Katika ulimwengu, mahusiano ya karibu ya kimwili kabla na nje ya ndoa
yanakubalika, na hata kushabikiwa. Vipindi vya uchumba vinahesabika
kama nyakati za wahusika hao wawili kuona kama ‘wanafaana’. Hili mara
nyingi linawapelekea katika kuwa na mahusiano ya karibu ya kimwili.
Inasikitisha kwamba katika makanisa mengi vijana wanauiga mtindo huu
huu, na wale walio katika nafasi za mamlaka – uongozi wa kanisa, wazazi,
nk., hawashughuliki na hili suala
kwaumakiniunaohitajika.Vijanawanaachiwa kujiamulia wenyewe mipaka katika
hili suala nyeti, badala ya kupewa miongozo ya Kibiblia iliyo wazi.
Hebu tuwe wazi tokea mwanzo ya kwamba Mungu hachanganyikani; Neno
lake halijaficha jambo. Ndani mwake, tunaona maono na mpango wake
vilivyo dhahiri, kwa watu wake na Kanisa lake. Ni wazi kwamba hataki
tujichanganye na ulimwengu na njia zake. Na wala Mungu hataki sheria na
kuhukumiana Kanisani mwake, ambavyo havina nguvu yoyote ya kumbadilisha
mtu. Anachotaka ni Wakristo wote wahakikishwe na Roho Mtakatifu kuhusu
dhambi kupitia Injili ya Yesu Kristo ambayo inaweka mpaka ulio wazi na
kutuonyesha tunapaswa tusimame juu ya msingi upi. Hii ndiyo maana
ninaamini tunapaswa kurejea kwenye msingi – Neno la Mungu – ili tuone
anasemaje juu ya hili suala.
MIILI YETU NI VIUNGO VYA KRISTO
Hebu tuangalie Mungu anavyoiona ndoa na mahusiano nje ya ndoa, na
tutaona ya kwamba uhusiano wowote wa kimwili nje ya ndoa, uwe wa aina yo
yote ile, unahesabika kuwa ni dhambi machoni pa Mungu. Si suala la
‘Tuweke wapi mipaka?’ kwa sababu tukijaribu kuweka mipaka ya aina
yoyote, tutaivuka tu. Ni kama lile tangazo la breki za magari lisemavyo,
“Usianzishe jambo ambalo hutaweza kulizuilia!”
1 Wakorintho 6:15 inasema: “Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!” Kwa hivyo, si roho zetu tu zilizounganika na Kristo; nafsi yetu yote ni mmoja naye. Mistari ya 16 – 17 inasema, “Au
hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana
asema, ‘Wale wawili watakuwamwilimmoja.’Lakiniyeyealiyeungwa na Bwana ni
roho moja naye.”
Paulo hapa anasema waziwazi ya kwamba ni lile tendo la ndoa
linalowaunga watu kuwa mwili mmoja, na hili linapaswa kuchukuliwa kwa
uzito. Katu hatupaswi kusahau ya kuwa roho zetu, nafsi zetu na miili
yetu imeungwa pamoja na Kristo. Siku hizi Wakristo wengi wanafanya
wanavyopenda na miili yao, pasipo kutambua madhara ya rohoni
yanayotokana na matendo yao. Kwenye kifungu hiki Paulo anaweka utofauti
kati ya dhambi ya mwili na dhambi nyingine; katika zinaa unatenda dhambi
dhidi ya mwili wako kwa sababu unafanyika kuwa mmoja na yule
mnayeunganika naye kimwili. Uzinzi ni uhusiano wowote wa kimwili nje ya
ndoa. Uongo, wizi, hasira, nk. ni tofauti; haya ni matunda ya tamaa zetu
za kimwili.
Ikiwa Mungu aliamua kuweka utofauti kati ya dhambi katika miili yetu
na dhambi nyingine, tunapaswa kuwa makini sana, na kuufahamu moyo wake
katika hili suala. Msitari wa 18 unasema, “Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.”
Hatupaswi kusahau ya kuwa miili yetu pamoja na roho zetu vimeungwa na
Kristo, na tunapotenda zinaa ni jambo zito sana machoni pa Mungu.
Mistari ya 19-20 inatukumbusha ya kuwa mwili wetu ni hekalu la Roho
Mtakatifu, na tunahimizwa, “mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
MWILI UNAPASWA KUSULUBIWA
Katika Wagalatia 5:24-25, Paulo anasema, “Na hao walio wa Kristo
wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.” Kila Mkristo ana uelewa
fulani wa maana ya haya Maandiko. Lakini kwa wale wanaotamani kutembea
rohoni, na wako tayari kuoa au kuolewa, yana maana zaidi maishani mwao.
Tumeitwa kuisulubisha miili yetu na tamaa zake. Hii ndio maana
tunahitajika kuusikia ujumbe wa Msalaba kila wakati kwa sababu
unatukumbusha kujikana nafsi zetu na kuyapoteza maisha. Hakuna nafasi ya
kudanganyana, wala kujaribisha mambo… Sisi ni watu waliochaguliwa ambao
miili yetu ni mali ya Bwana Yesu Kristo.
Iweje, basi, tuwaze ya kuwa ni sahihi kwa watu wawili waliochumbiana
rasmi au vinginevyo, kufanya mambo wanayoruhusiwa kufanya tu mume na
mke, eti kwa kuwa wamefikia uamuzi wa kuwa wenza? Uamuzi wa watu wawili
wa kuoana huko mbeleni unapaswa umaanishe ya kwamba wataheshiminiana kwa
utimilifu mbele za Bwana. Hadi siku ya kuoana, Bwana anawataka waishi
maisha safi na matakatifu.
Vijana, sikilizeni… isipokuwa una uhakika moyoni mwako ya kuwa
uhusiano umeanzishwa na Mungu, usithubutu kuuingia. Ukitaka kuufahamu
mpango wake, na mtu aliyekuandalia kuwa mwenzi wako, fahamu ya kuwa
atakufunulia.
Mkishafahamu ya kuwa ni mpango wa Mungu muoane, na ikiwa mnafahamu
maisha ya utakatifu mnayopaswa kuishi kabla ya harusi, hakuna hatari.
Mnaweza mkachumbiana na kutiana moyo katika kuheshimiana, kwa sababu
mmehakikishiwa mioyoni mwenu ya kuwa mnapaswa kuishi maisha matakatifu
mbele za Bwana hadi mtakapooana. Utakuwa na kicho kitakatifu cha uwepo
wa Mungu katika maisha ya mwenzi wako na kufanyika kielelezo kwa
wengine.
Ndio maana unapaswa uthibitike katika kile Mungu anachosema, ili
pasiwepo na kubahatisha. Je, kuna mahusiano ya aina yoyote ya kimwili
kabla ya ndoa yanayokubalika? Hasha! Neno la Mungu liko wazi sana juu ya
hili suala.
MANUKATO YA UHUSIANO SAFI NA MTAKATIFU
Labda tayari uko katika uhusiano wa kimwili nje au kabla ya ndoa, na
Bwana anakunenea ya kwamba si sahihi. Ushauri wangu ni kwamba utubu na
ufanye uamuzi imara wa kuacha mahusiano yote ya kimwili mara moja; na
usigeuke nyuma. Si jambo ambalo linafanyika hatua kwa hatua, wala si
jambo la kuchukulia kwa wepesi. Neema ya Mungu ipo kukusaidia. Na ikiwa
ninyi wawili mnafahamu mioyoni mwenu ya kuwa mmeandaliwa kuoana, basi
jitunzeni hadi siku hiyo, mheshimiane kama vile ndugu wa kiume
anavyomheshimu ndugu wa kike kanisani, na katika kufanya hivyo muishi
maisha matakatifu na safi. Injili ya Msalaba wa Yesu Kristo inaleta
jawabu kwa, na kuchora msitari ulio wazi katika kila jambo
tunalokabiliana nalo maishani mwetu. Inatusaidia kuenenda katika
uhakikisho, na kwa maana hiyo tunatembea katika ushindi. Wakristo wa
kila rika, walio kwenye ndoa na ambao wako bado, wanahitajika wasikilize
kwa umakini kile Mungu anachosema katika Neno lake ili waweze kuishi
maisha matakatifu na kufanyika vielelezo kwa wengine. Je! si ni jambo la
utukufu moyo wako unapokushuhudia ya kuwa kuna hali ya usafi katika
uhusiano wa ndugu wanaotaraji kufunga ndoa? Hili linaleta harufu nzuri
ya manukato inayopendeza. Je, ni ushuhuda wa jinsi gani wa nguvu ya
Injili watu wawili wanapooana juu ya huu msingi!
Ninaamini huu ndio mpango wa Mungu kwa Kanisa lake na kwa watoto wake. Hakuna haja ya kukata tamaa. Mungu yu hai; anaweza kuleta watu wawili pamoja. Anajua ya mbeleni. Anajua kila kitu kuhusu maisha yetu, na shauku yake ni sisi tuishi maisha safi na matakatifu. Ndio maana ni heri kusubiri, kuliko kujaribisha mambo. Fungua moyo wako; mwache Mungu azungumze na wewe na akushawishi. Kwa Yesu Kristo hakuna kuchelewa. Leo inaweza ikawa siku yako ya kumtangazia Bwana ya kuwa unaenda kuishi maisha yako ya Ukristo kabla ya ndoa kwa kulifuata Neno lake.
Wednesday, September 17, 2014
Tuesday, September 9, 2014
Masista watatu wauawa Burundi
Baba
Mtakatifu Francisko, amepeleka salaam zake za rambirambi kwa familia za
Masista watatu wanashirika la Mtakatifu Xavery, waliouawa katika
nyumba yao ya Kamenge, Kaskazini mwa mji wa Bujumbura siku ya Jumapili.
Majina ya Marehemu Masista ni Sista Olga Raschietti, Sista Luchia
Pulici na Sr Bernadetta Boggian. Wote wanatajwa kuwa raia wa Italia.
Rambirambi za Papa zimetumwa kwa Mjumbe wake wa Kitume nchini Burundi, Askofu Mkuu Evariste Ngoyagoye na nyingine kwa Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Xavery, akionyesha kusikitishwa sana na kilichotokea kwa Masista hao. Papa anatumaini damu hii ya watu wa Mungu iliyomwangika bure, itaweza kuwa mbegu ya matumaini katika ujenzi wa udugu wa kweli kati ya jamii ya watu wa Burundi. Na ameahidi kuwakumbuka katika sala zake mashahidi hawa wa Injili , na ukaribu wake kwa shirika, na jumuiya ya waamini nchini Burundi.
Mkuu wa Shirika la Watawa Xaverian nchini Burundi, Padre Mario Pulcini, akithibitisha uwepo wa tukio, ameonyesha hisia kwamba ni tukio la wizi. Na kwamba, Sista Lucia na Sista Olga, waliuawa Jumapili mchana wakati Sista Bernadetta, alikwenda kupokea Masista wengine waliowasili katika uwanja wa ndege tokea Italia.
Wakati aliporejea nyumbani alikutana na hali ya ukimya uliompa wasiwasi na baadaye akiwa na Padre Mario waliona wenzao tayari walikuwa wameuawa ndani ya nyumba yao. Na Sista Bernadetta ameuawa usiku wa kuamkia Jumatatu akiwa katika chumba chake.
Askofu Henry, Jimbo la Parma Italia, kwa niaba ya Kanisa lote la Parma, amepeleka pia niaba ya waamini wa Parma , salaam zake za rambirambi kwa Usharika wa Missionari Xaverians, wakiwafariji kwa sala ya imani kwa Bwana wa Maisha. Askofu pia ametoa ombi kwa Wakristo wa Jimbo la Parma na kwa wote wenye mapenzi mema, kuwakumbuka Masista hawa katika sala zao.
Rambirambi za Papa zimetumwa kwa Mjumbe wake wa Kitume nchini Burundi, Askofu Mkuu Evariste Ngoyagoye na nyingine kwa Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Xavery, akionyesha kusikitishwa sana na kilichotokea kwa Masista hao. Papa anatumaini damu hii ya watu wa Mungu iliyomwangika bure, itaweza kuwa mbegu ya matumaini katika ujenzi wa udugu wa kweli kati ya jamii ya watu wa Burundi. Na ameahidi kuwakumbuka katika sala zake mashahidi hawa wa Injili , na ukaribu wake kwa shirika, na jumuiya ya waamini nchini Burundi.
Mkuu wa Shirika la Watawa Xaverian nchini Burundi, Padre Mario Pulcini, akithibitisha uwepo wa tukio, ameonyesha hisia kwamba ni tukio la wizi. Na kwamba, Sista Lucia na Sista Olga, waliuawa Jumapili mchana wakati Sista Bernadetta, alikwenda kupokea Masista wengine waliowasili katika uwanja wa ndege tokea Italia.
Wakati aliporejea nyumbani alikutana na hali ya ukimya uliompa wasiwasi na baadaye akiwa na Padre Mario waliona wenzao tayari walikuwa wameuawa ndani ya nyumba yao. Na Sista Bernadetta ameuawa usiku wa kuamkia Jumatatu akiwa katika chumba chake.
Askofu Henry, Jimbo la Parma Italia, kwa niaba ya Kanisa lote la Parma, amepeleka pia niaba ya waamini wa Parma , salaam zake za rambirambi kwa Usharika wa Missionari Xaverians, wakiwafariji kwa sala ya imani kwa Bwana wa Maisha. Askofu pia ametoa ombi kwa Wakristo wa Jimbo la Parma na kwa wote wenye mapenzi mema, kuwakumbuka Masista hawa katika sala zao.
Thursday, August 28, 2014
Wednesday, August 27, 2014
Nembo ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016
Heri
wenye rehema maana hao watapata rehema, ndiyo kauli mbiu itakayoongoza
maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itakayofanyika
Jimbo kuu la Cracovia, Poland. Kamati kuu ya maandalizi imechapisha
nembo itakayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani
ambayo Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuhudhuria na kushiriki
kikamilifu.
Nembo ina rangi kuu tatu: Bluu, Nyekundu na Njano; inaonesha ramani ya Poland na ndani yake kuna Msalaba inayomwonesha Yesu Kristo, kiini cha mkutano huu. Nembo hii inawaalika vijana kujiaminisha mikononi mwa Mungu, utekelezaji wa maneno ya Mtakatifu Faustina Kowalska aliyeeneza Ibada ya Huruma ya Mungu.
Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 26 hadi Julai 2014. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuwasili nchini Poland hapo tarehe 28 Julai 2016.
Nembo ina rangi kuu tatu: Bluu, Nyekundu na Njano; inaonesha ramani ya Poland na ndani yake kuna Msalaba inayomwonesha Yesu Kristo, kiini cha mkutano huu. Nembo hii inawaalika vijana kujiaminisha mikononi mwa Mungu, utekelezaji wa maneno ya Mtakatifu Faustina Kowalska aliyeeneza Ibada ya Huruma ya Mungu.
Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 26 hadi Julai 2014. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuwasili nchini Poland hapo tarehe 28 Julai 2016.
Kambumbu kuchezwa kwa ajili ya kueneza Ujumbe wa amani duniani
Septemba
Mosi katika viwanja vya Olympic vya mjini Roma, kutafanyika mashindano
ya mpira wa miguu kati ya timu mbili za kidini kwa heshima ya Papa
Francisco, kwa ajili ya kutoa ujumbe wa nguvu wa amani duniani. Ni
mpango uliowasilishwa siku ya Jumanne kwa wanahabari katika ukumbi wa
Makao Makuu ya Redio Vatican. Kati ya walio shiriki katika mkutano huo
ni Msgr. Guillermo Karcher, afisa katika Sekretarieti ya Vatican kwa
ajili ya khafla za Kipapa , mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu Javier
Zanetti, wakiwepo pia wachezaji kutoka timu ya Lazio, Cristian
Ledesma,na Juan Iturbe wa timu ya Roma.
Mchezo huu utakao
fanyika katika uwanja wa Olympic Roma, Mosi Septemba 20:45, si mechi
za kipinzani bali ni mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kutoa ujumbe wa
amani, na washiriki wa mechi hii wanatoka mataifa mbalimbali na watu wa
imani mbalimbali . Sehemu ya mapato yake yatatengwa kwa ajili ya
kufanikisha miradi ya Papa kwa ajili ya elimu na ustawi wa maisha kwa
watu maskini mradi unaofanikishwa na kuendelezwa na taasisi ya
"Scholas Occurentes" ambayo ni taasisi ya elimu, mkono wa Papa
Francisko katika utoaji wa misaada na chama cha "Pupi" kilicho anzishwa
na aliyekuwa Argentina mchezaji wa mpira wa miguu Javier Zanetti na mke
wake Paula, kwa ajili udumishaji juhudi za kutoa msaada katika mradi
unaoitwa "maisha mbadala". Kwa ajili hii, pia unaalikwa kutoa msaada
wako katika juhudi hizi kwa kutuma ujumbe wa SMS namba 45593.
Katika
mkutano wa waandishi wa habari, Msgr. Guillermo Javier Karcher,
aliwasilisha rasmi salaam za Papa Francisko, ambamo alitoa shukurani
zake za dhati kwa mpango huo uliandaliwa kwa ajili ya amani, kama
alivyowahi kupendekeza siku za nyuma, uwepo wa mechi ya kirafiki kati ya
wachezaji kutoka kila timu na wa dini zote na madhehebu yote
Kikristo.Taasisi ya “Scholas Ocurrentes”, ililichukua kwa makini
pendekezo hilo na kuandaa mechi hii na pia ina lenga kujenga mtandao
kwa ajili ya kubadilishana miradi na maadili elimu kwa ajili ya
kuendeleza utamaduni wa mijadala na utamaduni wa amani. Katika mtazamo
huo, Papa Francisko alipendekeza kwamba kabla ya kila mchezo, kila timu
ipande mti wa mzeituni, kama ishara ya amani , kama ilivyo fanyika
katika maadhimisho ya mwaka Mtakatifu 2000, yeye akiwa Askofu Mkuu wa
Buenos Aires, alipanda mti katika uwanja wa Plaza de Mayo , akiwa na
wanafunzi elfu saba kutoka shule za Kiserikali bila ya utengano wa
kidini.
Waandaaji wa tukio hili wanatumaini, mchezo huu wa kwanza
wa madhehebu,utaweza kuwa hatua ya mwanzo katika juhudi za kueneza
ujumbe wa amani kwa njia ya michezo, kama Papa Francisco alivyo
pendekeza. Michezo pamoja na kuwa ni uwanja wa upinzani kati ya timu
mbili zinazocheza, lakini ni tukio ambalo daima hufanyika katika hali ya
amani na utulivu, kuburudisha na kufurahisha mioyo ya watu. Na hivyo
unakuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na vyama vya kisiasa , kwamba licha ya
kuwa na maoni tofauti katika utendaji lakini katika utofauti huo,
unakuwa ni nafasi ya kujenga mazuri kwa ajili ya ustawi wa jamii. Na
kuwa mchezaji wa mpira au mwana riadha hakumwondolei mtu imani yake.
Imani ni suala linalo ambatana na mtu katika maisha yake yote. Na
ndivyo licha ya watu kuwa na imani mbalimbali, wanapaswa kuchanganyika
na kucheza pamoja kwa amani na utulivu kama ilivyo timu za mpira katika
mechi, hucheza kwa ajili ya manufaa ya wote.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...