingine.
Ukweli huo unaonekana hata kwa macho, kama ilivyotokea kuwa kiasi cha wiki moja iliyopita pale umoja huo ulipofanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam wakijadili mambo mengi.
Baada ya mkutano huo wa Jangwani, mijadala mingi ambayo imetawala katika jamii kwa sasa ni kuhusu umakini wao katika kutekeleza maazimio yao saba ambayo umoja wao umejiwekea.
Ni suala la muda na kusubiri kuona kinachoendelea ndani ya Ukawa, ingawa nafahamu wapo wengi au wachache wanaobeza nguvu hiyo ya Ukawa kuilinganisha na ile ya soda ambayo hudumu kwa sekunde chache, kisha ikapotea.
Pia, wapo watu ambao wamekuwa wakijaribu hata kupenyeza chuki ndani ya umoja huo ili azma yao ya kushirikiana wakati wa uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ikwame.
Kwa bahati mbaya, azma hiyo inaelekea kuwa itakuwa ngumu endapo Ukawa itakuwapo na hata kutambuliwa kisheria, kama ambavyo tumeambiwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, ambayo inabeba jukumu la kusimamia sheria ya vyama vingi nchini.

 >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

NHC sasa kujenga miji ya kisasa Dar es salaam

Tanga.Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limepata mkopo wa Dola za kimarekani 1.7 bilioni kutoka China kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa miradi mitatu mikubwa ya miji ya kisasa jijini Dar es salaam.

Mkopo huo ambao umetolewa na makampuni mawili tofauti ya nchini China hauna dhamana ya Serikali kutokana na Shirika la NHC kuanza kuaminiwa kukopesheka bila kutegemea udhamini.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Nehemiah Mchechu alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika jijini hapa.
Aliyataja makampuni yaliyotoa mkopo huo kuwa ni ya kihandisi ijulikanayo CRJE ambapo imetoa dola za kimarekani 1.bilioni kwa ajili ya ujenzi wa mji wa kisasa wa Salamanda Creek Jijini Dar es salaam.
Kampuni hiyo ya kihandisi alisema pia imetoa dola za kimarekani500.milioni kwa ajili ya ujenzi wa eneo la kibiashara litakalotambuliwa kama Financial Square pia la jijini Dar es salaam.
Aliitaja kampuni nyingine ya nchini China iliyotoa mkopo kwa NHC bila ya masharti ya kudhaminiwa na Serikali ya Tanzania kuwa ni PollyTechnologies ambayo imekopesha dola za kimarekani 200.milioni kwa ajili ya ujenzi wa mji wa kisasa wa Valahala Estate utakaokuwa Masaki Jijini Dar es salaam. na kwamba fedha hizo zitasaidia kuliwezesha shirika la NHC kutekeleza miradi hiyo.Alisema fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuliwezesha shirika hilo kutekeleza ujenzi wa miji hiyo ambayo itaibadilisha Dar essalaam kuwa ya kisasa nay a kuwezesha kufanyika shughuli bila msongamano kama ilivyo sasa.
“Dar es salaam tuna miradi mikubwa ya uwekezaji ikiwamo ya Tanganyika Parkers ambayo tumeshakabidhiwa hati ya kumiliki eneo hilo, lakini pia kuna Kigamboni na Luguruni”alisema Mchechu.
Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi kilifunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi,Alpahyo Kidata ambayealiseka Serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha miradi ya NHC inatekelezwa kama ilivyopangwa.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Washauriwa kuchangamkia mfunzo ya ujasiriamali


















MWAMKO mdogo wa wajasiriamali katika kujitokeza kwenye mafunzo yanayotolewa bure, umetajwa kuwa chanzo kikubwa cha kushindwa kupamabana na umasikini.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) mkoani hapa, Abel Mapunda wakati akizungumza na Tanzania Daima.
Alisema wajasiriamali walio wengi wako tayari kuendesha biashara zao bila utaalamu zaidi, jambo linalowafanya kutolipa kipaumbele mafunzo.
“Walio wengi wakielezwa kuwa kuna mafunzo juu ya ujasiriamali wanaoufanya, hawako tayari hata kama mafunzo hayo yanatolewa bure,” alisema.
Mapunda alisema kutokana na umuhimu huo, aliwataka wajasiriamali hao kulipa kipaumbele suala la mafunzo ili waweze kuboresha utengenezaji wa bidhaa zao na namna ya kupata masoko kwa wakati.
Pia alisema kwa sasa Sido inaendesha mafunzo kwa vijana wapatao 35 ambao wanafundishwa kutengeneza bidhaa za ngozi baada ya kuingia mkataba na Shirika la Misaada la Uholanzi.
Alisema mafunzo hayo yalianza Oktoba mwaka huu, na yatafungwa Novemba mwaka huu, ambapo kati ya washiriki 35, washiriki 10 ni wanawake na 25 ni wanaume.

Usafiri wa daladala Dar es salam hatari

Dar es Salaam. Maisha ya maelfu ya Watanzania yapo hatarini baada ya kubainika kuwa kwenye magari ya abiria maarufu daladala ya jijini humo, yanayotoa huduma za usiku kwa safari za kwenda na kutoka maeneo mbalimbali yamekuwa yakihusishwa na mtandao wa vibaka unaoendesha vitendo vya uporaji na ukabaji.

Mtandao huo unaelezwa kufanya vitendo hivyo kwa kutumia silaha mbalimbali ikiwamo visu na bastola, huku baadhi ya vibaka hao wakitumia magari hayo kujificha kwa kujifanya ni abiria.

Mbali na uhalifu huo unaoendelea kufanyika kwenye daladala nyakati hizo za usiku, magari mengi yanayotoa huduma za usafiri nyakati hizo hadi alfajiri ni mabovu yakiwa pia hayana vibali vya kutoa huduma hizo.

Magari hayo yanayofahamika kwa jina la ‘daladala bubu’ au ‘ya kuwanga’ madereva wake pia hufanya kazi hiyo bila ya kuwa na leseni za udereva, jambo linalohatarisha zaidi maisha ya abiria.

Uchunguzi wa gazeti hili katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo ikiwamo Sinza, Ubungo, Kariakoo, Faya, Buguruni, Gongo la Mboto Machinjioni, Kimara, Mbezi, Magomeni, Kinondoni, Tandika, Temeke, Yombo Dovya, Vingunguti, Bom Bom na Machimbo, umebaini kuwa magari hayo hufanya kazi nyakati za usiku pekee kutokana na kutokuwapo askari ama kuwapo askari wachache wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Gazeti hili limebaini kuwa wizi kwenye daladala hizo, madereva wa daladala kuwapa makondakta au wapiga debe kuendesha magari ya abiria vinaendelea kushamiri, huku nyakati za hatari zaidi kwa daladala hizo ni kuanzia saa 6 usiku hadi alfajiri.

Uhalifu unaofanywa

Uhalifu unaofanywa kwenye magari hayo unahusisha vibaka wanaokuwa ndani ya gari ambao hujifanya kuwa miongoni mwa abiria.

Imebainika kuwa abiria akikaa vibaya ndani ya daladala, vibaka hao hutumia nafasi hiyo na kujihalalishia chochote watakachoweza kuibia.

Aina nyingine ya vibaka ni wale wanaokula njama na madereva na kondakta wa daladala. Vibaka hao pia hujifanya abiria kwenye daladala bubu husika ambapo wakifika kituoni hujihusisha na kupiga debe kuita abiria, lakini mbele ya safari dereva hubadili njia, akiweza kwenda vichochoroni ndipo abiria huvamiwa na kuporwa mali zao huku wakitishiwa kwa silaha.

Uchunguzi unaonyesha kuwa aina nyingine ya wizi huo hufanywa na kundi la vibaka ambalo hujifanya ni abiria ambapo kila mmoja hulenga kumfanyia uhalifu abiria mmoja.

“Abiria akishuka tu na yeye anashuka, humfuata na kumwibia, halafu anakwambia utembee bila kugeuka. Ukigeuka tu wanakuchoma na kisu au silaha yoyote wanayokuwa wamejihami nayo,” alieleza mmoja wa madereva wa daladala aliyeomba jina lihifadhiwe kwa kuwaogopa vibaka hao.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>.

 

Sheikh: Ahadi ya Pinda ‘kitanzi’ cha CCM

Dar/Siha. Suala la Mahakama ya Kadhi jana liliibuka wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Idd el Haji wakati naibu Imamu wa Msikiti wa Shafii, Sheikh Othman Amani aliposema kuwa ahadi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu Mahakama ya Kadhi ndiyo itakayoamua kura za Waislamu dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika kutuliza mvutano baina ya pande mbili zilizokuwa zikibishana juu ya kuingiza Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba wakati wa kikao cha Bunge Maalumu la Katiba wiki iliyopita, Waziri Pinda alisimama na kuahidi kuwa Serikali itawasilisha muswada wa kutaka chombo hicho kitambuliwe kwenye Bunge la Februari.
Akihutubia baada ya Swala ya Idd al Haji kwenye Viwanja vya Msikiti wa Taqwa, Ilala jijini Dar es Salaam jana, Sheikh Amani alisema Waislamu wanasubiri Mahakama ya Kadhi iliyopo itambuliwe kimfumo na iwepo ndani ya Katiba.Alisema kila mmoja miongoni mwa Waislamu ametia akilini na kwamba wanamfuatilia Waziri Mkuu ili Februari muswada uende bungeni na Mahakama ya Kadhi ikae sawasawa.
“Tunachotaka, iwe ndani ya Katiba na kikubwa tunafanya hivyo kwa busara na hekima. Tusitumie mabavu mpaka viongozi watakapotuambia sasa jamani tusiipigie kura CCM... Hayo maelezo yatakuja baadaye. Kwa sasa tunakwenda polepole, kuna mwelekeo wa kuelewana,” alisema.Alisema wanachokitaka Katiba ndiyo itaje Mahakama ya Kadhi kwa sababu Waislamu ni sehemu ya walipa kodi wa nchi hii na hivyo wana haki hiyo.
 “Kwamba upelekwe muswada ukafikiriwe wengine wakubali, wengine wakatae... Ni muswada moja kwa moja unatakiwa upite, kwa sababu sisi nasi ni wahusika katika nchi hii,” alisema Sheikh Amani.
 Vijana na maendeleo
Mkoani Kilimanjaro, vijana wa Kiislamu wametakiwa kuwa wamoja na kufahamu umuhimu wao katika maendeleo ya mkoa wao na nchi kwa ujumla ili watumie ujuzi na nguvu walizonazo kwa manufaa ya Taifa.

1 comment:

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR