Jiografia ya Makardinali wanaoingia kwenye Conclave mjini Vatican
Kwa jumla, kuna Makardinali 115 wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura wanaoanza mchakato huu kwenye Kikanisa cha Sistina kwa kula kiapo, tafakari ya Neno la Mungu na uchaguzi wa kwanza. Makardinali 60 wanatoka katika nchi za Ulaya, kuna Makardinali 33 kutoka Amerika, Makardinali 11 kutoka Barani Afrika, Asia kuna Makardinali 10 na Oceania kuna Kardinali mmoja. Itakumbukwa kwamba, kwenye Conclave ya Mwaka 2005, Kenya haikuwa na Kardinali, lakini mwaka huu, Kardinali John Njue yupo.
Kuna Makardinali 40 ambao wametekeleza utume wao au bado wanaendelea kufanya shughuli mbali mbali mjini Vatican. Kati ya Makardinali wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura 67 ni wale walioteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.
Wastani wa umri wa Makardinali wanaopiga kura ni kati ya miaka 71. Kardinali Walter Kasper mwenye umri wa miaka 80 ni kati ya wale waliobahatika kuingia katika Conclave wakiwa na umri mkubwa zaidi. Kati ya Makardinali vijana wana umri wa miaka 54 na 56. Kardinali Luis Antonio Tagle ana umri wa miaka 56.
Mwishoni, itakumbukwa kwamba, kundi la Makardinali Maaskofu lina Makardinali 6; Kundi la Makardinali Mapatriaki lina jumla ya Makardinali 4; Kundi la Makardinali Mapadre lina jumla ya Makardinali 153 na Makardinali Mashemasi wako 44. Kuna jumla ya Makardinali 207.
No comments:
Post a Comment