Mkufunzi wa Semina ya Utawala Bora na Ujasiriamali, Ndugu Dniho alisema juzi kwenye ufunguzi wa semina kuwa; vijana ni
tumaini la Kanisa na Jamii kwa ujumla.
Jambo
la kusikitisha ni kuona kwamba, kuna kundi kubwa la vijana
wanaokimbilia mijini kutafuta riziki ya maisha, lakini mazingira
wanamoishi ni hatari na ya kukatisha tamaa kiasi kwamba, vijana wanakosa
dira na mwelekeo katika maisha.
Majiundo na malezi makini ni
muhimu sana kwa vijana, ili kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu
katika ustawi na maendeleo ya Jamii zao. Elimu ni ufunguo wa maendeleo
na matumaini kwa vijana, lakini kuna haja ya kuwezeka na kuboresha zaidi
mfumo wa elimu nchini Tanzania ili vijana waweze kuelimishwa barabara,
kwani wao ni matumaini ya leo na kesho iliyo bora zaidi.
Shule
za kata au sekondari zisiwe ni "mazizi" ya kuwakusanyia wanafunzi, bali
mahali maalum pa vijana kuweza kupata: ujuzi, maarifa, maadili na utu
wema. Hii ni changamoto kwa wadau mbali mbali wa elimu nchini Tanzania,
kuhakikisha kwamba, wanafanya maboresho makubwa katika mfumo wa elimu,
kwani matokeo ya mitihani ya hivi karibuni ni aibu kubwa kwa taifa
linalotaka kuwekeza kwa vijana.
Walimu wanapaswa kutambua dhamana na
wajibu wao katika malezi na makuzi ya vijana wanapokuwa shuleni.
Watambue kwamba, wana mchango mkubwa katika utoaji wa majiundo makini
kwa vijana wa kizazi kipya. .
Ndugu Dniho, anasema
kwamba, watanzania wengi ni watu wa kawaida kumbe, hawana uwezo wa
kuwapeleka watoto wao katika shule za binafsi. Vijana popote pale walipo
wahakikishiwe kwamba, wanapata elimu bora na wala si bora elimu ili
kuweza kupambana na mazingira pamoja na changamoto za maisha kwa siku za
usoni. Hii inatokana na ukweli kwamba, elimu ndiye mkombozi wa maskini!
Katika
Maadhimisho ya Mwaka wa Familia, Mama Kanisa anaendelea kukazia umuhimu
wa malezi bora kwa vijana katika Familia , ili
waweze kuja kuwa na Familia bora zenye misingi ya Imani ya Kristo na Kanisa lake. Mikakati
ya malezi ya vijana ipewe msukumo wa pekee katika ngazi mbali mbali za
maisha na utume wa Kanisa.
Vijana wakifundwa barabara na kuwa ni
Wakristo wema, hapana shaka kwamba, watakuwa pia ni raia wema
watakaojenga na kuimarisha misingi bora ya kifamilia, hapa familia
zitakuwa ni viota vya miito mbali mbali ndani ya Kanisa. Malezi bora na
makini ni ujenzi wa Jamii bora kwa sasa na kwa siku za usoni.
Ndugu Dniho, anasema, vijana wasaidiwe kuwa ni watu kadiri ya
mpango wa Mungu. Jamii na Kanisa ni wadau wakubwa katika ujenzi wa
vijana wa kizazi kipya katika medani mbali mbali za maisha. Elimu na
malezi bora yapewe msukumo wa pekee katika maisha ya vijana.
Ndugu Kijana Nazidi kukualika uungane nasi Siku ya Ijumaa tarehe 28/11 mpaka Jumamosi tahere 29/11/2014 kwenye semina Muhimu sana ya Mwaka wa Familia na Elimu ya Ujasiriamali.
Monday, November 10, 2014
Sunday, November 2, 2014
Tabia ya Waamini kuvaa nusu Uchi kanisani
waamnini wanaopenda kuvaa mavazi mafupi kanisani |
Waumini wa kanisa katoliki la St.
