Saturday, November 1, 2014

masomo ya Sikuku ya Watakatifu Wote 01/11/2014

01
 November
 JUMAMOSI: Sikuku ya Watakatifu Wote. 2014.
SOMO  1. Ufu. 7:2-4, 9-14

Somo katika  kitabu cha ufunuo. 
 Mimi Yohane niliona Malaika mwingine, akipanda kutoka mawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale Malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na Bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.......

Somo katika kitabu cha Yohane wa kwanza. 
2. 1Yoh. 3:1-3
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa; kama yeye alivyo Mtakatifu.


  INJILI.Mt. 21:33-43 
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.

Yesu alipowaona Makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, Heri walio Maskini wa Roho; Maana ufalme wa Mbinguni ni wao. Heri wenye Huzuni; maana hao watafarijika, Heri wenye upole, Maana hao watarithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa Mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; Kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Friday, October 31, 2014

MAFUNZO YA WALIMU WA WALIMU wa UJASILIAMALI


 Mafunzo ya walimu wa walimu "Training of Trainers" kuhusu ujasiliamali yatatolewa kwa Halmashauri za VIWAWA za Parokia za BOKO na BUNJU siku ya Tarehe 08/11/2014 kwenye ukumbi wa Masista wa Karmeli Boko. Mafunzo yamepangwa kuanza saa 2:00 asubuhi. Pamoja na viogozi hao kijana yoyote mwenye nia na anayependa kuhudhuria anakaribishwa.

Tofauti na mafunzo mengine ya Ujasilimali ambayo hufundisha mfano: - jinsi ya kuzalisha bidhaa mbalimbali, mafunzo haya yatalenga katika kumwezesha kijana kutambua na kuzitumia mbinu zifuatazo: -

  • Je unataka kuzifahamu "Sifa 12 za mjasilimali mwenye mafanikio?"
  • Je unafahamu "Kanuni saba ambazo humuungoza mjasiliamali?"
  • Je unafahamu kuwa "biashara/ huduma/ bidhaa inao mzunguko wa maisha  na Ipo misingi ya kubadili biashara/ bidhaa husika iwapo haileti faida yoyote?".
  • Je ungependa "kubuni biashara mpya kabisa?"
  • Je ungependa kufahamu jinsi ya "Kuchagua bidhaa au huduma gani iwe biashara yako?"
  • Jifunze "Mbinu za kuingiza biashara/ bidha/ huduma sokoni"
  • Jifunze kuhusu "Vyanzo vya mitaji"
  • Jifunze kujiandalia mchanganuo wa biashara yako kwa kutumia "Njia rahisi ya kutayarisha mchanganuo wa biashara"

Hizi ni baadhi ya elimu utakazopata katika mafunzo haya na pia mengine mengi katika mfululizo wa mafunzo siku zijazo. Kumbuka Biashara inaishi, hukua na hubadilika, hivyo katika kila hatua mbinu muafaka zinahitajika ili isife.

 Mafunzo haya yamegawanyika kama ifuatavyo: - 40% nadharia na 60% jinsi ya kutenda. Kijana ukitoka katika mafunzo haya ya awali utajengwa kuwa mwalimu ambaye utashiriki kuongeza timu ya walimu wa ujasiliamali. Pia utaweza kubuni biashara yako mwenyewe na jinsi ya kuiingiza kwenye soko lenye ushindani mkali.

Mwana halmashauri, na kijana USIKOSE fursa hii adimu kwa gharama nafuu sana Jiandikishe sasa. Kwa mawasiliano piga simu namba 0713 900 905,0784 799 455, 0765 755 519 na0714 118 788


Mapendo…..



Thursday, October 30, 2014

Semina ya Awali (ujasiriamali na kijana)

Tarehe 08/11/2014, Halmashauri za VIWAWA, Parokia ya Boko na Bunju, Watakuwa na Semina Elekezi ya Ujasiriamali, Itakayofanyikia kwenye ukumbi wa masista Wakarmel Boko
Semina Hii itaanza saa 2:00 Asubuhi, na itaongozwa na Mkufunzi wetu, Mr. Aloyce Dinho, zaidi ya hawa viongozi pia tunawakaribisha vijana wengine wenye uelewa wa elimu ya ujasiriamali au wale ambao tayari wanafanya ujasiriamali.
unaweza kuwasiliana nasi kupitia number hii 0713 900 905. bonyeza hapa endelea kusoma hapa>>>>>>>

Saturday, October 18, 2014

Kesho Dominika ya tarehe 19/10/2014, Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI anatarajiwa kushiriki katika Ibada ya Misa Takatifu mjini Vatican

Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI ni kati ya viongozi wakuu wa Kanisa wanaotarajiwa kuhudhuria katika ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumtangaza Mtumishi wa Mungu Papa Paulo VI, Jumapili, tarehe 19 Oktoba 2014 majira ya asubuhi kwa saa za Ulaya. Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu Benedikto XVI aliteuliwa na Papa Paulo VI kuwa Kardinali.

Hadi sasa kuna Makardinali wawili ambao bado wako hai, hawa ni wale walioteuliwa na Papa Paulo VI wakati alipokuwa analiongoza Kanisa. Hawa ni Kardinali Evaristo Arns na Kardinali wakefield Baum. Haya yamesemwa na Padre Federico Lombardi Msemaji mkuu wa Vatican, siku ya Ijumaa alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mjini Vatican.

Hili litakuwa ni tukio la pili la aina yake kwa Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kushiriki hadharani katika Ibada zinazoongozwa na Papa Francisko, tangu alipong'atuka kutoka madarakani.


 

Maadhimisho ya Siku ya 88 ya Kimissionari Duniani kwa Mwaka 2014

Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa Siku ya 88 ya Kimissionari  Duniani kwa Mwaka 2014.

Mama Kanisa tarehe 19 Oktoba 2014 anaadhimisha Siku ya 88 ya Kimissionari Duniani, iliyoanzishwa kunako mwaka 1926 na Papa Pio wa Kumi na moja na kuanza kuadhimishwa rasmi hapo mwaka 1927 kama siku ya kukoleza ari moyo wa kimissionari katika kuwatangazia Watu wa Mataifa Habari Njema ya Wokovu. Hii ni siku ambayo inaadhimishwa mwezi Oktoba, ambao kimsingi ni mwezi wa kimissionari.
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa maadhimisho ya Siku ya 88 ya Kimissionari Duniani kwa mwaka 2014 anasema kuna umati mkubwa wa watu ambao haujabahatika kusikia Habari Njema ya Wokovu, Familia yote ya Mungu inawajibika kushiriki katika Uinjilishaji kwa kutambua kwamba, Kanisa limeanzishwa na linatumwa kuwatangazia watu juu ya Ufalme wa Mungu.

Hii ni siku ambayo waamini wanaalikwa kushiriki kikamilifu kwa njia ya sala na sadaka yao ili kuonesha mshikamano na Makanisa machanga duniani kama njia ya kumshukuru Mungu kwa neema sanjari na kuonesha ile furaha ya ndani. Yesu anawatuma wafuasi wake na kuwategemeza katika shughuli za kimissionari kama inavyojionesha katika Maandiko Matakatifu pale alipowatuma wafuasi wake Sabini na wawili, wakarudi huku wakiwa wamesheheni furaha baada ya kutangaza kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaandaa watu kukutana na Yesu.

Mitume wanapoonesha furaha yao, Yesu anawataka wafurahi kwa sababu majina yao yameandikwa mbinguni na kwamba, wamebahatika kuyaona matendo makuu ya Mungu yakitendwa mbele ya macho yao! Hii si nguvu ya kutoa pepo wachafu, bali ile nguvu ya upendo ambao wamekirimiwa na Mwenyezi Mungu. Uzoefu na mang'amuzi haya yanakuwa ni sababu ya furaha hata kwa Yesu Mwenyewe kiasi cha kumshukuru Roho Mtakatifu, huku akimtolea sifa Baba yake wa mbinguni, kwani ile siri kubwa kuhusu Ufalme wa Mungu iliyokuwa imefichika inajionesha kwa njia ya Yesu Kristo na ushindi wake dhidi ya shetani.

Hii ni siri ambaye imefunuliwa kwa maskini na wanyenyekevu wa moyo ambao wamebarikiwa mbele ya Mungu. Hawa ni kama Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu, Wavuvi kutoka Galilaya na Mitume wote ambao wamebahatika kushikamana na Yesu wakati alipokuwa anawahubiria watu Habari Njema ya Wokovu.

Baba Mtakatifu anasema, Yesu anaonesha ile furaha inayobubujika kutoka katika undani wake kutokana na ufunuo wa mpango wa Mungu katika kazi ya ukombozi wa mwanadamu, kielelezo cha hali ya juu kabisa cha upendo wa Mungu kwa mwanadamu kwa njia ya Yesu Kristo. Hii ndiyo furaha iliyokuwa inabubujika kutoka moyoni mwa Bikira Maria pale alipomtembelea binamu yake Elizabeti kumshirikisha kuhusu matendo makuu ya Mungu katika maisha yake.

Hii ndiyo furaha inayoendelea kububujika katika maisha ya waamini hadi nyakati hizi, anasema Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa maadhimisho ya Siku ya themanini na nane ya Kimissionari Duniani na kuwawezesha waamini kuingia katika maisha ya Fumbo la Utatu Mtakatifu. Mungu Baba ni chemchemi ya furaha, Yesu Kristo ni kielelezo cha furaha hii na Roho Mtakatifu ndiye mwezeshaji mkuu, changamoto kwa waamini kumjifunza na kumwendea Yesu ili aweze kuwafariji na kuwakirimia maisha ya uzima wa milele, wale wote wanaobahatika kukutana na Yesu.

Wale wanaokombolewa na Yesu, wanaondolewa dhambi, hofu na "jangwa la maisha ya kiroho" kwani kwa njia ya Yesu, daima waamini wanaweza kupata na kuendelea kububujika furaha. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Bikira Maria pamoja na Mitume wake walioamua kubaki pamoja na Yesu ili kushiriki azma ya Uinjilishaji, Yesu akawa ni sababu ya furaha yao ya ndani!

Baba Mtakatifu Francisko anasema ulimwengu mamboleo unakabiliwa na hatari kubwa ya kumezwa na ulaji wa kupindukia unaojikita katika ubinafsi, mambo yanayousononesha moyo wa binadamu kwa kutaka furaha za mpito pamoja na dhamiri mfu. Binadamu anachangamotishwa kujichotea wokovu ulioletwa na Yesu, wafuasi wake wakiwa wa kwanza kuguswa na upendo wake ili kuwa kweli ni vyombo vya Injili ya Furaha, ili kushiriki ile furaha ya uinjilishaji.

Maaskofu wana dhamana ya kwanza kabisa katika utekelezaji wa mchakato wa Uinjilishaji, kwa kujenga na kuimarisha umoja wa Kanisa mahalia na kuendeleza utume wa Kimissionari hadi miisho ya dunia, hasa katika maeneo yaliyoko pembezoni mwa dunia, huko ambako kuna maskini wanaosubiri kwa hamu kubwa kusikia Habari Njema ya Wokovu.

Upungufu wa miito ya Kipadre na Kitawa ni kielelezo cha Jumuiya kukosa ile furaha yenye mvuto na mguso, inayobubujika kwa mwamini kukutana na Yesu kwa kuwashirikisha pia maskini. Hii ni changamoto kwa Parokia na Vyama vya Kitume kuonesha ushuhuda wa udugu unaojikita katika upendo wa Yesu pamoja na kuguswa na shida pamoja na mahangaiko ya maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii. Pale ambapo kuna furaha ya kweli, hapo pia kuna ari na moyo wa kutaka kuwashirikisha wengine, hapo ni mwanzo wa miito mitakatifu. Waamini walei wanahamasishwa pia kushiriki maisha ya kimissionari, ili kutangaza Injili, lakini wanahitaji majiundo makini.

Baba Mtakatifu anasema kwamba, Siku ya Kimissionari Duniani ikuze ndani ya waamini wajibu wa kimaadili wa kushiriki kwa furaha utume wa kuwatangazia Watu wa Mataifa Habari Njema ya Wokovu, kwa kuchangia kwa hali na mali, kwa kutambua kwamba, sadaka hii ni sehemu ya mchakato wa Uinjilishaji wa watu unaobubujika kutoka katika upendo.

Baba Mtakatifu anawataka waamini katika Makanisa mahalia kutokubali kupokwa ile furaha ya Uinjilishaji. Anawaalika kujizamisha katika furaha ya Injili kwa kuirutubisha kwa upendo. Furaha ya mfuasi wa Kristo inajionesha kwa kukaa na Yesu, mwamini anapotekeleza mapenzi ya Mungu na anaposhirikisha imani, matumaini na mapendo ya Kiinjili.

Imehaririwa na
Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S

It was on August 15, 1815 that Saint Gaspar began the Missionaries of the Precious Blood at the abbey of San Felice in Giano, Italy.  Since that beginning, thousands of Missionaries have been inspired by the zeal of St Gaspar and have continued the apostolic work that he began.  It is in recognition of our foundation and in anticipation of the celebration of our bicentennial anniversary in 2015, that the Congregation has begun a three year observance of our founding. 

Download free Ms office here

click here to start download free

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR