Monday, June 9, 2014
Thursday, June 5, 2014
Masomo ya Jumapili 8/6/2014 Dominika ya sherehe ya Pentekoste Mwaka A
08
|
JUNI
SHEREHE YA PENTEKOSTE
MWAKA "A" 2014
MWAKA "A" 2014
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI

KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI
Zaburi: Tazama sala ya siku
Zab: 104:1-24, 29-31,34
Ee Bwana, Nawe waufanya upya uso wa nchi.

SOMO LA 1: Mdo. 2:1-11
Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. kakaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Waparthi na wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapodokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu ba Kerene, na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu
SOMO 2:1Kor.12:3b-7, 12-13
Hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yule yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. kisha pana tofauti za kutenda kazi bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. maana kama vile mwili mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi , ni mwili mmoj; vivyo hivyo na Kristo. kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
INJILI:Mt. 28:16-20
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawambia, pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
MATANGAZO
mara baada ya misa ya pili saa 4:00 asubuhi, Parokiani Boko, Tutakuwa na kikao cha VIjana waote wanaotarajia kushiriki ziara ya uinjilishaji Jimbo la Mbulu Parokia za Dareda, Sanu, Daudi na endabashi, pia kwenda kutembelea mbuga ya Wanyama ya ngorongoro.
Fika na mchango wako ikiwa bado haujamalizia mchango ni tshs 150,000 kwa mshiriki, ziara ni tarehe 01/07 mpaka tarehe 07/07/2014....
Tunawatikia Dominika njema, Amani ya Bwana Iwe nasi.........Mapendo sana,,,,,,,
Jumapili ya Pentekoste
Katika Ukristo vipaji vya Roho Mtakatifu ni
misimamo tunayotiwa na Roho Mtakatifu wa kuangaza, kuimarisha na
kuzoesha akili na utashi wetu ili kushirikiana naye katika mambo ya
utumishi wa Mungu.
Kusudi tujue kweli muundo wa Kiroho unaotuwezesha kuishi kama wana wa Mungu, haitoshi tuyajue maadili. Ni lazima tuzingatie pia vipaji vya Roho Mtakatifu, pasipo kusahau namna mbalimbali za kupata msaada wa Mungu.
Orodha ya Vipaji saba ya Roho Mtakatifu
Orodha ya vipaji ya Roho Mtakatifu kuanzia juu:
Hekima ni kipaji cha Roho Mtakatifu cha kutusaidia tupende na kufurahia mambo ya Mungu. Akili ni mwanga wa Roho Mtakatifu wa kutusaidia tumjue zaidi Mungu na ukamilifu wake pamoja na kuelewa ufunuo wake. Shauri ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotuelekeza kuchagua siku zote mambo yenye kufaa zaidi kwa sifa ya Mungu na kwa wokovu wetu. Nguvu ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotutia moyo wa kushika sana amri za Mungu na mambo ya utumishi wake tusiogope watu wala matukano wala mateso wala kufa. Elimu ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotutia maarifa ya mambo ya ulimwengu huu, kwa kutambua mapungufu yake pamoja na mitego, werevu na udanganyifu wa shetani akitujaribu mwenyewe au kwa kupitia vitu kama watu. Ibada ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotufanya tumpende Mungu kama Baba yetu mwema na watu wote kama ndugu; kwa msingi huo kutimiza utumishi wa Mungu na yote yale yenye kumpa Mungu sifa na heshima. Uchaji wa Mungu ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotutia hofu ya kumchukiza Mungu kwa dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumtia baba yake uchungu.
Ushuhuda wa Biblia
Ufunuo kuhusu vipaji vya Roho Mtakatifu unapatikana hasa katika dondoo la Isa 11:2 ambalo linamhusu kwanza Masiya, halafu kwa kumshiriki yeye linawahusu waadilifu wote ambao Yesu aliahidi kuwapelekea Roho Mtakatifu: “Roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana”. Kipaji cha ibada hakitajwi katika lugha asili ya Kiebrania, bali katika tafsiri za Septuaginta na Vulgata. Halafu, Isaya 11:3 kwa Kiyahudi inataja tena “kumcha Bwana”, ambapo katika Agano la Kale “kumcha Bwana” na “ibada” ni maneno mawili yenye maana karibu ileile. Hivyo kuanzia karne III mapokeo yanashika idadi ya vipaji saba.
Katika kitabu cha Hekima tunasoma: “Naliomba, nikapewa ufahamu; nalimwita Mungu, nikajiliwa na roho ya Hekima. Naliichagua kuliko fimbo za enzi na viti vya enzi, wala mali sikudhani kuwa ni kitu ikilinganishwa nayo; wala sikuifananisha na kito cha thamani, mradi dhahabu yote ya nchi ni kama mchanga kidogo mbele yake, na fedha itahesabiwa kama udongo. Naliipenda kupita afya njema na uzuri wa sura, hata zaidi ya nuru nikataka kuwa nayo, kwa maana mwangaza wake haufifii kamwe. Na pamoja nayo nikajiliwa na mema yote jamii… ingawa sijajua ya kama yeye ndiye aliyeyazaa… Maana yeye amekuwa hazina kwa wanadamu isiyowaishia; nao wale waitumiao hujipatia urafiki na Mungu… na tangu kizazi hata kizazi huwaingilia roho takatifu, huwafanya wanadamu kuwa rafiki za Mungu na manabii” (Hek 7:7-11,12,14,27).
Ufunuo wa Agano la Kale umetimilizwa na Mwokozi: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli… anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu… huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yoh 14:15-17,26). Mtume Yohane, akitaka kuwakinga waamini dhidi ya wazushi, akaongeza, “Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu… Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo” (1Yoh 2:20,27). Katika Maandiko yapo pia madondoo kuhusu kipaji kimojakimoja.
Ushuhuda wa mapokeo
Mababu wa Kanisa waliyafafanua mara nyingi maneno hayo na kutamka wazi kuwa vipaji saba vya Roho Mtakatifu vimo ndani ya waadilifu wote. “Hivyo vipaji vya Roho Mtakatifu kwetu ni kama chemchemi ya Kimungu tunapochota ujuzi hai wa amri za maisha ya Kikristo, na kwa njia yake tunaweza kujua pia kama Roho Mtakatifu anakaa ndani mwetu” (Katekisimu ya Mtaguso wa Trento). Ushuhuda muhimu wa Mapokeo kuhusu vipaji saba unapatikana katika liturujia ya Pentekoste: “Wape waamini wako, / wenye tumaini kwako, / paji zako zote saba” (sekwensya “Uje Roho Mtakatifu”). “Mtoa wa vipaji saba... / tia nuru akilini / na upendo mioyoni” (utenzi “Uje Roho Muumbaji”).
Ushuhuda huo ulielezwa vizuri na Papa Leo XIII, “Mwadilifu anayeishi kwa neema inayotia utakatifu na kutenda kwa njia ya maadili kama kwa vipawa mbalimbali, anahitaji kabisa vipaji saba, ambavyo vinaitwa kikamilifu zaidi vipaji vya Roho Mtakatifu. Kwa vipaji hivyo roho ya mtu inainuliwa na kuwezeshwa kutii kwa urahisi na mapema zaidi miangaza na misukumo ya Roho Mtakatifu. Vipaji hivyo vina nguvu kubwa hata kumwongoza mtu kwenye utakatifu mkuu; ni bora hivi hata kudumu mbinguni pia, ingawa kwa kiwango cha juu zaidi. Kwa njia yake roho inaongozwa na kuhimizwa kujipatia heri za Kiinjili, ambazo ni maua yanayochanua kwa wakati wake, dalili tangulizi za heri ya milele... Kwa kuwa vipaji ni vikubwa hivyo navyo vinaonyesha wema mkuu wa Roho Mtakatifu kwetu, vinatudai tumuonyeshe heshima na utiifu mkuu kabisa.
Tutafikia kwa urahisi hatua hiyo tukijitahidi zaidi na zaidi kumjua, kumpenda na kumuomba... Tunapaswa kumpenda Roho Mtakatifu kwa kuwa ni Mungu... tena kwa kuwa ni upendo wenyewe, asili, wa milele, kwa sababu hakuna kinachopendeza kuliko upendo... Yeye atatujalia kwa wingi zawadi zake za kimbingu, hasa kwa sababu utovu wa shukrani unafunga mikono ya mfadhili, lakini moyo wa shukrani unaifungua tena... Tunapaswa kumuomba mfululizo na kwa tumaini kubwa atuangaze zaidi na zaidi na kuwasha ndani mwetu moto wa upendo wake, ili kwa kutegemea imani na upendo tutembee kwa ari kuelekea tuzo la milele, kwa kuwa ndiye amana ya urithi wetu”.
Maelezo ya Thoma wa Akwino
Mwalimu wa Kanisa huyo alifundisha hasa matatu: 1° kwamba vipaji ni misimamo ya kudumu, lakini tofauti na maadili; 2° kwamba ni vya lazima kwa wokovu; 3° kwamba vinashikamana na upendo na kukua pamoja nao.
1° “Ili kutofautisha vipaji na maadili mbalimbali tunapaswa kufuata lugha ya Biblia inayoviita si vipaji bali roho” kusudi tuelewe kuwa vinapatikana ndani mwetu kwa uvuvio wa Mungu au msukumo kutoka juu wa Roho Mtakatifu. Ni lazima tuzingatie kwamba binadamu ana mambo mawili yanayomuongoza: moja limo ndani mwake, yaani akili, lingine liko nje, yaani Mungu. “Ni wazi kwamba chochote kinachosukumika kinatakiwa kulingana na lile linalokisukuma; na ukamilifu wake ni urahisi wa kusukumwa nalo. Basi, kadiri hilo lilivyo bora, ni lazima kinachosukumwa kiwe kikamilifu zaidi ili kupokea msukumo wake. Hatimaye ni wazi kwamba maadili ya kiutu yanamkamilisha mtu katika kujiongoza kwa akili yake katika maisha ya ndani na ya nje. Basi unahitajika ndani mwake ukamilifu wa juu ambao umuandae kusukumwa Kimungu, na namna hizo kamilifu zinaitwa vipaji si tu kwa kuwa tunamiminiwa na Mungu, bali pia kwa sababu kwa njia yake mtu anawezeshwa kupokea mara uvuvio wa Kimungu, alivyosema Isaya (50:5): ‘Bwana Mungu amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma’. Ndiyo sababu wengine wanasema vipaji vinamkamilisha binadamu vikimuandaa kutenda mambo bora kuliko ya maadili”.
Hapo tunaona kuwa vipaji vya Roho Mtakatifu si matendo wala si misukumo au misaada ya kupita ya neema, bali ni misimamo ya kudumu tunayomiminiwa, inayotuweka tayari kupokea uvuvio wa Mungu, kama vile tanga zinavyowezesha chombo kwenda kwa nguvu ya upepo. Kwa utayari huo wa kupokea misukumo vinatusaidia kutenda mambo yale bora ambayo ukamilifu wake unaonyesha kwamba yanategemea vipaji kuliko maadili.
Mfano huo ulitolewa na Yesu Kristo mwenyewe aliposema, “Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” (Yoh 3:8). Hatujui vizuri upepo unaovuma umetokea wapi na utasikika mpaka wapi; vilevile hatujui vizuri uvuvio wa Kimungu unaanzia wapi, na utatufikishia ngazi gani ya ukamilifu tukiufuata kwa uaminifu. Tusiwe kama wanamaji wazembe wasiotweka tanga wakati wa kufaa.
Vipaji vinatofautiana na maadili kama wanavyotofautiana wanaoviongoza, yaani Roho Mtakatifu na akili iliyoangazwa na imani; hiyo ni miongozo na kanuni tofauti. Utendaji wa kibinadamu unafuata kanuni ya kibinadamu, utendaji upitao maumbile unafuata kanuni ya Kimungu, yaani uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hata busara iliyoinuliwa na upendo inatenda kwa kuzingatia mifuatano ya mawazo, tofauti na kipaji cha shauri kinachotuandaa kupokea uvuvio maalumu usioihitaji. Kwa mfano, tukiuliziwa siri fulani, busara inasita kuona namna ya kutunza siri hiyo bila ya kusema uongo, kumbe uvuvio wa Roho Mtakatifu unaondolea wasiwasi (taz. Math 10:19). Vilevile, imani inaambatana tu na kweli tulizofunuliwa, kumbe kipaji cha akili kinatuwezesha kuona vilindi vya kweli hizo, na kile cha hekima kinatuwezesha kuonja utamu wake.
2° Vipaji vya Roho Mtakatifu ni vya lazima kwa wokovu wa milele. “Maana Mungu humpenda yeye tu akaaye na Hekima” (Hek 7:28). “Miongoni mwa ndugu awatawalaye ana heshima, bali machoni pa Bwana ni wao wamchao” (YbS 10:20). Sasa kipaji bora ni hekima, na cha mwisho ni uchaji wa Mungu.
Maadili ya Kimungu yanajilinganisha na namna ya kibinadamu ya akili na utashi wetu, na hivyo yanatuacha katika hali isiyotosha kwa lengo letu kuu lipitalo maumbile, ambalo tunahitaji kulijua kwa namna hai, ya kuchimba na kuonja, na ambalo tunatakiwa kulilenga kwa ari zaidi. Imani hata ikiwa kubwa inaendelea kuwa na upungufu kwa sababu tatu za msingi: 1) yale inayoyaamini ni giza kwake, haiyaoni moja kwa moja, ila “kwa kioo kwa jinsi ya fumbo” (1Kor 13:12); 2) inayafikia kwa njia ya matamko mbalimbali ya Kanisa, kumbe Mungu ni sahili kabisa; 3) inayafikia kinadharia, kwa kukiri au kukanusha maneno fulanifulani, kumbe Mungu aliye hai anatakiwa kujulikana kama kwa mang'amuzi. Tumaini linashiriki upungufu wa imani, na vilevile upendo, kwa kuwa imani ndiyo inayoupatia la kupenda. Zaidi tena busara ina upungufu, kwa kuwa inahitaji kufuata mawazo, kutafuta sababu za kutenda, ili kuelekeza maadili ya kiutu; mara nyingi inasita isijue la kufanya, ikihitaji mwanga kutoka juu, k.mf. ili kushinda vishawishi visivyotambulikana au vikali na vya muda mrefu.
“Akili ya binadamu, hata baada ya kukamilishwa na maadili ya Kimungu, haiwezi kujua yale yote inayohitaji kuyajua, wala haiwezi kuepuka kila upotovu. Mungu tu aliye na ujuzi wote na enzi zote anaweza kufidia ujinga na upumbavu, ugumu wa moyo na kasoro nyinginezo tulizo nazo. Ili kutuondolea kasoro hizo tumejaliwa vipaji vya Roho Mtakatifu, vinavyotuwezesha kupokea vizuri uvuvio wa Kimungu... Kwa njia ya maadili ya Kimungu na ya kiutu, binadamu hajakamilika kuhusu lengo lake kuu linalopita maumbile asihitaji daima kusukumwa na Roho Mtakatifu kutoka juu”. Haja hiyo ni ya kudumu, ndiyo sababu vipaji ni misimamo ya kudumu tunayomiminiwa.
Sisi tunatumia vipaji kwa mfano wa utiifu, ili kupokea na kutekeleza vizuri agizo kutoka juu, lakini hatuwezi kuwa na uvuvio huo kila tunapotaka. Upande huo vipaji vinatufanya tusitende wenyewe, bali kwa Roho Mtakatifu. Hivyo ni wazi kuwa vipaji, kama vile utiifu, ni misimamo ya kudumu ya mwadilifu.
3° Kwa kuwa vipaji ni vya lazima kwa wokovu, vinashikamana na upendo. Roho Mtakatifu haji ndani mwetu pasipo vipaji vyake, ambavyo vinaendana na upendo na kupotezwa pamoja nao kwa dhambi yoyote ya [[mauti]. Basi, vipaji ni sehemu ya muundo wa Kiroho wa neema inayotia utakatifu, ambayo kwa sababu hiyo inaitwa “neema ya maadili na vipaji”. Kama vile maadili ya kumiminiwa yanavyokua pamoja kwa mfano wa vidole vya mkono, vipaji pia vinakua pamoja. Hakuna mwenye kiwango kikubwa cha upendo wa Mungu, inavyotakiwa na ukamilifu, asiye na vipaji vya Roho Mtakatifu kwa kiwango hichohicho.
Huo muundo wa Kiroho, ambao ni chanzo cha uzima wa milele, una thamani kubwa kuliko ile ya macho, ya afya na ya akili kwa maana mwadilifu akipotewa navyo hapotewi na hazina hiyo ambayo kifo chenyewe hakiwezi kumnyang'anya. Ni thamani kubwa kuliko ile ya karama (kufanya miujiza n.k.) kwa kuwa hizo ni alama za nje tu ambazo zinaweza kuelekeza njia ya kumfikia Mungu, lakini haziwezi kutuunganisha naye inavyofanya neema ya utakaso.
Kusudi tujue kweli muundo wa Kiroho unaotuwezesha kuishi kama wana wa Mungu, haitoshi tuyajue maadili. Ni lazima tuzingatie pia vipaji vya Roho Mtakatifu, pasipo kusahau namna mbalimbali za kupata msaada wa Mungu.
Orodha ya vipaji ya Roho Mtakatifu kuanzia juu:
- 1. hekima
- 2. akili (kipaji)
- 3. shauri (kipaji)
- 4. nguvu (kipaji)
- 5. elimu (kipaji)
- 6. ibada (kipaji)
- 7. uchaji wa Mungu.

Thursday, May 29, 2014
SHEREHE YA KUPAA BWANA MWAKA "A" masomo dominika 01/06/2014 jumapili
01
|
JUNI
SHEREHE YA KUPAA BWANA MWAKA "A"
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI TETA.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI
ZAB:47:1-2,5-6,7-8
SOMO LA 1: Mdo. 1:1-11
Kitabu kile cha kwanza naliandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha, hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale Mitume aliowachagua; wale alowadhihirisha mafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyohusu ufalme wa Mungu. Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohane alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. basi walipokutanika , wakamuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufamle? Akawaambia, si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, ikiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa Nchi. Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkatazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hivyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Somo 2:Efe.1:17-23
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu awape ninyi Roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; aliotenda katka kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufamle wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajalwo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
INJILI:Mt. 28:16-20
Wale wanafunzi kumi na moja walikwenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari.
Matangazo mbali mbali
Jumapili
hii tarehe 01/06/14 kutakuwa na kikao cha vijana wote wanaoshiriki ziara ya uinjilishaji parokia za Dareda, Sanu, Daudu na endabashi, kikao kitafanyikia parokiani Saa 4:00 asubuhi mara baada ya ibada ya pili.
zaidi......jdhibitisha ushiriki wako kwenye ziara ya Dareda 01-07/07/14 kwa kulipa ada ya ushiriki sasa ni tshng 150000 lipa kwa mhazini wako jumuiya, kigango au parokia.....tunawatakia maandalizi mema.
Monday, May 26, 2014
Ziara ya Baba Mtakatifu Francisco Israel
Hotuba ya Papa kwa Mufti Mkuu wa Jeresalemu
Jumatatu Baba Mtakatifu Francisiko, aliifungua ratiba yake ya Hija katika nchi Takatifu kwa kukutana na Mufti Mkuu wa Jeresalem , katika Msikiti Mkuu wa Jerusalem.
Na katika nyayo za watangulizi wake, na hasa katika mwanga wa Paul VI , aliyefanya hija hii miaka hamsini iliyopita, na hivyo kuwa Papa wa kwanza kutembelea Nchi Takatifu ,pia alitamani sana kufanya hija hii ya kutembelea maeneo ambayo yamemshuhudia Yesu akiyaishi maisha haya ya kidunia. Na kwamba hija yake isingekuwa kamili bila ya kukutana na kutafakari pamoja na watu wanao ishi katika nchi hii. Na hivyo kwa heshima na taadhima ameweza kukutana na Mufti Mkuu wa Jerusalem , na Waislamu wengine , wake kwa waume.
Hotuba ya Papa ilielekeza mawazo kwa Ibrahimu , ambaye aliishi kama Mhujaji wa imani katika nchi hiI ambayo Waislamu, Wakristo na Wayahudi wanamtabua Ibrahimu kuwa Baba yao wa Imani, ingawa kila mmoja, humwabudu Mungu Mmoja katika njia tofaut. Ibarahim ni mfano mkubwa sana wa jinsi ya kumfuata Mungu kwa imani kuu.
Papa amewatia moyo waamini wote kwamba, katika Hija hii ya kidunia, hatuko peke yetu. Kwa Wakristo, kwa njia ya msalaba, huungana na waamini wa dini nyingine , kushiriki na kutembea pamoja na hata kuishi pamoja kama sehemu njia ya kutimiza mapenzi ya Mungu. Papa alitoa shukurani zake za dhati kwa wote walio wezesha mkutano huo na kwa ukarimu wao ulioonyesha kwamba , hija ya maisha, ni yetu sote binadamu . .
Papa aliomba uwepo wa mawasiliano ya kidugu na kubadilishana mawazo , kama hatua yenye kutoa mwanya wa chaguzi na nguvu mpya, katika kukabiliana na changamoto katika maisha ya kawaida, na wao kama viongozi waweze kuwa msitari wa mbele likabiliana na changamoto kwanza.
Alisema, hawawezi kusahau ,ukweli kwamba Hija ya Ibrahimu, pia ilikuwa ni wito kwa uadilifu : Mungu alimtaka aishuhudie imani yake kimatendo. Na hivyo , pia wao, kama viongozi, wangependa kuwa mashahidi wa utendaji wa Mungu katika dunia yetu. Aliomba kukutana kwao kutia shime vuguvugu la ndani la kusambaza wito huu na katika kuwa mawakala wa amani na haki” . Papa aliwasihi katika zawadi ya sala pia kujifunza kuwa na huruma kuu, kumheshimu kila mmoja na kupendana kama kaka na dada ! Pia kujifunza kuelewa maumivu mwingine !
Na jina la Mungu lisitumiwe kama chombo cha kuhalisha vurugu na maonevu, balijina hilo liwe kichocheo cha utendaji wa pamoja kwa ajili ya kujenga haki na amani!
Aidha Baba Mtakatifu , majira ya asubuhi, alikutana na Rabbi Wakuu wawili wa Israel, na pia alitembelea Makao makuu ya Rais wa Israel.
Baba Mtakatifu majira ya jioni kabla ya kuongoza Ibada ya Misa itakayokamilisha Hija yake katika nchi Takatifu , anakutana na Mapadre watawa na waseminaristi katika Kanisa la Getsemani.
Tuesday, May 6, 2014
Dominika ya 4 ya pasaka mwaka “A”. tarehe 11/05/2014
JUMAPILI DOMINIKA YA 4 ya Pasaka ya Mwaka A.
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA MH. ISIDORI BAKANJA- BOKO.
MISA YA KWANZA 12:15-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. FRANCIS WA ASIZ-MBWENI
MISA YA KWANZA SAA 1:10-3:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 3:00-4:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
SAA 1:00-3:00 ASUBUHI.
MISA YA PILI SAA 3:00-5:00
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA-MBWENI TETA
MISA NI SAA 3:00-5:00.

SOMO 1. Mdo.2:14a, 36 – 41
Siku
ya Pentekoste Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake,
akawaambia, basi nyumba yote ya Israel na wajue yakini ya kwamba Mungu
amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo. Walipoyasikia haya
wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na Mitume wengine, Tutendeje, ndugu
zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo,
mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwa
ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali,
na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno
mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.
Nao waliolipokea neon lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka wata wapata
elfu tatu.
WIMBO WA KATIKATI; Zab.
23:1-6
(Kitikio)
Bwana
ndiye mchungaji wangu sitopungukiwa na kitu au Aleluya
SOMO 2: 1Pet. 2:20b – 25
Kustahimili,
mtendapo mema na kupata mateso, huu ndiyo wema hasa mbele za Mungu. Kwa sababu
ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia
kielelezo, mfuate nyanyo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana
kinywani mwake. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogopa;
bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. Yeye mwenyewe alizichukua
dhambi zetu katika mwili wake juu yam ti; ili, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi,
tuwe hai kwa mambo ya haki; na kupigwa kwake mliponywa. Kwa maana mlikuwa
mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi
wa
roho zenu.
SHANGILIO. Yn. 10:14
Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu
nawajua; nao walio wangu wanijua mimi
Aleluya
INJILI.:Yn. 10:1-10
Yesu
aliwaambia Wayahudi, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika
zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwizi naye ni mnyang’anyi. Aingiaye
mlangoni ni mchungaji wa kondoo. Bawabu humfungilia huyo, na kondoo humsikia
sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na huwapeleka nje. Naye awatoapo
nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua
sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui
sauti za wageni. Mithali hiyo Yesu aliwaambia; lakini wao hawakuelewa na mambo
hayo aliyowaambia. Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi
ndimi mlango wa kondoo. Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini
kondoo hawakuwasikia. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka;
ataingia na kutoka, naye atapata malisho. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;
mimi nalikuja ili wawe na uzima, kasha wawe nao tele.
Mdo - kitabu
cha Matendo ya Mitume
1Pet - kitabu
cha waraka wa kwanza wa mtu Petro kwa
watu wote
Yn - kitabu cha muinjili Yohana.
Na Abel Reginald……………….niwatikieni
maandalizi mema ya Dominika
usikose kuhudhuria kwenye kikao cha Halmashauri ya VIWAWA Parokia ya Boko mara baada ya Misa ya kwanza Kigangoni Rafael
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...