Francis mjini Diani kusini mwa pwani ya Kenya walipigwa na butwaa baada
ya baadhi yao kuzuiwa kuingia katika kanisa hilo kutokana na mavazi yao
yaliokuwa nusu uchi.
Julia baraza ambaye alikuwa amevalia kisibao
,ukanda wa manjano na viatu vyenye kisigino kirefu alishangazwa na
sheria hizo mpya ambazo zilimsababisha kukosa misa ya asaubuhi.Kulingana na gazeti la the standard nchini kenya,Julia alisema kuwa watu wawili walimsimamisha nje ya mlango wa kanisa hilo na kumwambia kwamba mtindo wake wa mavazi ulipigwa marufuku katika kanisa hilo na kwamba ametakiwa kuvaa mavazi ya heshima.
Aidha wasichana waliokuwa wamevalia suruali walilazimishwa kujifunga leso juu yake.
Julia alisema kwamba iwapo makanisa yataanza kufuata sheria kama hizo basi wengi hawatahudhuria maombi.
Baadhi ya waumini wamesema kuwa mhubiri wa kanisa hilo aliyejulikana kama Joseph pekee alikuwa ametangaza katika ibada ya awali kwamba mavazi yasio ya heshima hayatakubalika katika kanisa hilo.
Van Gaal aapa kuishinda Mancity (Man City vs Man u)
Meneja wa kilabu ya Manchester
United Louis Van Gaal anaamini kwamba timu yake itatumia fursa ya
kushuka kwa soka ya kilabu ya Manchester City katika uwanja wa Etihad
kuishinda kilabu hiyo.
Kilabu ya Manchester City imepoteza mechi zake mbili za mwisho baada ya kushindwa na West Ham na Newcastle.''Kile tulichokiona katika mechi mbili za mwisho si matokeo ya kuridhisha,alisema Van Gaal.
''Tuna hisia njema kuhusu mechi hii''.''Tunahitaji matokeo mazuri na huenda yakawa dhidi ya Manchester City''.Aliongezea Van Gaal.
Tangu ipoteze kwa mabao 5-3 dhidi ya Leicester mnamo Septemba 21,Manchester United haijapoteza na huenda ikaikaribia Mancity katika nafasi ya nne iwapo itashinda mchuano huu wa 'Derby'.
Hatahivyo ushindi dhidi ya Manchester United utakuwa wa nne kati ya timu hizo mbili hatua ambayo haijaafikiwa kwa takriban miaka 44 na timu hiyo.
Siku ya Marehemu tarehe 02/11(Mungu amewekeza siri ya upendo katika Fumbo la KIFO!)
Kifo
ni kitendawili ambacho binadamu ameshindwa kabisa kukitegua. Anabaki
kuhoji na kujihoji bila kupata jibu la kwa nini anakufa. Mbele ya kifo
binadamu anabaki kutoa visingizio vya kujitetea na kulaumu, hatimaye
anakiona kifo kuwa mwiko
Zamani mwiko ulikuwa masuala ya „mapenzi”, kumbe kifo na misiba hakikuwa kitu cha kuogopa sana. Lakini sasa ni kinyume, mambo ya mapenzi yamegeuka kuwa kitu cha kawaida kabisa isipokuwa kifo kimekuwa kiboko chetu.
Watu tunakiogopa na pengine hatutaki hata kukisikia. Tunapolazimika kwenda msiba basi tunawaachia wengine walipambe jeneza maua, nasi tukisubiri kwenda kutia sahihi kwenye kitabu cha maombolezo na kutoa rambirambi kwenye bahasha kisha kukaa mbani na jeneza huku tukizungumza chinichini. Sanasana tunajisahaulisha kwa kuimba nyimbo za maombolezo au kusikiliza nyimbo za Injili. Tunaogopa kabisa kukizungumzia kifo au walau kukijadili. Mbele ya kifo binadamu tunabaki kulaumiana, kushikana uchawi na hasa tunamlaumu Mwenyezi Mungu.
Mathalani, kuna baadhi ya wakristu wa kale hata wa sasa walisali na kuomba msaada kwa Mungu au kwa kupitia watakatifu fulani kusudi waepushwe na kifo. Sala hizo zinapoacha kupokelewa, binadamu anachukia, na kumlaumu Mungu. Kristu aliwahi pia kulaumiwa pale alipokataa mwito wa Marta na Maria walipomwomba aenda kwao kumponyesha kaka yao Lazaro aliyekuwa mgonjwa. Yesu akaenda huko kwa kuchelewa kusudi siku nne baada ya kifo. Siku ile alipojionesha msibani, Maria na Marta wakamjia juu na kumlaumu sana. “Bwana ungalikuwapo ndugu yetu asingalikufa”. Hata katika nafasi hiyo, bado hatutaki kulijibu swali ni sababu gani Yesu alifika duniani. Je Yesu alifika duniani ili kuendeleza uhai huu wa kibaolojia au kushinda mauti?
Tukitaka kujua ukweli wa mwenendo mzima wa maisha yetu, hatuna budi kuangalia pia hatima yake, yaani kuelewa kwamba maisha yetu yana mwanzo (yaani kuzaliwa) na yana ukamilifu wake. Ama sivyo tutaendelea kukiogopa kifo, nacho kitaendelea kupeta na kutuogofya zaidi.
Ndugu zangu, tulishukuru Kanisa limetutengea mwezi mzima wa Novemba tulioishauanza ili tukitafakari kitendawili hiki cha kifo. Asiyetaka kukitafakari kifo anaonywa na methali ya kiswahili isemayo: “Asiyejua kufa na atazame kaburi.” Kwa hiyo tunaalikwa pia kwenda makaburi mara nyingi kuwaona wenzetu walioishapambana na kifo, nao watatusaidia kutafakari vizuri zaidi fumbo hilo la kifo.
Hebu tujaribu kutafakari kidogo na kupata jibu stahiki juu ya kifo na hatima ya maisha yetu. Tuanze utafiti wetu na Wayahudi, hasahasa manabii na wanazaburi. Wenzetu walianza utafiti mpya juu ya kifo wakitegemeza hoja zao juu ya kitu hiki “upendo”. Yaani kama Mungu aliingia katika mahusiano na binadamu na kufanya naye maagano iwe kwa njia ya manabii wa aina yoyote ile ni kwa sababu Mungu alimpenda binadamu na hivi akataka kuwa na mawasiliano naye. Ukimpenda mtu kwa dhati, huwezi ukamwacha tu kienyeji.
Hiyo ndiyo sheria ya upendo. Kwa hiyo ukisema: “Mungu ninakupenda”, naye akikuambia “Ninakupenda”, basi upendo huo hauwezi kwisha. Namna hii ya kufikiri, ina nguvu sana katika maisha. Katika Agano la kale, Mungu anawaambia wayahudi: “Wewe una thamani machoni pangu, nami ninakupenda” (Isaya). Hapo yaonesha wazi kuwa Mungu anao mradi wa kumpenda kiumbe chake kwa sababu amemwumba. Kwa hiyo katika Injili, tunaona kuwa katika mradi huo, Mungu amewekeza katika upendo kwa njia ya udalali ambao ni yeye mwenyewe katika nafsi ya pili ya Mungu, Yesu Kristu.
Injili ya leo imechukuliwa toka mazungumzo juu ya chakula cha uzima Ekaristi. Mradi huo wa Mungu umeanishwa kwa neno moja tu “Mapenzi”. Neno hilo limetamkwa na Yesu karibu mara nne: “sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu”; halafu, “bali niyafanye mapenzi yake aliyenipeleka”; halafu tena “Mapenzi yake aliyenipeleka ni haya”; na mwisho “Kwa kuwa mapenzi yake baba yangu ni haya”.
Hebu tumwangalie kwa undani Dalali aliyekabidhiwa kutekeleza mradi wa Mungu kwa wanadamu anasema: “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”. Hivi ndiyo Mungu anavyomwaminisha Yesu mradi huo wa mapendo kwa binadamu. Mungu anauaminisha ubinadamu wote kwa Yesu bila masherti. Kwa hiyo ili kuelewa maana ya kifo na ukombozi toka kifo, yabidi tuingie katika mradi huo wa mahusiano ya upendo (mapenzi) na Yesu.
Hoja ya msingi ya kuingia katika mahusiano hayo ni ile anayoisema Yesu mwenyewe, “Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.” Hivi ni dhahiri kwamba Yesu amefika duniani kama dalali ili kutekeleza mradi wa Mungu, yaani kunadisha na kuendeleza mahusiano hayo ya upendo. Mungu amemdhamini Kristu mwanae mradi mzima wa upendo. Kama anavyothibitisha Yesu mwenyewe: “Mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.” Hapo ndipo palipojaa uhondo! Maana yake bila Kristu, hatuwezi kupata jibu sahihi juu ya kifo, jibu linalookoa na kuelewa mwisho au hatima yetu. Na Yesu aliye mdhamini wa mradi huo hataki kujiangusha mwenyewe anaposema, “Katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho” anamaanisha kwamba atatuwapelekesha hao aliokabidhiwa hadi kieleweke.
Kufufuliwa siku ya mwisho, kadiri ya mwinjili Yohane haimaanishi mwisho wa dunia, bali ni Kalvario, juu ya msalaba siku ile anaposulibiwa na kufa. Tendo la mwisho la Yesu la upendo ni pale alipoitoa roho na maisha yake ya kimungu, nguvu ya upendo aliyoitolea yote kabisa wakati wa uhai wake na kuihitimisha pale msalabani. Siku hiyo ya mwisho anaitoa roho yake na maisha yale ya milele yanaingia kwenye mahusiano ya daima na Mungu, na maisha hayo hayana mwisho. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.
Mradi huo unatekelezeka tu endapo tutamtambua Mungu katika Kristu: “Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.”
Maana yake, upendo huo wa Baba utatekelezeka kwa namna tatu: kwanza kwa yule “amtazamaye Mwana,” kumbe yatubidi kuona au kutazama. Kuutazama au kuuona huu mradi wa Mungu na kumtambua Kristu ambaye ndiye mdhamini mkuu wa Mungu. Halafu yabidi “kumwamini Yesu”, yaani kutoa ushuhudi wa binafsi kwa huyo mdhamini pekee. Kisha matokeo ya kumtambua na kuishi kama alivyoishi huyo mdhamini yatakuwa ni “kufufuliwa naye”.
Kwa hiyo katika maisha yetu yatubidi tuyadhihirishe hayo mahusiano ya mapendo na Mungu kwa njia ya Kristu mdhamini wa mapendo. Kwa wale wenzetu walioishazaliwa kwa Baba, yaani waliofariki, wameutambua tayari uso wa Yesu na kumwaminia hivi sasa wamepokea maisha ya kimungu. Kwao hao sisi leo tunawapa ushirikiano kwa kuwa karibu sana nao, na siyo leo tu bali daima. Kama maisha yao hayakuwa makamilifu, sisi tuwaombee yaani kuwaonesha upendo, kwani Mungu amewekeza upendo katika Yesu Kristu.

Saturday, November 1, 2014
Ben Kiko Hatunaye tena!
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana
Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenela Mukangara kuomboleza kifo
cha aliyekuwa Mtangazaji na Mwandishi Mkongwe na Mahiri hapa nchini wa
iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo kwa sasa ni TBC
Taifa, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko.
Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 31 Oktoba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akiendelea na matibabu ya figo baada ya kuhamishiwa hapo akitokea Hospitali ya Jeshi ya Milambo Mkoani Tabora. “Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mwanahabari na Mtangazaji huyu Mahiri ambaye ametoa mchango mkubwa wa kihabari kwa Taifa letu”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba wa Ben Hamis Kikoromo.
“Namkumbuka Marehemu Ben Kiko, enzi za uhai wake, kama Mtangazaji aliyekuwa na mvuto mkubwa kwa wasikilizaji wake kutokana na namna yake ya kipekee ya kuripoti matukio hususan katika kipindi kilichojizolea umaarufu mkubwa wakati huo cha MAJIRA kilichokuwa kikirushwa hewani na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD)”.
Wakati wa vita dhidi ya Nduli Idi Amin wa Uganda mwaka 1978, Ben Hamis Kikoromo alifanya kazi kubwa kwa Taifa kwani aliweza kuripoti matukio mbalimbali kutoka katika uwanja wenyewe wa vita, na hivyo kuliwezesha Taifa na wananchi kwa ujumla kuhabarika vilivyo na matukio yaliyokuwa yakiendelea.
“Kutokana na msiba huu mkubwa, pokea salamu zangu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza mmoja wa Waandishi na Watangazaji Mahiri katika Tasnia ya Habari hapa nchini.
Vilevile kupitia kwako, naomba Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi ziifikie Familia ya Marehemu Ben Hamis Kikoromo kwa kupoteza Kiongozi na Mhimili Madhubuti wa Familia. Nawaomba Wanafamilia wote, ndugu na Jamaa wa Marehemu wawe wavumilivu na wenye subira wanapoomboleza kifo cha mpendwa wao huku wakitambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.
Amewahakikishia Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika muda wote wa maombolezo, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu Ben Hamis Kikoromo, Amina.
Aidha Rais Kikwete ametuma Salamu za Rambirambi kwa Wanahabari kote nchini ambao kwa hakika msiba wa Ben Kiko utakuwa umewagusa kwa karibu. Hata hivyo amesema kuondoka kwa Ben Kiko kusiwe chanzo cha wao kukata tamaa, bali kifo chake hakina budi kuwa chachu katika kujituma zaidi, na wawe tayari kuiga yote mazuri aliyoyafanya Marehemu enzi za uhai wake hapa duniani hususan katika Taaluma ya Uandishi wa Ha

Chelsea, Arsenal safi
*Liverpool waoga kichapo kwa Newcastle
Chelsea wameendeleza rekodi ya kutofungwa baada ya kuwachapa QPR 2-1, Arsenal wakavuna pointi tatu na mabao matatu bila majibu kwa Burnley huku Liverpool wakipoteza mechi.
Chelsea sasa wanaongoza kwa tofauti ya pointi nne, baada ya kufikisha 26 katika michezo 10, wakiwa mbele ya Southampton. Diego Costa alirejea dimbani baada ya kukosekana katika mechi nne zilizopita, lakini hakufunga bao.
QPR walicheza vyema na kuwabana wenyeji, kwani hadi dakika ya 74 mabao yalikuwa 1-1, Chelsea wakaja kubahatika kwa bao la penati la Eden Hazard dakika moja baadaye na kutoka na ushindi. Bao jingine lilifungwa na Oscar wakati la QPR lilifungwa na Charlie
Kocha Jose Mourinho amesema hakufurahia ushindi huo akisema timu yake hawakucheza vizuri, tofauti na alivyotarajia. Kocha wa QPR, Harry Redknapp alisononeshwa na penati iliyotolewa, akisema haikuwa haki.
Katika mechi nyingine Arsenal wamewafurahisha washabiki wao kwa kuwatandika Burnley 3-0 kwa mabao mawili ya Alexis Sanchez ambaye kwa msimu huu amefikisha 10 wakati furaha nyingine ilikuwa kwa beki kinda Calum Chambers aliyefunga bao lake la kwanza tangu aanze kuchezea timu ya wakubwa.
Theo Walcott alicheza kwa mara ya kwanza tangu alipoumia Januari, akichukua nafasi ya Alex Oxlade-Chamberlain dakika 10 kabla ya mechi kumalizika na Arsene Wenger anasema alivyocheza ni dhahiri atarudi kwenye hali yake ya kawaida mapema.
Newcastle wameendelea kufufuka ambapo wamefanikiwa kuwalaza Liverpool 1-0, hali inayozidi kumfedhehesha kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers na kumpa ahueni kubwa yule wa Magpies, Alan Pardew.
Bao pekee la mchezo lilifungwa na Perez Guiterez katika dakika ya 73, ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo wakati Liverpool wamefikisha mechi mbili bila ya kufunga hata bao moja. Watu walikuwa wakimwangalia Mario Balotelli awe mkombozi wa Liver, lakini sasa amefikisha mechi nane pasipo kuzifumania nyavu.

Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...