Saturday, September 15, 2012

ASANTENI SANA..............

MAPENDO SANA.........ME PIA KAMA KATIBU WA VIWAWA PAROKIA YA BOKO NAPENDA SANA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA WALEZI PD. MAJETA, PD DISMAS, SISTER SABINA NA FRATEL PAUL,PIA KWA BARAZA LA WALEI PAROKIA YA BOKO NA BUNJU, UONGOZI WA VIWAWA PAROKIA YA BOKO,UONGOZI WA KIGANGO CHA BUNJU,MABWE PANDE,KIDIMU NA VIKAWE KWA PAMOJA SASA NI PAROKIA YA BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMEL- BUNJU.

PIA NAWASHUKURU VIONGOZI WA KIGANGO CHA BOKO, MBWENI NA MBWENI MALINDI KWA PAMOJA SASA NI PAROKIA YA MWENYE HERI ISIDORI BAKANJA- BOKO. PAMOJA NA VIJANA WOTE WA PAROKIA YA BUNJU NA WA PAROKIA YA BOKO KWA USHIRIKI WAO KWANZIA KWENYE MAJETA CUP MPAKA KWENYE TAMASHA, TUNAWAPENDA SANA NA UPENDO UZIDI MIOYONI MWETU ILI TUWEZE KUUKUZA ZAIDI UTUME WETU WA VIWAWA.

 PIA NAWASHUKURU WAZAZI NA WALEZI KWA MICHANGO YAO ILIYOFANYA SISI KUWEZA KUFANIKISHA YOTE HAYO, MUNGU AWABARIKI SANA NA AWAZIDISHIE PALE WALIPOTOA.

NA MWISHO NAWASHUKURU SANA WAKUFUNZI WOTE TULIKUWA NAO KWA KUUTOA MUDA WAO WANAKUFUNDISHA VIJANA. MUNGU AWABARIKI SANA.

MWISHO NI KWA KAMATI ZOTE ZA TAMASHA KAZI YENU IMEONEKANA NA TUNAWASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO ULIOTUPATIA NA KWA WALE NILIOWAKWAZA NAWAOMBA WANIWIE RADHI NA TUZIDI KWA PAMOJA KUUENDELEZA HUU UTUME WETU.
                                       NAWAPENDA SANA

CHANGAMOTO ZA VIWAWA


CHANGAMOTO KUBWA KWA VIWAWA.

1. Utume Wetu
Changamoto tuliyonayo ni kuona namna gani tunaweza kuendeleza au
kuanzisha utume wa Viwawa katika ngazi ya Kigango, Parokia na Jimbo
hasa kwa vijana ambao ni walengwa wakuu, hivyo kufanya vijana wengi
kujiunga na kujua utume halisi wa Viwawa.
Utume halisi wa Viwawa ni Tafakari ya Maisha kwa kutumia njia ya
Kuona, Kuamua, Kutenda na Kutafakari, hufanyika katika vikundi vya
watu wasiozidi watano kwa kila wiki mara moja.
Kuna njia tatu za kufanya Tafakari ya Maisha (i)Tafakari ya wazi
(ii) Tafakari ya Injili (iii) Tafakari ya mada.
Lazima tutambue Tafakari ya Maisha ni Utume halisi wa Viwawa Duniani
kote.Mwanzilishi wa Viwawa Joseph kardinali Cardijn alisema pasipo
Tafakari ya Maisha hakuna Viwawa hai
Kwa kutotumia njia ya Tafakari ya Maisha kama alivyosema mwanzilishi
tunapoteza ladha ya kukubalika na Vijana na kuonekana kama chama
kisicho na malengo au kukosa mwelekeo.
Wengine wanadiliki kutuita waimba kwaya,wacheza ngoma,wababishaji.
sisi atutambuliki kwa shughuri zetu tu tunazofanya bali kwa mang’amuzi
ya utume wetu.Vijana wengi wana matatizo ya Kiroho na Kimaisha
lengo la Tafakari ya Maisha ni kutatua matatizo ya vijana kupitia njia
ya Kuona,Kuamua,Kutenda na Kutafakari.Tafakari ya Maisha hutoa
ufumbuzi wa kina, endelevu na uponyaji wa ndani.



Sunday, September 2, 2012

SALA YA VIWAWA

   SALA YA VIWAWA

Bwana Yesu nashukuru kwa siku hii ya leo.Nakukabidhi kazi za
mikono yangu,na matumaini yangu,jitihada zangu,furaha zangu na
huzuni zangu.

Nisaidie mimi na vijana wenzangu ili tuweze kufikiri kama wewe
kufanya kazi na wewe na kuishi ndani yako.

Nisaidie nikupende kwa moyo wangu wote na kukutumikia kwa nguvu
zangu zote.

YOTE MIPANGO YA MUNGU

Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli- Bunju Padre Thomas Mtei akiwa na Padre Adolph Majeta aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Boko. wakati wa sherehe za Upadrisho na Bunju kutangazwa Parokia.

Monday, August 27, 2012

WALEI PAROKIA

Baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Walei parokia yaBoko wakiwa na Baba Paroko siku ya somo wa Parokia na kilele cha Tamasha la vijana tarehe 12/08/2012

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR